Dalton elijah
JF-Expert Member
- Jul 19, 2022
- 373
- 829
Kijana Simon Nyamsika (30) mkazi wa sabasaba mjini Lindi, amelazwa katika wodi ya uangalizi maalumu (ICU) katika hospitali ya rufaa ya Sokoine mkoani Lindi kwa kile kinachodaiwa kuwa amekata sehemu zake za siri kwa kitu chenye ncha kali na kuiondoa kabisa sehemu hiyo
Taarifa inasema kijana asubuhi ya Tarehe 07 Julai aliwasili ofisini kwake na kutoa taarifa kuwa hayupo vizuri kiafya.
Baada ya kurudi nyumbani alikimbia ghafla kutoka chumbani kwake akiwa mtupu huku damu nyingi zikimtoka katika eneo la uume wake na mbio hizo alizielekeza moja kwa moja katika eneo la bahari ambapo inadaiwa raia wema walimkuta akiwa anajiosha kidonda chake kwa maji ya bahari kwa dhumuni la kukata damu.
Chanzo: EastAfricaTV
Pia soma: Kijana aliyejikata uume hataweza tena kujamiiana