Kijana mtafutaji, ukijenga Dar unaulazimisha umasikini uendelee kuwepo mlangoni mwako

Wewe unataka kuishi town kodi ya laki 5 kwa mwezi unayo? Ofisi nyingi zinafunguliwa saa 08 mpaka 08:30 ,sasa chanika unatoka saa 9 usiku unafika ofisini saa ngapi? Sasa Elfu 4 kwa siku 24 si elfu 96 tu? Wenye magari wanaoweka mafuta ya elfu 15 hadi 25 kwa siku nao wasemeje? Kwahiyo ukipanga mjini ndiyo utakuwa unaenda kwa miguu ofisini hautumii nauli?
 
mkuu nimekuelewa, ila umenikaripia sana...
 
mkuu nimekuelewa, ila umenikaripia sana...

Hapana ,natoa facts kwa wengine ,watu wanakaa Kibaha au Bagamoyo wanafanya kazi posta! Kwa mfanyakazi unatakiwa uwe active,kulalamika kwamba unaamka saa 9 usiku unaona kama kero wakati kuna wengine wanalala saa 4 tu kwa siku saa zilizobakia wapo macho!

Ukitaka kufanikiwa inabidi uaamke mapema sana na kchelewa kulala .kama unajitafuta unaona tabu kuamka basi una safari ndefu sana ,kama upo dar siku nenda ukae bahari beach angalia watu wana ma V8/Vogue Autobiography/Brabus saa kumi wapo barabarani wanawahi mishe ,mwenzangu na mimi hata Fan Cargo huna unalalamika kuamka saa 9.

Kama nauli ya elfu 96 kwa mwezi unaona ni nyingi basi acha hiyo kazi haina manufaa utachelewa sana kufika malengo.
 
Hao wengine ni kuachana nao tu lengo n kutaka kuponda wanaojenga chanika wote hawana akili sio kama anasema n mbali watu wanakaa mkuranga wengine mlandizi na wanapiga mishe mjini posta au kariakoo kila siku ss yy analalamika nauli elfu 2 ivi mtu ka huyu ana akili kweli hata akija kuwa baba wa family iyo family itakuwaje anafikiria kwenda kujenga mikoani wakat anafanya mishe zake dar izo n akili ss
 
Dalili za umasikini ni pamoja na kuwa na milioni kumi na tano na kufikiria kununua kiwanja na kujenga
 
Acha stori za kufikirika wewe. Mtu anazungumzia kujenga Chanika huko unaleta stori za kuhamisha watu Sinza. Mtu wa kuhamisha mtu Sinza hayuko level za nyumba ya kulala. Take that to the bank.
Zaidi ya 18 yrs nipo Dar ila sijawahi hata kuwaza kuishi Sinza, Magomeni wala Keko maana ni maeneo ambapo mvua ikinyesha ni balaa tupu, ni vile tu umaarufu wa maeneo hayo upo kwa kuwahi kujengeka na biashara kabla ya miji iliyoibukia hivi karibuni kama Tabata, Kinyerezi, Kimara na Mbweni.

Ubinadamu ni kazi/The humanity is a work.
 
Pole sana
 
Maisha ya dar kwa sasa hivi, kuanza kujenga kabla ya kindinga ni uongo mtupu.
 
Kweli kabisa !
Dar Acha wajenge matajiri !
 
Miaka mitano ijayo Hii comment yako juu ya kerege uenda ukatamani uifute, mimi nimejenga pale mapinga mwaka 2012, nilijilaumu sana,japo bado najilaumu ila si kivile, ila kwasasa hayo maeneo kumekucha mkuu, japo kodi yake hailizishi sana
 
Mimi nakaa Kerege Bagamoyo, kila siku naenda Kawe kwa mishe zangu, mambo yanaenda japo ninapanda magari mawili kila siku. Kwako ni kwako, choo chako na familia yako. Ila inategemea kipato chako kwa siku ni ngapi.
Kerege na kawe karibu sana mkuu,
 
Points tupu.
 
Uza ukajenge huko kwenu mkuu? Bado mbona una machaguo mengi. Au kaza tena ununue gari halfu uanze kusema msinunue magari hata kama ni toyota cc ndogo, gharama za mafuta zinaumiza 😆

Unaweza pangisha kisha ukarudi mjini karibu na kazi zako kupanga mkuu.

Thamani ya kiwanja na nyumba yako inaongezeka mkuu, umefanya jambo zuri, sasa nyumba inayofatia anza kujenga huko unaposema.
 
Kuna mwenzako pia kajenga mkoani sehemu ambayo haitoi mrejesho mzuri kiuchumi nae anawaza angejenga Dar anapofanyia kazi.

Kwa zama hizi sidhani kama kuna haraka ya kujenga makazi, kukuza kipato inapaswa kuwa lengo kuu zaidi, ndio vile tena hatujifunzi na hatufundishwi. Kama kiwanja bado kinaruhusu fanya projects hapo, jenga hata greenhouse ya nyanya au mboga za majani, ila fanya utafiti kidogo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…