CIA mgumu
JF-Expert Member
- Aug 8, 2022
- 962
- 1,934
Shikamoni wakubwa na wadogo zangu habarini za mda huu.
Naomba niende kwenye mada tajwa hapo juu kuwa "kijana mwenzangu wa kitanzania usisubiri kutafutiwa maarifa zaidi bila mwenyewe kuweka bidii katika kuongeza maarifa".
Kwanza kabisa nataka kuongea na vijana ambao wamebahatika kusoma kozi za tehama na ambao kwa namna moja au nyingine walipenda kusoma kozi hizo, kumekuwa na changamoto kubwa kwa vijana wengi kwenda chuoni na kusoma kozi hizo ambazo ukiziangalia kwa jicho la ndani ukizisoma na kujiongezea maarifa mwenyewe na ukawekeza nguvu akili mda mwingi katika kutafuta au kujiongeza zaidi na kile ulichofundishwa na mwalimu nina unahikika hutakaa uwaze ajira kamwe maishani mwako.
Nazungumza haya nikiwa na uhakika maana nina kampuni yangu inayohusika na utengenezaji wa mifumo ya computer na vingine vinavyohusiana na tehama, hivyo nimekuwa mwajiri, lakini kinachonisikitisha ni kijana mwenye shahada ya software engineering au computer science na mda mwingine akijinasibu na cv nzuri kuwa yeye ni programmer mzuri web developer mzuri lakini ukimwambia nina kazi hii naomba uifanye hapo ndio utajua ukweli wa mambo kuwa chuoni hakujiongeza wala kutafuta maarifa zaidi yeye aliwekeza katika kutafuta ufaulu mkubwa zaidi na sio kubobea katika kile alichokisomea.
NINI KIFANYIKE ILI KIJANA UNAESOMA KOZI ZA TEHAMA UACHE KULALAMIKA KWAMBA HAKUNA AJIRA:
Kama ni kweli mwenyewe uliipenda tehama na ukaamua kusoma mojawapo ya hizo kozi basi naomba nikufumbue macho, kuwa hakuna chuo kizuri au darasa zuri au mwalimu mzuri wa kukufanya wewe uwe nguli katika taaluma ya Tehama, tumia mda wako vizuri uwapo masomoni, tumia akili yako vema uwapo darasani, tumia maarifa yako vizuri kujiongeza tofauti na ulichofundishwa darasani.
Hakikisha upatapo nafasi ya kuwa na Internet hakikisha asilimia 90% ya matumizi yako katika mitandao ni kutafuta kitu kipya na kujifunza katika tehama, hakikisha hupotezi mda kwa vitu visivyokuwa na msingi nje ya kozi yako, hakikisha kutumia maarifa kidogo ulionayo kujiongeza na kuyatafuta makubwa zaidi, jenga urafiki na waliokuzidi katika maarifa kwenye kozi za tehama kuwa mnyenyekevu, jishushe penda kujifunza kitu kipya kila mara.
Namaliza kwa kusema kuwa hata ukienda kusoma Harvard University or Yale University kama utabaki na akili za kwenda kutafuta ufaulu mkubwa na kutojiongeza basi utarudi na cheti na cv nzuri sana huku kwenye utendaji ukiwa sifuri, Mungu wa mbinguni awafungue akili kijana mtanzania mwenzangu.
NAOMBA KURA YAKO

Upvote
11