Kijana badilika uaminifu wako ndo mtaji wako

Kijana badilika uaminifu wako ndo mtaji wako

Hakuna jambo naloliogopa katika maisha yangu kama kupoteza credibility. Vijana tunapotea sana
 
Habari wanaJF nikiangalia muda huu ni saa tano kasoro ila nimemua kuandika walaka huu ili kutukumbusha vijana kuhusu uaminifu sehemu zinazotupatia riziki.
Nimeamua kuandika JF nikiamini kuwa itakuwa funzo kwa wengine pia mhusika ujumbe utamfikia kwa urahisi zaidi nikiamini kuwa atausoma pia.
Binafsi nimesaidiwa sana na ninaowajua na nisio wajua na wengine pia wakiwa wanaJF ambao tumekutana humu, na tumekuwa tukishirikiana katika mambo tofauti zikiwemo biashara za kujiingizia kipato..
Miezi kadhaa iliyopita niliwahi kuleta bandiko nikihitaji kijana wa kuuza duka langu la mahitaji ya nyumbani ila wakati nikiendelea na mchakato huo nikakumbuka kuwa kuna member mmoja ambaye tunafahamiana kwa muda mrefu kidogo (ni dogo sana) kwa muda ambao tulifahamiana ni kijana niliyetokea kumuamini sana kuliko kijana yeyote niliyewahi kufanya nae kazi.
Kutokana na hali yake ya maisha ilivyokuwa nikakumbuka kuwa hata mm nilikuwa na hali mbaya kuliko hata yeye ila nilinyanyuliwa na nisiowajua na kufikia hapa.
Nikamfanya kuwa mdogo wangu nikimsaidia katika hari zote na kuamua kumpangia chumba kabsa ili aanze maisha na kumuachia biashara yangu ya duka kwa makubaliano kuwa nitakuwa nikimpa 50%ya anachokiingiza.

Alianza kwa kuwa na nidhamu na pesa na kuniheshimu sana na biashara ilienda vizur sana.
Biashara ikakua ila ghafla akabadilika na kuanza kubadili wanawake kama nguo hapo ndo picha la kihindi lilipoanzia..

Anabadilisha simu na kudanganya kahongwa.
Mara chuma ulete wameiba pesa
Muda wote yuko online Whatsp
Anaongea na simu na kuchati masaa 24.
Kufungua badala ya 1 asubuhi akaanza kufungua saa 3
Nilikuja kugundua kuwa dogo ananichapa baada ya kuja na Id mpya Jf akiomba msaada wa kutumia mobile bank ndo kugundua kuwa dogo anapitisha pesa mlango wa nyuma..
Hii Id yake mpya niliigundua baada ya kushika simu yake akiwa amelala na kusahau kulog out..
Maamuzi niliyoyachukua ni kuuza duka jambo ambalo nimelifanya tiyari maana sina msimamizi.
Pili kesho asubuhi namkabidhi mwenye nyumba chumba chake na kumfukuza rasmi ili aendelee na maisha yake...

Funzo. haya maisha kuna muda mwingine huruma haipaswi kuzidi sana .

NB. Kama kama kuna member yeyote kaja hapa dar hana pa kulala au hana chumba nitampa bure hicho chumba akae bure mpaka kodi itakapoisha..
Hakika uaminifu ni mtaji tosha maishani..!
 
Dogo boya kweli tena ni mbute iliyooza, badala akae shop kutafuta pesa yeye analeta starehe najua mwisho wa siku ungemfungulia duka lake mbali na kumlipa mshahara.....Watu wanataka kazi hata ya kufagia yeye analeta udwanzi kazini,
Nasema hivi atakukumbuka.
 
Huyu mjinga maisha yake yote atahangaika mafanikio hatokaa ayaone.usually kama hujaweza kusimamia kitu ulichoaminiwa basi kuja kutengeneza cha kwako ukakisimamia mpaka kikaa stable ni shughuli kubwa sana.
 
Dogo boya kweli tena ni mbute iliyooza, badala akae shop kutafuta pesa yeye analeta starehe najua mwisho wa siku ungemfungulia duka lake mbali na kumlipa mshahara.....Watu wanataka kazi hata ya kufagia yeye analeta udwanzi kazini,
Nasema hivi atakukumbuka.
Mkuu sio kufagia tu mimi nilishawahi kuomba kazi kwa malipo ya msosi tu.
 
Back
Top Bottom