Kijana, fanya mambo hayo muhimu kuilinda afya yako

Kijana, fanya mambo hayo muhimu kuilinda afya yako

Poor Brain

JF-Expert Member
Joined
Jul 5, 2019
Posts
19,644
Reaction score
40,546
Hii imetoka kwa mdau mmoja huko jukwaa la afya...

Sawa wakuu hakuna kitakachobaki wote tutakufa.. ila zingatia haya kama kijana mwenzangu ambaye ni hustler

Ile kauli ya kusema magonjwa fulani ya wazee achana nayo.. ila kuna mambo unafanya wewe mwenyewe ambayo ina take long time ku show sign kwenye mwili wako.

Tunanukuu kama ifuatavyo

""Magonjwa mengi ya kuanzia miaka 40+ ni fujo za ujana

Fujo za ujana

Ujana maji ya 🔥 moto, ujana una mambo mengi, wengi huwa tunafeli hapa. Play safe ndugu yangu
Hizo ndo fujo za ujana

SIGARA NA SHISHA- kila kitu kinapozidi huwa harmful hizi sigara ndo hapo badae husababisha Presha, Cancer ya fizi, koo, mapafu, n.k.

POMBE - Pombe bana kama sio mtumiaji sema alhamdullilaah ila kama unatumia basi tumia kwa kiasi badae hapo ukisikia Homa ya ini, Mawe ya kibofu, Presha jua ni zao la pombe

NGONO ZEMBE
-Kumekua na ujinga ujinga sana vijana kushawishiana katika mambo ya ngono. Assume tu kijana ka mimi sitaki mambo mengi nimetulia na antiel lakini kuna watu wa anakuja kuku shauri et pita na huyu au huyu. Ngono zembe ndio chanzo cha UTI ambayo haiwezi kuja kutibika, Ukimwi, watoto wa nje, n.k.

PUNYETO -Hapa siongei sana 😂😂😂😂😂 mara moja moja usiwe kama kina drone yaani wenyewe kwa siku mara 7.
kuna watu now wanasumbuliwa sana na nguvu za kiume, Usahaulifu uliopindukia (ukungu kwenye ubongo)
Unajiuliza mbona huyu mzee anasahau sahau sana kumbe deep down mzee alikua CHAPUTA😂😂😂😂😂

KUENDEKEZA KULA VYAKULA VYENYE MAFUTA HASA VYA KUKAANGWAkula -Hi ndo ilisababisha zamani tujue kuwa kuna magonjwa yanawapata matajiri tu..
kwanini, kutokana na life style yao wanayoishi ya kula haya madude ya ajabu ajabu .. huku wewe pangu pakavu unatamani lakini unakosa unaishia kula michemsho.. hapa kwa vyakula siongei sana namuachia Aaliyyah

Sasa mambo yamebadilika hakuna huu wa maskini au huu wa nani wote tunachezea kipigo. Kutokana na vyakula vya mafuta

KUTUMIA VIFAA VYA ELECTRONICS - Manyanza hapa panakuhusu kabisa unapokua mtu wa kukaa sana kwenye electronics basi jaribu kuwa hata na miwani ya kupunguza mwanga.

Ukishindwa kabisa basi ukipata time angalia rangi ya kijani na blue kwa mda wa lisaa limoja hizi elections matatizo yake hapo badae ni matatizo ya macho, masikio, kupinda mgongo,

SODA, ENERGY DRINKS, GRAND MALT JUISI ZA VIWANDANI NK.-Tumia lakini kwa kiasi mfano kuna sisi ambao tunakunywa zile za kutengeneza na sio za viwandani.

Sometimes unajiuliza kwani hakuna shirika la viwango bongo hapa...?

Jibu ni wapo lakini kiufupi mpaka uwone tbs wametia mguu basi ujue hiyo product kwa binadamu imeleta side effect ya haraka. Nawaza tu.
lakini hii ya gradually wanakaushia tuu masoda hayo ndo chanzo cha kisukari wakuu

KUDHULUMU HAKI ZA WATU KWA MASLAHI BINAFSI.(wizi, utapeli, rushwa, n.k) -all in all acha hayo mambo mana karma is real..

Matokeo yake ni vilio vya uliowafanyia havikuachi salama, kuna namna utalipa hata kama utakuwa tajiri wa pesa.

Kwa kumalizia mdau akasema

Kijana kunywa si chini ya lita 1 ya maji kila siku,hi lita moja ni kawaida sana hata kama unakaa njombe kwenye baridi huko hii lita moja haina shida...

Kama ni pombe kunywa mara 1 au 2 kwa wiki or special occasions, hii ningesema acha kabisa ila naona watakuja kuanzisha vagi..

Kama ni mvutaji wa sigara acha,
Ahahahah sigara jau sana wakuu naona wanangu wa mjani nyie mpo salama jah bless koh koh Koh yao yao...

Hapa pa muhimu sasa

Tafuta mwenza mtulie pamoja haijalishi ni mshangazi au ni nani ila tafuta uishi nae.

Acha kuchovya chovya, acha kula kimasikhara, acha kuteleza...

Haya mambo sio ujanja na hayana tuzo...

Kula sana mboga za majani na matunda, hizi chips na vyakula vya kukaangwa epuka ama punguza sana,

Tafuta sana pesa fainali uzeeni lakini usidhulumu, kuiba, kuua, n.k


Atoto Mpaji Mungu muwe mkipata time mnapitia jukwaa la afya kule wakuu.

Hakuna kitu kina ghalama kama afya,

Afya ndio mtaji....

Wasalaaam 🙏🙏🙏
 
Back
Top Bottom