Confession I very much disagree with you. Ila napenda ulivyo positive kwenye mjadala wako. Hata wanaokutukana, unawajibu kwa staha.
Kwa jamii yetu, itatuchukua mda sana kukubaliana na hii hali. Changamoto nyingine ni jinsi ushoga unavotetewa kwa nguvu zote kwa kivuli cha human rights. Wakati tunajua fika kuna human rights kibao zinavurugwa na kupotezewa. Tena na hao hao walio mstari wa mbele kutetea ushoga. Huu utetezi unatufanya tuone kuna agenda ya siri.
In all, sina cha kukushauri. Wewe ni binadamu kama mimi. Hatuna ukamilifu wowote.
Labda swali kwako: unaamini hii hali ya mtu kuwa shoga inaweza kuwa addressed mhusika akaachana nayo? Kwa njia Zipi? Mimi Naamini tunaweza kujifunza kutoka kwako na wengine.