Kijiji cha Oltepes Longido kina maji, hakuna anayetumia mkojo wa ng'ombe kujisafisha akiwa hedhini

Kijiji cha Oltepes Longido kina maji, hakuna anayetumia mkojo wa ng'ombe kujisafisha akiwa hedhini

Pfizer

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2021
Posts
590
Reaction score
807
"TULIKUA TUNAZUNGUMZIA CHANGAMOTO TULIZOPITIA MIAKA YA NYUMA"

Kutokana na taarifa iliyotolewa inayodai kwamba wanawake wa kijiji cha Oltepes Longido hutumia mikojo ya ng'ombe kujisafisha wakiwa hedhini, Mhe. Waziri wa Maji Jumaa Aweso ameagiza watendaji wa sekta ya Maji mkoani Arusha kulifuatilia jambo hilo ka ukaribu ambapo Meneja wa Mamlaka ya Maji AUWSA Kanda ya Longido amefika katika kijiji cha Oltepesi kufuatilia uhalisia wa jambo hilo na kuleta ripoti kwa Mhe Waziri kuwa kulikua na kutoelewana kwa lugha katika mahojiano hayo kutokana na mhusika kutozungumza lugha ya kiswahili kwa uhakika akihitaji mtafasiri.

Baada ya timu ya Wizara ya Maji kufika katika eneo hilo imebainika kwamba mhusika Bi Elizabeth alikua akisimulia habari za muda mrefu na kueleza changamoto walizopitia katika maisha ya nyuma kwani kwasasa maji yanapatikana katika eneo hilo na hawana changamoto.

Pia, soma: Ukosefu wa maji: Watumia mkojo wa ng'ombe kujisafisha wakiwa hedhini
 
Waandishi makanjanja wanapotosha ukweli kwa maslahi ya nani
 
Back
Top Bottom