Mindyou
JF-Expert Member
- Sep 2, 2024
- 1,869
- 4,877
Wakuu,
Askari wa Usalama wanaomlinda Rais wa Uganda Yoweri Museveni walimzuia mwanaume asiyetambuliwa aliyekuwa akijaribu kumkaribia Rais Museveni katika viwanja vya Msikiti wa Mbogo wakati wa mkutano wa kampeni za mgombea wa NRM, Faridah Nambi anayewania ubunge katika jimbo la Kawempe Kaskazini.
Dhamira ya mwanaume huyo aliyekuwa amevaa fulana yenye picha ya Mtoto wa Kwanza wa Museveni, Jenerali Muhoozi Kainerugaba haikujulikana kama alikuwa na nia ovu au kwa mapenzi alitaka kumkumbatia Rais wake.
Mkutano huo umefayika jana Machi 11, 2025 katika jimbo la Kawempe Kaskazini ambapo Nambi anashindana na wagombea wengine kumi ili kupata atakaerithi kiti cha mbunge aliyefariki Muhammad Ssegirinya’