Kijiji cha Hangaya Suluhu ni kijiji shubiri

Kijiji cha Hangaya Suluhu ni kijiji shubiri

TANZANIA NI SHUBIRI

  • Kijiji cha hangaya ni SHUBIRI

  • SHUBIRI SI TAMU


Results are only viewable after voting.

Abuunuuman

Member
Joined
Sep 11, 2021
Posts
20
Reaction score
29
Kijiji cha malkia HANGAYA SULUHU

Hupewa mfano wa kijiji kilichotawaliwa na wageni ambacho kilikuwa na amani na utulivu

Watu wake hupata chakula chao kutoka katika rasilimali zilizopo ndani yake

Wanaishi na kuendesha kijiji chao kwa rasilimali hizo.

Yakapita majira na miaka baadae watawala wa Kijiji hicho utu wao na nidhamu yao ikaanza kupotea

Ukaanza ufisadi juu ya Mali walizonazo.

Kutokana na matabaka ya walionacho dhidi ya wanyonge

Watoto walitumikishwa kazi mbalimbali za kijamii kama ni watu wazima wadogo

Wanawake waliupoteza utu wao zaidi kutokana na ugumu wa maisha yaliyoisibu jamii yao.

Hali ilipofika hapo ikawapata njaa kali na amani kutoweka kabisa katika kijiji hicho.

Kikabaki kuwa ni kijiji cha mfano kwa methali ya kiswahili isemayo "lakuvunda halina ubani"

Kwa Mapenzi ya mwenyezi mungu wanakijiji walijitwalia uhuru wao kutoka kwa utawala huo wa kibeberu uliopo hapo kabla.

Wakatawala viongozi wazawa makini waliokomaa kidemokrasia.

Baadae kidogo akapatikana kiongozi jasiri mwenye uthubutu wa mafanikio aliyetembea na kauli mbiu ya HAPA KAZI TU

Kutokana na utendaji wake Kijiji hicho kikawa ni shubiri Kwa mataifa ya kigeni na nuru ya mabadiliko Kwa wazawa

kisha kiongozi huyo jasiri akaondoka zake njiani wakati kijiji hicho kilimuhitaji zaidi aendelee kuwaongoza watu wake

Bahati iliyoje kuibuka Kwa chifu hangaya aliyeliongoza taifa hilo katika mabadiliko kwa kauli mbiu ya KAZI IENDELEE.

Nduguzangu wanakijiji tuilinde tunu ya amani na utulivu tuliyonayo.

Jamii yenye ukomavu mzuri wa kidemokrasia na utawala bora tulionao haki zote za msingi zenye ustawi ikiwemo ajira Kwa vijana zitapatikana.

Amani na utulivu ndio msingi bora na imara wa maendeleo ya kila kijiji kwa kila

Kijiji chetu cha Tanzania ni amani na tulivu.
 
Back
Top Bottom