Kijana anaomba Ushauri kuhusu husiano lake na binti huyu wa Saudia. Mnamshaurije?

story love

Member
Joined
Nov 24, 2025
Posts
7
Reaction score
13
Kulikuwa na kijana mmoja mnyenyekevu mwenye moyo wa upendo na kujali. Alikutana na mwanamke aliyekuwa akifanya kazi Saudia. Kwa maneno, mwanamke huyo alionekana kumpenda kwa dhati.

Alimuita majina mazuri, akaweka jina lake kwenye Facebook na kumfanya ajihisi mtu wa thamani sana maishani mwake.

Kadiri muda ulivyopita, kijana alianza kuona tofauti kubwa kati ya maneno na vitendo. Mawasiliano yao yalikuwa ya kila saa mchana na usiku. Mwanamke huyo hakupenda kusikia kijana ana shughuli nyingine. Akiwa na majukumu au akiweka mipaka kidogo tu, mwanamke alianza kulalamika kuwa ameachwa au kutopendwa. Kijana alipojaribu kupanga ratiba yake, yeye alisema “unanitesa” au “sihisi vizuri bila wewe.”

Lakini pale kijana alipopata matatizo kama simu kuharibika, pasipoti kukamatwa au kuugua, hakuwahi kupata msaada wa maana.

Mwanamke huyo alitoa maneno tu ya “pole” bila kuonyesha jitihada yoyote ya vitendo. Hapo ndipo kijana alipoanza kujiuliza kwa nini mtu anayesema anakupenda hawezi kukusaidia hata kidogo unapohangaika.

Siku moja, mwanamke huyo alimwomba kijana amsaidie kuchukua pesa benki. Alisema atatuma milioni moja kwa ajili ya kumpelekea kaka yake, lakini alituma milioni tatu. Kijana alienda kwa uaminifu, akatoa pesa zote na akampa mtu aliyotumwa kuja kuchukua.

Baada ya kazi hiyo yote, mwanamke alimwachia kijana elfu themanini pekee bila hata shukrani ya dhati. Kijana alibaki kushangaa kama hiyo ndiyo thawabu ya kazi kubwa aliyofanya.

Alipomwambia kuwa aliwahi kuuza kitu ili apate pesa za matumizi, mwanamke huyo alimcheka akisema “kumbe hali ilikuwa serious 🤣🤣.” Maneno hayo yalimuumiza sana.

Mara nyingine, mwanamke ameonyesha tabia za utata kama kukubali kutongozwa kupitia akaunti bandia, kutoa visingizio vya usingizi bila ujumbe, kutosaidia hata kwa kiasi kidogo wakati kijana ana shida na bado kujionyesha kama mpenzi mwaminifu mbele za watu. Akihitaji msaada mdogo wa kifedha, mwanamke huwa mkali au anamkata kauli.

Kwa nje, anaonekana mpenzi mzuri, lakini ndani matendo yake hayalingani kabisa na maneno yake. Kijana sasa amebaki njia panda, moyo wake unahitaji upendo lakini akili yake inamuonya kuwa kuna kitu hakiko sawa.

Anauliza je anapendwa kwa dhati au anatumika tu kama daraja la hisia. Je akipata matatizo makubwa zaidi, mwanamke huyo atasimama naye au atamkimbia.

Vijana wenzangu, mnashauri nini kwa kijana huyu?
 
Pumbavu sana mwanaume mzima unalialia na kuomba hela kwa demu?
Shenzy kabisa
 
Si useme ni wewe!
Achana na hela zake zina kazi!
 
Usipende sana kusaidiwa na mwanamke wako. Usione una haki ya kudekezwa au pesa yake una haki nayo.
Kwa maelezo yako unaonekana unataka kunufaika na kipato cha huyo mwanamke huku ndani yako huna upendo wa kweli kwake.
Tafuta vyako sheikh.
 
Jamaa wewe ni ...... sana,yaani mwanamke anakuonyesha vituko vyote hivyo bado umekaza tu kumung'ang'ania? Embu piga nyeto utaepusha na stress za kiwaki.
 
"Kadiri muda ulivyopita, kijana alianza kuona tofauti kubwa kati ya maneno na vitendo"

Mwisho wa kunukuu

Hapo ndo walianza kuishu kiuhalisia sasa

Cc Smart911
 
Hadithi za kutunga zina raha baadhi ila hii inakera zaidi

Yaani mwanaume unaona kazi kubwa kubwa kutuma bank na unalalamika kabisa eti kazi kubwa
Ndio maana huna hata kipato Bali kusubiri mwanamke achangie maisha yako kama disabled person

Kama ni kuolewa bora utafute bwana wa kukutunza maana hujui majikumu ya mwanaume wewe
 
Kulikuwa na kijana mmoja mnyenyekevu mwenye moyo wa upendo na kujali. Alikutana na mwanamke aliyekuwa akifanya kazi Saudia. Kwa maneno, mwanamke huyo alionekana kumpenda kwa dhati.

Alimuita majina mazuri, akaweka jina lake kwenye Facebook na kumfanya ajihisi mtu wa thamani sana maishani mwake.

Kadiri muda ulivyopita, kijana alianza kuona tofauti kubwa kati ya maneno na vitendo. Mawasiliano yao yalikuwa ya kila saa mchana na usiku. Mwanamke huyo hakupenda kusikia kijana ana shughuli nyingine. Akiwa na majukumu au akiweka mipaka kidogo tu, mwanamke alianza kulalamika kuwa ameachwa au kutopendwa. Kijana alipojaribu kupanga ratiba yake, yeye alisema “unanitesa” au “sihisi vizuri bila wewe.”

Lakini pale kijana alipopata matatizo kama simu kuharibika, pasipoti kukamatwa au kuugua, hakuwahi kupata msaada wa maana.

Mwanamke huyo alitoa maneno tu ya “pole” bila kuonyesha jitihada yoyote ya vitendo. Hapo ndipo kijana alipoanza kujiuliza kwa nini mtu anayesema anakupenda hawezi kukusaidia hata kidogo unapohangaika.

Siku moja, mwanamke huyo alimwomba kijana amsaidie kuchukua pesa benki. Alisema atatuma milioni moja kwa ajili ya kumpelekea kaka yake, lakini alituma milioni tatu. Kijana alienda kwa uaminifu, akatoa pesa zote na akampa mtu aliyotumwa kuja kuchukua.

Baada ya kazi hiyo yote, mwanamke alimwachia kijana elfu themanini pekee bila hata shukrani ya dhati. Kijana alibaki kushangaa kama hiyo ndiyo thawabu ya kazi kubwa aliyofanya.

Alipomwambia kuwa aliwahi kuuza kitu ili apate pesa za matumizi, mwanamke huyo alimcheka akisema “kumbe hali ilikuwa serious 🤣🤣.” Maneno hayo yalimuumiza sana.

Mara nyingine, mwanamke ameonyesha tabia za utata kama kukubali kutongozwa kupitia akaunti bandia, kutoa visingizio vya usingizi bila ujumbe, kutosaidia hata kwa kiasi kidogo wakati kijana ana shida na bado kujionyesha kama mpenzi mwaminifu mbele za watu. Akihitaji msaada mdogo wa kifedha, mwanamke huwa mkali au anamkata kauli.

Kwa nje, anaonekana mpenzi mzuri, lakini ndani matendo yake hayalingani kabisa na maneno yake. Kijana sasa amebaki njia panda, moyo wake unahitaji upendo lakini akili yake inamuonya kuwa kuna kitu hakiko sawa.

Anauliza je anapendwa kwa dhati au anatumika tu kama daraja la hisia. Je akipata matatizo makubwa zaidi, mwanamke huyo atasimama naye au atamkimbia.

Vijana wenzangu, mnashauri nini kwa kijana huyu?
Nilifikiri hapa ni jukwaa la siasa!
 
Baada ya kazi hiyo yote, mwanamke alimwachia kijana elfu themanini pekee bila hata shukrani ya dhati. Kijana alibaki kushangaa kama hiyo ndiyo thawabu ya kazi kubwa aliyofanya.
Tatizo siku hizi Madogo mnaanza Mapenzi hata Condom haziwatoshi (Condom zinapwaya).

Mwanaume unalilia kusaidiwa na Mwanamke, hizi tabia mnazitoa wapi nyie washenzi! Yaani kidume kabisa unaona unastahili kulipwa kwa kwenda kutoa hela Bank, Fakiyu.

Halafu usiseme anafanya kazi Saudia, sema anafanya kazi za ndani. Hio kukuchatisha sana ni UPWEKE na sio Mapenzi, wale mademu huwa wanakuwa wapweke sana, hivyo atakuwa anakutumia kupigia NYETO.

Be a Man, Jifunze kujitegemea.
 
Back
Top Bottom