Kijana mtafutaji, ukijenga Dar unaulazimisha umasikini uendelee kuwepo mlangoni mwako

Bwawani ni km ngapi kutoka Moro town? Uelekeo wa Dom,Iringa au Dar kutokea round about ya Msamvu.
Kwa kilomita nitakudanganya ila bodaboda huwa napenda tsh 15k kutoka msamvu hadi bwawani..so unaweza kukadiria..ni njia ya Dodoma...
 
Maisha yanabadilika sasa hv mikoani kuko fresh tu dar usumbufu sana
 
Kosa ulilifanya kwenda kujenga Chanika huko hata ukisema uipangishe hiyo nyumba kama ni ya familia humpati mtu wa 200K huko ni kwenye (ashakum si matusi) makalio ya mji,Chanika ni mbali na jamii inayokaa kule sometimes ni kama ya vurugu vurugu ukiwa mtu mpenda utulivu utapata sana shida.

Na wengi hukosea tangu kununua viwanja wanaangalia urahisi wa bei mpaka tunapojadiliana hapa huko Chanika kuna viwanja vya Tsh 1.6mill ukubwa 20x20 lakini ukienda uelekeo wa Morogoro road size hiyo hiyo utaambiwa Tsh 8mill Kibaha sasa hivi 20x20 vinafika 5mill na ukijenga nyumba ina soko sababu infrastructure ya kuingia town ni rafiki na kila siku inaboreshwa.
 
Huwa nawaambia vijana wahindi sio wajinga kupanga town always, jenga nyumba yako pangisha then ww kaishi karibu na mishe mishe zako au kama habari za kupanga kwako hutaki basi tafuta pesa kwa bidii muamishe mtu mfano sinza pale unamuamisha mtu unajenga nyumba yako unayotaka ww ukiwa karibu na harakat zako za utafutaji!
 
Hakuna mtu anaeweza kumhamisha mtu Sinza ili ajenge nyumba yake ya kwanza aishi. Mtu mwenye uwezo wa kumhamisha mtu Sinza anakuwa ashapita level za nyumba ya kwanza ya kulala.
 
Kuishi Dar es Salaam angalau uwe na usafiri wako binafsi walau ata pikipiki.
 

 
Mkuu pole sana. Wewe ndio ulichemka. Kujenga Dar ukimaliza basi wewe maisha umeyapatia mno.

Na ulienda kujenga mbali kutokana na kipato chako kidogo.
 
Ujenzi wa Dar ni rahisi kwa ghalam ukilinganisha na baadhi ya mikoa hapa TZ kama Mwanza
 
Nimekuelewa mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…