Kijana mzalendo kuiburuza serikali mahakamani mkataba DP

Samia kiumbe wa ajabu sana, hivi mpaka leo bado anaamini kuna mtanganyika mwenye akili timamu anayemuunga mkono kwenye ule mkataba wa hovyo wa bandari?

Hayupo.

Hata hao wanaomuunga mkono, ni kwa ajili ya matumbo yao tu, sio uungwaji mkono wa 100%
 
*Mungu akutie nguvu #David Levi Nkindikwa Esq, umma wa Watanzania milioni 53 kati ya 60 ambayo ni asilimia 88.3% wanaunga mkono jitihada za kukosoa kusudio la mkataba huo wa DPW wenye vifungu tata dhidi ya rasilimali na njia kuu za uchumi wa nchi. Umeonesha njia ukiwa kijana bila kujali madhara ya wale unaowakabili kwa faida ya taifa la Tanzania (Tanganyika). Tumia weledi wako katika taaluma ya sheria za ndani na za kimataifa kuhusu uwekezaji na biashara za kimataifa kutetea uhai wa taifa na leo na kesho.

Ipo siku viongozi wote wa serikali wanaoshiriki mchakato huu kuja kufunguliwa mashitaka ya uhujumu, utakatishaji fedha na uongozaji magenge ya kiharifu dhidi ya mali za umma.
 
Ndugu yangu kama inafanya kazi, unapata pesa ni Bora TU ukajikuta kwenye shughuri za kukuingizia kipato, hii nchi ukiifatilia sana unaweza ukaishia kuwa masikini au ukapotezwa...😭😭😭 Kwa kifupi great thinking hii nchi haiwafai... Ashakum SI matusi tunaongozwa kama makondoo vile😭😭😭
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…