Nyanda Banka
JF-Expert Member
- Mar 14, 2023
- 304
- 1,054
🔹Kuwa kijana huja na Matukio ya kusisimua ambayo yana Changamoto maradufu.
🔹Akili ya kijana hukua Kulingana na namna anavyoshughulikia maisha yake ya kila siku.
🔹 Tafiti Zinaeleza kuwa 75% ya Matatizo ya akili huanzia katika umri wa ujana. Kijana mmoja Kati ya vijana watano huripoti kuwa na Tatizo la akili....
🔹 Ni muhimu kutambua kuwa sio kila Changamoto ya akili itatambuliwa kuwa shida ya Akili, Lakini kila Changamoto inapaswa kuchukuliwa kwa uzito...
🔹 Changamoto ya akili ikiachwa bila kudhibitiwa inaweza kuwa tatizo kubwa zaidi ambalo huathiri afya ya mwili, afya ya Akili, afya ya hisia na Tabia kwa ujumla..
🔹Kijana anapokuwa, huanza Kutumia wakati mwingi pamoja na marafiki zake, katika wakati huu hupata utambulisho nakuwa huru zaidi katika Kufanya Mambo ambayo Ikiwa Hana Maarifa ya kutosha kuhusu Mambo hayo ni rahisi zaidi maisha yake kuharibika Jambo ambalo hupelekea Kupoteza nguvu kazi ya TAIFA....
🔹 VIJANA wanahitaji zana za kuzungumza kuhusu kile kinachoendelea ndani yao, na wanahitaji zana za maarifa ya kijamii ili kukabilana na ushawishi wa marafiki wabaya wanapowafikia....
🔹Utafiti unaonyesha kwamba vijana wana uwezekano mkubwa wa kuzungumza na marafiki zao kuliko watu wazima kuhusu matatizo wanayokabiliana nayo.
🔹Ni kupitia Mazungumzo haya VIJANA wengi maisha yao yameharibika kwa sababu ya Ukosefu wa maarifa ya udhibiti wa Hisia(Emotional Control) pamoja na stadi za Maisha(Life skills) kutokana na ushauri wa Aina ya marafiki waliopo katika mduara wa maisha yao.....
🔹 Ukisoma Maandiko Matakatifu utagundua kuwa chanzo Cha uharibifu wa Maisha ya Amnoni Baada ya kumbaka Dada yake Tamari ni Ukosefu wa maarifa ya udhibiti wa Hisia pamoja ushauri mbaya aliopokea Kutoka kwa rafiki yake Yonadabu. (Soma 2 Samwel 13)
🔹 Ni muhimu Sana kuzungumza na vijana kwa lugha yao kuhusu Changamoto wanazoweza kukabiliana nazo wanapokua na kuvuka ujana..
🔹Vijana wanahitaji kujua Elimu ya udhibiti wa Hisia, wanahitaji kujua Elimu ya Stadi za Maisha, Wanahitaji kujua Elimu ya Mahusiano, Wanahitaji kujua Elimu ya ugunduzi wa uwezo uliopo ndani yao katika kuishi Kusudi la maisha yao ...
🔹Tunaweza kuandaa vijana wenye nguvu kubwa ya kufikiria katika kutatua Matatizo yaliyopo katika jamii zetu, Kama ilivyokuwa kwa Wale vijana Wanne katika Maandiko Matakatifu ( Daniel, Shadrack, Meshack na Abednego)...(Soma Daniel).
🔹Ni muhimu Kufanya uwezekezaji wakufao kwa vijana katika kujifunza maarifa muhimu ya Maisha ikiwemo udhibiti wa wa Hisia, stadi za Maisha, Elimu ya Mahusiano, pamoja na ugunduzi wa uwezo wao wa asili uliopo ndani yao...