Pre GE2025 Kijana aliyegonga gari la Mkuu wa Mkoa wa Mwanza anunuliwa pikipiki mpya

Pre GE2025 Kijana aliyegonga gari la Mkuu wa Mkoa wa Mwanza anunuliwa pikipiki mpya

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Said Mtanda amemkabidhi Pikipiki mpya kijana Kusan Alex Dereva Bodaboda ambaye aliligonga gari la Mkuu wa Mkoa huyo October 31 2024 katika eneo la Chakechake Mkuyuni Jijini Mwanza.

Mtanda amebainisha kuwa kwa mujibu wa sheria za usalama barabarani Bodaboda huyo alikuwa na makosa lakini kama Kiongozi aliamua kumsaidia na kumlipia gharama za matibabu kiasi cha Tsh. milioni 12 katika Hospitali ya Kanda ya Bugando pamoja na kumnunulia pikipiki mpya ili arejee kwenye shughuli zake kama kawaida.

..chanzo cha fedha za kununua hiyo pikipiki ni fedha za serikali, binafsi za mh Rc?

..mtu aliyepata ajali akalazwa icu wiki tatu ni salama kurudi tena barabarani kuendesha bodaboda?
 
Back
Top Bottom