mwanawao
JF-Expert Member
- Aug 18, 2010
- 3,192
- 5,743
Tanzania ya leo imejawa na vijana wengi ambao wamekuwa wakiiga mfumo wa maisha ambao hawajui adhari zake. Kwa mfano mijini utakuta vijana wengi wanataka kufanya kazi ambazo ni laini laini tu, zisizofikirisha na kupanua ubongo, huku wakijiita wao masharobaro. Kijana sharobaro ambaye hata ukimuajiri ofisini anabakia kuchat kwenye facebook muda wote badala ya kufikiri aifanyie nini kampuni ili iweze kuwa na ushindani wa kutosha? Kijana sharobaro ambaye hawezi kwenda shambani na kulima ardhi kubwa ya Tanzania iliyojaa rutuba tele? Kijana sharobaro mwenye ndoto ya kujenga nyumba nzuri au kuwa na gari zuri huku akiishia kwenye mikorogo ya kukoboa uso, kukalikiti nywele na kuvaa milegezo?
Hivi huyu kijana sharobaro wa Kitanzania kama hataishia siku moja kuwa kibaka mtaani na kuchomwa moto anaweza kufanya kazi gani ya kuinua uchumi wa Tanzania?
Hivi huyu kijana sharobaro wa Kitanzania kama hataishia siku moja kuwa kibaka mtaani na kuchomwa moto anaweza kufanya kazi gani ya kuinua uchumi wa Tanzania?