Kijana mtafutaji, ukijenga Dar unaulazimisha umasikini uendelee kuwepo mlangoni mwako

Viwanda vyote na maduka ya jumla ya vifaa vya ujenzi yapo Dar, bei haiwezi ikalingana, lazma Dar itakua chini. Nini hasa kinachofanya ghalama ya ujenzi wa nyumba ya ramani moja Dar ikawa kubwa??
Endelea tu kubisha
 
Bingwa
Usisikilize ushauri wa walugaluga wa maporini huko mikoani
Wewe ni mkazi wa Dar es Salaam, Wilaya ya Ilala
Na kama umejenga nyumba yako,umemaliza , wewe sio tena wa mikoani
Pambana hata upate pikipiki, usiogope kuendesha, utakula mema ya nchi
Halafu hata hauko mbali na Masaki B

 
Viwanda vyote na maduka ya jumla ya vifaa vya ujenzi yapo Dar, bei haiwezi ikalingana, lazma Dar itakua chini. Nini hasa kinachofanya ghalama ya ujenzi wa nyumba ya ramani moja Dar ikawa kubwa??
Mbona aihitaji hata degree kifikiria? Hizo material za kutengenezea vifaa vinatokea wapi? Hivi bei ya tofali dar utalinganisha na moro au iringa? Hivi gharama ya fundi unaweza linganisha na fundi wa dar?

Acha ubishibi usio na faida
 
Hongera kwa kujenga. Ushauri umeshajipa hapo juu, pangisha huo mjengo na wewe nenda kapange karibu na mishemishe zako.

Mji unakuwa huu, siku moja hapo ulipojenga thamani yake itaongezeka maradufu. Dar ni Dar tu. Waliojenga Kimara walichekwa leo hii ndio baba wenye nyumba wenye viburi vya kuchukua kodi wanayoitaka wao.
 
Nilikaa Chanika mwenyeji wangu alikua na gari. Nikabadili mtazamo, hakuna mahali ni mbali kama una usafiri. Na gharama hazikimbiwi tafuta namna ya kuongeza kipato kuzikabili.
Hapa unamaanisha Jamaa anunue Gari la kwake sio kudandia Boda na Gari za kupangwa kwa kuminywa km maparachichi
 
Chanika ni sehemu ya ovyo sana, wanajenga ovyo ovyo, wanazaana ovyo ovyo
yaani miaka michache ijayo Vingunguti ikasome
Kule kuna wenyeji na wakuja na hapo kabla watu walikua wachache mno miaka ya 2000 Ila nenda leo 2024 ulienda Mwaka 2000 utapagawa sio Chanika Ile soon patakua na flyover pale Chanika mjini
 
Kwanza ni mbali kinoma huko CHANIKA, mziki wa kutoka GOMZ hadi ufike Chanika si haba..

Huko kwa mtu mwenye kipato cha kati si pa kuishi.. kwanza watu wengi wanaokaa huko ni tabaka fulani la waswahili.. pia mpangilio sio kabisa mtu ana laki mbili tyr kapata kiwanja unategemea nini?

Pia wale waliohamishwa vinginguti etc wamejazana huko..

Ni kheri utafute sehemu Tabata Kinyerezi at least ingawa napo hapashikiki huko.
 
Wewe ni masikini ,u za hicho kibanda
 
Hayo maeneo ya bei rahisi huwa yanakuwa ya kijinga mwanzoni ila ndo hujazana wapiga kura wengi. Unajua nini hutokea sehemu yenye wapiga kura wengi? Miaka inavyozidi kwenda hugeuka maeneo ya biashara sababu ya idadi ya watu na watawala wa vyama vya siasa huwa wanataka kura.
 
Tafuta pikipiki itatatua 60% ya changamoto ulizonazo
 
Kama unalalamika kwa nauli ndogo hiyo wewe dar hapakufai. Na huko umejenga kijumba na sio nyumba.

Dar pesa ipo, kutumia nauli ya laki kwa siku ni kawaida tu. Kikubwa tutabanana hapahapa
 
Nimemkumbuka jamaa aliyehamia Kerege.

Tuambiane ukweli tu kuna sehemu wanapaswa kuishi wastaafu au uwajengee wazazi wako wakae hapo.

Kujenga nyumba si lazima ukae hapo, au kujenga nyumba si kwamba unamkomowa baba mwenye nyumba, wewe ukihama mpangaji mwingine anaingia.

Tujifunze kwa wahindi na Waarabu hawa hawakaagi mbali na town, either akae town kabisa au kilometer 3 tu nje ya town.

Tujifunze kwa wenzetu waliotuzidi maarifa.

Namshukuru Mungu mimi nikiamuwa kwenda town kwa mguu nakwenda bila tabu, nikiwa na harak bodaboda buku 3 tu.
 
Hakuna mtu anaeweza kumhamisha mtu Sinza ili ajenge nyumba yake ya kwanza aishi. Mtu mwenye uwezo wa kumhamisha mtu Sinza anakuwa ashapita level za nyumba ya kwanza ya kulala.
Tafuta hela kijana ndo utaelewa! kuna watu wana goals zao we hujawahi kuona mtu ndo nyumba yake ya kwanza lakini ni ghorofa la kutisha??
 
Tafuta hela kijana ndo utaelewa! kuna watu wana goals zao we hujawahi kuona mtu ndo nyumba yake ya kwanza lakini ni ghorofa la kutisha??
Acha stori za kufikirika wewe. Mtu anazungumzia kujenga Chanika huko unaleta stori za kuhamisha watu Sinza. Mtu wa kuhamisha mtu Sinza hayuko level za nyumba ya kulala. Take that to the bank.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…