Kijana wa kihindi ang'olewa Meno 232 Maajabu.......

Kijana wa kihindi ang'olewa Meno 232 Maajabu.......

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
42,872
Reaction score
34,363
10492255_466316446839156_8191546949939082089_n.jpg


10526092_466316463505821_2408776343661276441_n.jpg


10517967_466316476839153_4784611790807675963_n.jpg



KIJANA "ANG'OLEWA" MENO 232

Madaktari nchini India wametoa meno 232 kutoka katika mdomo wa kijana mwenye umri wa miaka 17, katika upasuaji uliochukua saa saba.


Kijana huyo Ashik Gavai alifikishwa hospitali akiwa amevimba na maumivu kwenye taya na shavu lake la upande wa kulia, amesema Dokta Sunada Dhiware, mkuu wa idara ya meno katika hospitali ya JJ jijini Mumbai.

Kijana huyo amekuwa akisumbuliwa kwa miezi 18, na alilazimika kusafiri kwenda mjini, baada ya madaktari katika kijiji chake kushindwa kufahamu chanzo cha tatizo.

Madaktari wameelezea hali hiyo kuwa "ni haba sana" kutokea na ni jambo ambalo "limevunja rekodi ya dunia".

Upasuaji huo uliofanyika siku ya Jumatatu, ulihusisha madaktari wawili na wasaidizi wawili.
Ashik sasa ana meno 28.

"Ashik aligunduliwa kuwa na ugonjwa wa aina yake ambao ufizi mmoja huunda meno mengi. Ni kama aina ya uvimbe wa saratani," amesema Dokta Dhiware.

"Mwanzoni, hatukuweza kukata fizi, kwa hiyo tulilazimika kutumia nyundo na tindo kufanikisha.

"Tulivyopasua tu, meno madogo madogo yakaanza kutoka, moja baada ya jingine, na

tulipoyahesabu, yalifika meno 232." Amesema daktari huyo. chanzo.MziziMkavu.


 
Maajabu hayaishi jamani

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Back
Top Bottom