Kijana amka, hakuna pesa rahisi

Kijana amka, hakuna pesa rahisi

Nasikia Forex, Nadex sijui nini.
Naona wengi wamemezwa na kampeni hiyo waki haidiwa kutajirika haraka.

Nakuasa kijana wangu, hakuna pesa rahisi, kila pesa ina jasho.

Ewe mwenye vipesa vyako vidogo usiingie kwenye biashara ambayo huijui na hujawa tayari kuipoteza hiyo pesa yako.

Huyo anaefanya kampeni ya Forex bado anakuambia analima na kufuga. Bado anakuambia forex inamuingizia mamilioni ya pesa. Kwanini asiachane na kilimo ambacho pesa yake huchukua muda mrefu kurudi?

Forex ni kama betting, ni km kamari tu, unapaswa kuwa na fedha ya ziada ambayo hata ikipotea huko haikuumizi kichwa.

Lakini kama ndio unategemea forex kama biashara yako ikutoe kimaisha, ikulishe, basi unapotea.

Sisemi hivi kwasababu ya chuki, au wivu, bali nakueleza ukweli kwamba usije piga kelele humu kuwa umepoteza muda na.pesa zako huko.

Nakuasa tena kijana, kama umeamua kuwa mfugaji, mkulima, muuza duka, mchuuzi, nk endelea na biashara yako.
Hizi biashara za kuaminishwa kuna ela na kutajirika kwa haraka hamna kitu kama hicho.

Hakuna biashara rahisi, nawachana live, atakae pasuka, nuna, atajua mwenyewe.

Ukweli Mezani.
Naweka Kumbukumbu sawa!!!!

Sent using Jamii Forums mobile app
Nani kakudanganya pesa ya forex ni rahisi? Ukiwa na mawazo mgando hivyo utaliwa. Forex inahitaji dedication na akili na maarifa kuliko unavowaza. Ukiweza hayo yote forex ni biashara nzuri kuliko zote dunian. Huwez uza nyanya na vitumbua. Forex is not get rich quickly. Forex is not for every one.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
We umeshatimiza wajibu wako,yakiwakuta shauri yao.iyo biashara wanaopiga pesa ni waanzilishi ambapo wengine ni wasindikizaji.
[emoji23] [emoji23] [emoji23] hivi hizi akili mnatoa wapi ? hao waanzilishi wa forex ndo akina nani ? kama huelewi kitu sio lazima ucomment

Sent from my iPhone6 using JamiiForums mobile app
 
Hivi hii biashara, ipo 'fully enabled' kwa hapa Tanzania? i.e mhusika anaweza ku-withdraw hizo pesa anazopata?

-Kaveli-
 
Nilitegemea mwishoni uwaase wanaingia kuwa makini lakini ulivyo malizia ni kwa chuki. Humu ni watu wazima sidhani kama kuna ubaya watu wajaribu wanapoona kuna manufaa. Cha msingi ni wao kuongeza umakini zaidi.
 
ONTARIO hii kampeni ya kutukwamisha wana forex haitozaa matunda waache wafungue account zao fake umu JF watachoka wenyewe
 
Wanasema kufikia kiwango fulani cha juu cha mafanikio ya utajiri (pesa na mali ) uwe na vyanzo vya mapato visivyo pungua zaidi ya vitano
 
The greatest risk in life is taking no risk_Robin sharma
A man who is not courageous enough to take risk can accomplish nothing in life_Mohammad Ally
 
Watanzania ni wepesi sana kusahau. Kipindi cha Deci ulikua humwelezi mtu asicheze akakuelewa. Hii thread itabaki kuwa reference.,
*kamari chezesha, usicheze*
mbulula kabisa....Deci unafananisha na Forex? unajua dunia hii hela iko wapi wewe? kweli? ngoja ni log off...
 
mbulula kabisa....Deci unafananisha na Forex? unajua dunia hii hela iko wapi wewe? kweli? ngoja ni log off...
Wewe si ni mpiga upatu wa forex, endelea kuwatafuta wanaotaka pesa bila kufanya kazi. Mungu hakua na akili za mbayuwayu kusema mtakula kwa jasho.
 
Mbona huu uzi ni kama umeandaliwa kumu-attack mtu humu. Nacho fahamu jamaa hakudai kuwa ni utajiri wa haraka haraka ama mimi ndo sikumuelewa vizuri nini mkuu?

Hata hivyo bado ni angalizo zuri kwa kiasi chake.
 
Back
Top Bottom