Kijana wa miaka 19 akamatwa na madawa yanayodhaniwa ni HEROIN

Kijana wa miaka 19 akamatwa na madawa yanayodhaniwa ni HEROIN

John Haramba

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2022
Posts
365
Reaction score
1,374
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linamshikilia LUSEKELO ELISHA MWAKANGATA mwenye umri wa miaka 19, Mkazi wa Mama John kwa kosa la kupatikana na kete sita sawa na gramu 0.3 za madawa ya kulevya yadhaniwayo kuwa ni heroin.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Ulrich Matei amesema kuwa mtuhumiwa alikamatwa mnamo tarehe 10.02.2022 maeneo ya Mama John, Kata ya Ilomba, Tarafa ya Iyunga jijini Mbeya katika misako inayoendelea maeneo mbalimbali ya Mbeya dhidi ya wahalifu wa matukio mbalimbali.

Mtuhumiwa amehojiwa na kukiri kujihusisha na uuzaji wa dawa hizo za kulevya.

Ulrich Matei,.jpg
 
Aiseee pesa hizi zinatafutwa kwa kila njia
 
Sijui ilikuwaje mpaka akaingia huko, yaani amejiharibia maisha bado mdogo miaka 19!
 
Bwana mdogo kaingia kwenye 18 za maafande. Gramu 0.3 zimeshamponza.
 
Location haziendani. kwa maama john iko mwanjelwa huko iyunga iko mbali kabisa njia ya kwenda tunduma huko au mbalizi

anyway shauri yake
 
Back
Top Bottom