tatanyengo
JF-Expert Member
- Mar 30, 2011
- 1,133
- 280
Katika siku za hivi karibuni nimesikia katika vyombo vya habari visa vya kushangaza. Kuna kisa cha huko Songea ambacho mama na kijana wake wa kuzaa wamekuwa wapenzi kwa takribani miaka kumi. Na kingine kimetokea huko kanda ya ziwa, baba alimfumania mke wake akifanya mapenzi na kijana wao. Baba aliwacharanga mapanga na kuwaondolea uhai.
Jamani wana JF tulizoea kusikia akina baba ndo wanatabia ya kufanya mapenzi na mabinti zao. Sasa hili wimbi la akina mama kufanya tendo hilo na vijana wao linashika kasi, ni kitu gani kimetokea katika jamii?