Joshua Simon
Member
- Oct 29, 2016
- 6
- 4
Kwenye maisha, lazima ujue nini kusudi lako.
Lazima ujue nini unaweza kukifia ama nini kinakufanya uishi.
Kwakweli wengi wetu tunapumua tu. Tupo hai si kwa kusudi lolote, ni basi tu oxygen inajipitisha mbele yetu na tunapita nayo.
Ni kama tunaiba hii hewa ya Mungu. Kwani kutumia hewa ya Mungu bila kutekeleza kusudi lake si ni wizi tu?
Nani kijana miongoni mwetu anajua asubuhi anapoamka anatakiwa kufanya nini na nini hicho kinachomfanya atoke kitandani asubuhi na mapema?
Leo hii vijana wamegeuka wadudu. Kwani chawa si mdudu?
Unadhani chawa ni wazee? Ni vijana.
Biblia inasema, nimewaandikia ninyi vijana kwa kua mna nguvu. Mnadhani ni nguvu za kiume biblia inaongelea?
Kikubwa Cha kukukumbusha ni hivi, si katika wingi wa miaka uliyoishi thamani yako inaonekana, ni juu ya kile ulichokifanya katika miaka uliyoishi.
©Baba Nasila