Pre GE2025 Kijana Mzalendo CCM: Tundu Lissu na Heche Ndio Majabali wa siasa Tanzania, ni Game Changers. Wananchi wote tuwaunge mkono bila kujali vyama

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Bush Dokta

JF-Expert Member
Joined
Apr 11, 2023
Posts
24,831
Reaction score
45,154
Huyu jamaa anayejiita Kijana Mzalendo amethibitisha uzalendo wake kwa kuweka siasa za maji taka pembeni na kujikita kwenye siasa za Tija.

Ameongea mambo mengi Muhimu sana kuhusu siasa za Tanzania lakini moja ktk mahojiano yake yamevuta Attention Kubwa Nchini.

Kwanza izingatiwe kuwa huyu si Mwanachama wa vyama vya upinzani bali ni CCM Damudamu.

Miongoni mwa Yale aliyohight ni kama ifuatavyo.

1. Tundu Lissu ni Jabali la siasa na Game Changer kwa sasa. Ni mzalendo.

2. Heche ni Mwanasiasa za Kizalendo na Mtetezi wa Rasilimali za Umma na Taifa
3. Tundu Lissu alithibitisha kile alichoamini na kushauri enzi za Makinikia pale Taifa liliposhtakiwa na kushindwa hadi kulipa faini ya mabilioni ya Kodi za Wananchi.

4. Tundu Lissu ni Mwanasiasa peke ndani ya Upinzani, ccm na hata serikali anayeweza kukemea Rushwa hadharani kwani hana Harufu wala dosali ya rushwa. Anajiamini.

5. Heche ni Mkali mwenye Busara, Upendo na anaipenda Nchi yake.
6. Tundu Lissu ni Mwanasheria aliyebobea na kujua kutumia taaluma yake kwa ajili ya Wananchi.

7. Tundu Lissu alipigwa risasi kutokana na uzalendo na misimamo yake.

8. Tundu ataimarisha upinzani, ccm na serikali pia vitafanya kazi.
9. Wabunge wa ccm hawana msada bungeni. Kila kitu kwao ni ndiyo tu. Hawana mtu wa kuwaamsha. Wako kwa maslahi yao tu.

Mwisho kabisa Tundu Lissu anafaa kuww Rais Wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.


View: https://youtu.be/Hip7RunpX8Y?si=Dru3yL0s6Nwl7xyg
Anamalizia kwa kusema Vyama vya siasa ni taasisi za umaa vinatumia Ruzuku Pesa za Walipa Kodi si vibaya kuvifatilia hata kama sio mwana chama wa chama.

Ni mali zetu hatufungwi kuviongelea.
 
Ukiangalia wale Wazalendo wote waliobakia huko CCM wanataka Lissu awe Mwenyekiti wa CHADEMA lakini yale mazezeta yenye low IQ yaliyojaa huko CCM yanataka Upinzani ufe kabisa Nchini kwasababu yameambiwa kuwa ati Wapinzani ni adui wa Taifa😆😆
 
Wewe inaonekana hujui kinachoendelea.wenzako wanawaza mbali sana.Jakuna mzalendo yoyote ccm wote wanawaza kunufaika badae.
 
Hahaha
 
CCM bado wapo Wazalendo sema wamezidiwa na WalaRUSHWA ambao ndio wanashikilia hatamu.
Lakini hao wala rushwa itakuwa wana nguvu sana. Tangu tumewasema hawateteleki nani anawalinda?
 
Lakini hao wala rushwa itakuwa wana nguvu sana. Tangu tumewasema hawateteleki nani anawalinda?
Ndio hao wanaoiambukiza CHADEMA RUSHWA hao ambao wanatuma Watoto wao kuja kwa Viongozi wetu wa CHADEMA na mabulungutu.

...of course wananguvu ya pesa za rushwa na wametajirika kwa muda mfupi sana.
 
7. Tundu Lissu alipigwa risasi kutokana na uzalendo na misimamo yake.

Mkuu Bush Dokta maneno ya huyo mzalendo yamekaa vizuri, naomba tu nikazie hii zaidi namba 7 uzalendo uliopitiliza
 
7. Tundu Lissu alipigwa risasi kutokana na uzalendo na misimamo yake.

Mkuu Bush Dokta maneno ya huyo mzalendo yamekaa vizuri, naomba tu nikazie hii zaidi namba 7 uzalendo uliopitiliza
Kijana mzalendo hakutaka kupinda pinda....Amenyooka.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…