Kijiji cha Kataryo Chaongeza Kasi ya Ujenzi wa Zahanati Yake: Mbunge Prof. Muhongo Achangia Saruji Mifuko 200

Kijiji cha Kataryo Chaongeza Kasi ya Ujenzi wa Zahanati Yake: Mbunge Prof. Muhongo Achangia Saruji Mifuko 200

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301

KIJIJI CHA KATARYO CHAONGEZA KASI YA UJENZI WA ZAHANATI YAKE: MBUNGE AKICHANGIA SARUJI MIFUKO 200

Kijiji cha Kataryo ni moja ya vijiji vitatu vya Kata ya Tegeruka. Vijiji vingine ni: Mayani na Tegeruka.

Kijiji cha Kataryo hakina zahanati yake, kwa hiyo wakazi wake wanalazimika kusafiri umbali wa zaidi ya kilomita saba (7) kwenda kupata Huduma za Afya kwenye zahanati ya kijiji jirani cha Mayani.

Kijiji cha Kataryo chaamua kujenga Zahanati yake:
Ujenzi ulianza rasmi Julai 2023, na Mbunge wa Jimbo, Prof Sospeter Muhongo alikaribishwa kupiga Harambee ya kuchangia ujenzi huo tarehe 4.4.2024

Wakazi wa Vitongoji sita (6) vya Kijiji cha Kataryo walikubaliana kuchangia vifaa vya ujenzi kulingana na wingi wa kaya za kila kitongoji. Michango ya awali ilikuwa kati ya Shilingi 5,000 na 7,000 kwa kila kaya.

Matokeo ya Harambee ya Mbunge wa Jimbo:
Harambee ilifanyika tarehe 4.4.2024 na matokeo yake ni:

(i) Saruji kutoka kwa Mbunge wa Jimbo:
Saruji Mifuko 200
(ii) Saruji kutoka kwa Diwani, Mhe Alpha Mashauri
Saruji Mifuko 50
(iii) Saruji kutoka kwa wanakijiji:
Saruji Mifuko 26
(iv) Fedha: Shilingi 600,000

Akaunti ya kuwasilisha michango yetu ya fedha:
Wana-Kataryo na Wadau wengine wa Maendeleo wanaombwa kutoa michango yao kupitia Akaunti ya Kijiji ambayo ni:

Benki: NMB
Akaunti Na: 30302300302
Jina: Kijiji cha Kataryo

Huduma za Afya Jimboni mwetu:
Jimbo la Musoma Vijijini lenye Kata 21 zenye Vijiji 68 lina:

*Hospitali 1 ya Halmashauri yenye hadhi ya hospitali ya Wilaya

*Vituo vya Afya: 6

*Zahanati za Serikali: 25
*Zahanati Binafsi: 4

*Zahanati zinazojengwa: 16

Picha za hapa zinaonesha:
*Boma la OPD la Zahanati inayojengwa Kijijini Kataryo, Kata ya Tegeruka

*Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini akitoa majibu ya kero na matatizo ya wananchi kabla ya kuanza kupiga Harambee ya ujenzi wa Zahanati ya Kijiji cha Kataryo

*Wananchi wa Kata ya Tegeruka wakiwa wamegawiwa vitabu viwili viwili (Volumes III & IV) vinavyoelezea mafanikio ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya Mwaka 2020-2025 ndani ya Jimbo la Musoma Vijijini.

Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz

P. O. Box 6
Musoma

Tarehe:
Jumapili, 28.4.2024
 

Attachments

  • WhatsApp Image 2024-04-27 at 23.48.26.jpeg
    WhatsApp Image 2024-04-27 at 23.48.26.jpeg
    92.3 KB · Views: 6
  • WhatsApp Image 2024-04-27 at 23.48.26(1).jpeg
    WhatsApp Image 2024-04-27 at 23.48.26(1).jpeg
    118.1 KB · Views: 6
  • WhatsApp Image 2024-04-27 at 23.48.26(2).jpeg
    WhatsApp Image 2024-04-27 at 23.48.26(2).jpeg
    112.7 KB · Views: 6
  • WhatsApp Image 2024-04-27 at 23.48.27.jpeg
    WhatsApp Image 2024-04-27 at 23.48.27.jpeg
    80.5 KB · Views: 4
Back
Top Bottom