Tetesi: Kijana mweusi aibuka na kudai yeye ni mtoto wa Bill Clinton, adai kufanyiwa DNA

KWEZISHO

JF-Expert Member
Joined
Jan 29, 2016
Posts
7,519
Reaction score
6,518

Kijana mweusi Danney Williams anayedai kuwa mwanawe rais wa zamani wa Marekani Bill Clinton, ameomba kufanyiwa vipimo vya DNA.
Williams aliwasilisha ombi hilo wakati mkutano aliofanya na vyombo vya habari katika mji wa Washington na kudai kwamba mgombea urais wa chama cha Democrats Hillary Clinton ni mamake wa kambo.
Katika maelezo yake, Williams alisema, ''Mimi ni mtoto wa Bill Clinton. Hillary Clinton ni mamangu wa kambo na Chelsea ni ndugu yangu.''
Kijana huyo anayeishi katika jimbo la Arkansas alitoa ombi la kufanyiwa vipimo vya DNA ili kuthibitisha madai yake.
Williams aliongezea kusema kwamba amekuwa akihangaika kufuatilia suala hilo tangu mwaka 1990 ili kutafuta uthibitisho.
Akibainisha kumpoteza mamake mzazi aliyeathirika kwa madawa ya kulevya tangu alipokuwa na umri mdogo, Williams aliitaka familia ya Clinton kuwasiliana naye.
Kwa upande mwengine, Williams alikanusha madai ya kusaidiwa na Donald Trump na kusisitiza kuwa alisimamia gharama za wakili mwenyewe huku akifahamisha kwamba madai yake hayana uhusiano wowote na uchaguzi mkuu ujao.
Chanzo: Blogu ya Siasa Huru
 
Tutake radhi wewe watu weusi, huyo siyo mweusi bali ni Mchotara kwa maana Baba yake ni Mzungu hivyo hawezi kuwa mweusi!
 
USA wanafiki sana, ila sijui yupi sahihi maana wote ni ibilisi tu
Ingawa kipindi cha uchaguzi kuna mambo mengi yanaibuka, ni lazima kuwa waangalifu katika kupokea taarifa na kuzifanyia kazi. Mzee Clinton anaweza kujitokeza na kupima DNA ili kuupata ukweli.
 
Tutake radhi wewe watu weusi, huyo siyo mweusi bali ni Mchotara kwa maana Baba yake ni Mzungu hivyo hawezi kuwa mweusi!
Naam ni kweli ni Mchotara. Sasa huyo ni chotara wa kizungu au kiafrika?
 
Kweli pua na macho kwenye eneo la kope chini ni MUTATIS MUTANDIS
 
Kuna problem kwa hillary inapokuja swala la six times six times far.
Inambidi bill kucheza mechi za mchangani.
Ni fikra tu wakuu.
 
Naam, mzee alikuwa anacheza sana mechi za mchangani. Wakati mwingine hata kama mko bize kiasi gani kuna umuhimu wa kutenga wasaa wa uumbaji.
Tunajua binaadamu tunatofautiana kuhusu kiasi na uwezo mujarabu wa kuridhishana katika tendo la ndoa hapo ndipo utaona huyu anachepukia mchangani na yule anabaki njia kuu.
 
Atakua muongo huyo,kapewa mshiko na mtandao wa Trump

Jamani msitake kumzulia kijana wa watu, madai haya yalikuwepo kwa miaka mingi tu hata kabla ya Clinton a jawa Rais - mleta mada aneweka picha mbili tu lakini mimi niliwahi kuona picha zaidi ya ishirini tangu yupo mtoto mdogo mpaka utu uzima, huyu kijana anamfanana sana Clinton kwa sura tofauti ni nywele na kwa mbali ragi ya ngozi - lakini mambo mengine ni copyright kabisa. Na mama yake alieleza walivyo kutana na Clinton wakati huo akiwa na Governor wa Arkansas.
 
Back
Top Bottom