Mindyou
JF-Expert Member
- Sep 2, 2024
- 1,869
- 4,877
Wakuu,
Wakati mnaendelea kujadili mchuano kati ya Lissu na Mbowe, viongozi wa CCM wameendelea kutustaajabisha!
=================================================
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Said Mtanda, amemkabidhi pikipiki mpya kijana Kusana Lumambo, aliyegonga gari la mkuu huyo wa mkoa na kuharibu pikipiki yake katika ajali iliyotokea eneo la Mkuyuni, Jijini Mwanza.
Akizungumzia tukio hilo, Mtanda amesema kuwa baada ya ajali hiyo, Lumambo alipelekwa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando akiwa hajitambui na alikaa katika Chumba cha Uangalizi Maalum (ICU) kwa muda wa wiki tatu.
Pamoja na kueleza kuwa kijana huyo ndiye aliyekuwa na makosa kwenye ajali hiyo, Mtanda amesema alihakikisha anapata matibabu ya kina, akilipa gharama zote za matibabu ambazo zilifikia jumla ya shilingi milioni 12.