Mkalukungone Mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 3,141
- 7,205
Kijana msomi na mtaalamu wa masuala ya udhibiti wa bidhaa za tiba, Japhari Saidi, ametangaza rasmi nia yake ya kuchukua fomu kuomba kuteuliwa kugombea Ubunge wa Jimbo la Singida Mjini kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), katika Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika mwaka 2025.
Akizungumza baada ya kutangaza nia yake, Japhari amesema kuwa ameamua kujitosa katika kinyang’anyiro hicho ili kutoa mchango wake katika maendeleo ya wananchi wa Singida Mjini kwa kutumia uzoefu wake katika utumishi wa umma, taaluma na ushirikiano wa karibu na jamii.
“Ninaamini kuwa Singida Mjini inahitaji mwakilishi mwenye maono mapana, anayejua changamoto za wananchi, na mwenye uwezo wa kushirikiana na serikali pamoja na wananchi katika kuleta maendeleo ya kweli,” amesema Japhari.
Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
Japhari ni mzaliwa wa Kata ya Utemini, Singida Mjini. Ana Shahada ya Kwanza ya Kemia kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), na Shahada ya Uzamili ya Sayansi ya Bioteknolojia na Udhibiti wa Bidhaa kutoka Purdue University, Marekani. Kwa zaidi ya miaka 10, amekuwa akihudumu kama Mkaguzi Mwandamizi wa Dawa katika Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA), akihusika na usalama na ubora wa dawa katika soko la Tanzania.