Mambo yamebadilika, ile dhana ya kusoma kwa malengo ya kuajiriwa imekosa dira, labda kusoma madigrii ya kuajiriwa kwenye nafasi za juu kama ukurugenzi na nafasi za kisiasa ngazi za juu, na wanaosomea hayo ni haohao walioko kwenye ajira tayari wana nafasi.
Hawa wengine kidato cha nne kinatosha, veta ndio mkombozi na uhakika wa kujiajiri katika ufundi. Mfumo wa elimu umebadilika automatically na kuwaacha watunga sera na wanasiasa hoi wasijue pa kuanzia kuweka mambo sawa.