Kijana SHAROBARO wa KITANZANIA anaweza kufanya biashara/kazi gani kuinua uchumi wa Tanzania?

mwanawao

JF-Expert Member
Joined
Aug 18, 2010
Posts
3,192
Reaction score
5,743
Tanzania ya leo imejawa na vijana wengi ambao wamekuwa wakiiga mfumo wa maisha ambao hawajui adhari zake. Kwa mfano mijini utakuta vijana wengi wanataka kufanya kazi ambazo ni laini laini tu, zisizofikirisha na kupanua ubongo, huku wakijiita wao masharobaro. Kijana sharobaro ambaye hata ukimuajiri ofisini anabakia kuchat kwenye facebook muda wote badala ya kufikiri aifanyie nini kampuni ili iweze kuwa na ushindani wa kutosha? Kijana sharobaro ambaye hawezi kwenda shambani na kulima ardhi kubwa ya Tanzania iliyojaa rutuba tele? Kijana sharobaro mwenye ndoto ya kujenga nyumba nzuri au kuwa na gari zuri huku akiishia kwenye mikorogo ya kukoboa uso, kukalikiti nywele na kuvaa milegezo?

Hivi huyu kijana sharobaro wa Kitanzania kama hataishia siku moja kuwa kibaka mtaani na kuchomwa moto anaweza kufanya kazi gani ya kuinua uchumi wa Tanzania?
 
Hamna zaidi ya kuimba bongo fleva na kwenda club . Kweli kazi ipo tz.
 
Kuomba omba na hatimaye kuwa mashoga,hatuna faida nao kabisa.
 
Hamna zaidi ya kuimba bongo fleva na kwenda club . Kweli kazi ipo tz.

Afadhali wangeimba hata hizo bongo fleva na kuhamasisha wananchi kwa nyimbo zitakazowaletea maendeleo. Kila anayeimba bongo fleva utakuta wanaimba nyimbo za kuhamasisha mapenzi tuu..., kwani nini basi wasiimbe angalau nyimbo za kuhamasisha kilimo, watu kufanya kazi kwa bidii maofisini, watu kuwa wazelando na nchi yao, watu kukataa na kupiga vita rushwa, KUTOA HATA ELIMU YA URAIA KWA NYIMBO ZAO? Kwani maana ya msamiati huu wa BONGO FLEVA ni nyimbo za kuhamisisha mapenzi?

Tanzania hii ya leo itajengwa tu na vijana walio makini na wanaofikiria sana nje ya box, tubadilike, tufanye kazi kwa bidii na tuwe wazalendo kwa nchi yetu.
 

Sekta nzuri inayowafaa ni Music and Film Industry (show business), lakin tatizo hapa Tanzania bado miundombinu yake haijawekwa sawa. Wakati tunapigania mazingira bora ya kazi za wasanii, ni vyema vijana hawa wakaenda shule ili kunoa bongo zao kwan hata show business inahitaji upeo na uelewa wa mambo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…