Habari wanaJF nikiangalia muda huu ni saa tano kasoro ila nimemua kuandika walaka huu ili kutukumbusha vijana kuhusu uaminifu sehemu zinazotupatia riziki.
Nimeamua kuandika JF nikiamini kuwa itakuwa funzo kwa wengine pia mhusika ujumbe utamfikia kwa urahisi zaidi nikiamini kuwa atausoma pia.
Binafsi nimesaidiwa sana na ninaowajua na nisio wajua na wengine pia wakiwa wanaJF ambao tumekutana humu, na tumekuwa tukishirikiana katika mambo tofauti zikiwemo biashara za kujiingizia kipato..
Miezi kadhaa iliyopita niliwahi kuleta bandiko nikihitaji kijana wa kuuza duka langu la mahitaji ya nyumbani ila wakati nikiendelea na mchakato huo nikakumbuka kuwa kuna member mmoja ambaye tunafahamiana kwa muda mrefu kidogo (ni dogo sana) kwa muda ambao tulifahamiana ni kijana niliyetokea kumuamini sana kuliko kijana yeyote niliyewahi kufanya nae kazi.
Kutokana na hali yake ya maisha ilivyokuwa nikakumbuka kuwa hata mm nilikuwa na hali mbaya kuliko hata yeye ila nilinyanyuliwa na nisiowajua na kufikia hapa.
Nikamfanya kuwa mdogo wangu nikimsaidia katika hari zote na kuamua kumpangia chumba kabsa ili aanze maisha na kumuachia biashara yangu ya duka kwa makubaliano kuwa nitakuwa nikimpa 50%ya anachokiingiza.
Alianza kwa kuwa na nidhamu na pesa na kuniheshimu sana na biashara ilienda vizur sana.
Biashara ikakua ila ghafla akabadilika na kuanza kubadili wanawake kama nguo hapo ndo picha la kihindi lilipoanzia..
Anabadilisha simu na kudanganya kahongwa.
Mara chuma ulete wameiba pesa
Muda wote yuko online Whatsp
Anaongea na simu na kuchati masaa 24.
Kufungua badala ya 1 asubuhi akaanza kufungua saa 3
Nilikuja kugundua kuwa dogo ananichapa baada ya kuja na Id mpya Jf akiomba msaada wa kutumia mobile bank ndo kugundua kuwa dogo anapitisha pesa mlango wa nyuma..
Hii Id yake mpya niliigundua baada ya kushika simu yake akiwa amelala na kusahau kulog out..
Maamuzi niliyoyachukua ni kuuza duka jambo ambalo nimelifanya tiyari maana sina msimamizi.
Pili kesho asubuhi namkabidhi mwenye nyumba chumba chake na kumfukuza rasmi ili aendelee na maisha yake...
Funzo. haya maisha kuna muda mwingine huruma haipaswi kuzidi sana .
NB. Kama kama kuna member yeyote kaja hapa dar hana pa kulala au hana chumba nitampa bure hicho chumba akae bure mpaka kodi itakapoisha..
maisha ya leo ni tofaut na miaka ya nyuma, zaman ukiwa mjanja mjanja ndio unatoboa maana weng ni mambumbumbu, sikuhz ukileta ujanja ujanja ktk kutoboa unaonekana boya na inakula kwako sbb karbn kila yule n mjanja ila haoni ni ujanja kutumia ujanja ujanja kutoboa km ww unavyoona,
kwa ufupi ukitumia ujanja ujanja half unayemjanjia akakusoma, ujue sasa huyo ndio mjanja na ujanja wake anautumia vzr.
Wema ni akiba! Ndicho nilichojifunza maishani naweza kuwa na uhitaji flani Ndugu yangu Wa damu asinisaidie lkn nikasaidiwa na rafiki tena Kwa moyo mweupe
Huyo hata angekuibia mamilion hela ya dhukuma haikai na atahangaika weeee Kwa tamaa zake na asipate Wa kumsaidia
Unaweza kuwa na ndugu wa karibu wenye nafasi na wasikusaidie. Nimekutana na jamaa hata simfahamu, amenisaidia na naona mwanga sasa katika maisha yangu.
Tusichoke kutoa msaada, Mungu wa Mbinguni ambariki sana huyu ndugu.
Wema ni akiba! Ndicho nilichojifunza maishani naweza kuwa na uhitaji flani Ndugu yangu Wa damu asinisaidie lkn nikasaidiwa na rafiki tena Kwa moyo mweupe
Huyo hata angekuibia mamilion hela ya dhukuma haikai na atahangaika weeee Kwa tamaa zake na asipate Wa kumsaidia
Nilichojifunza kutokana na uzoefu wa swala kama lako ni kwamba usimpe kula mwenye njaa atakufilisi watu wengi wenye umaskini, dhiki ,shida na njaa hubadilika haswa wanapoanza kushika hela hapo huota mapembe na kuanza kukugawia wewe kiasi cha fedha anachoamua yeye, kwa mtazamo wangu mtu baki ajitafutie mwenyewe kwa nguvu zake...
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.