Kijiji cha Roma chapokea Sabato

Kijiji cha Roma chapokea Sabato

Sosoma Jr

JF-Expert Member
Joined
Aug 7, 2020
Posts
312
Reaction score
281
Nchini Slovakia wapo wenyeji wenye asili ya India wapatao 2,000 (wajulikanao kama Roma) ambao hujitambua rasmi kuwa wao ni Wakristo japo hawahudhurii kanisani; wala hakuna hata mmoja wao ambaye alishawahi kuisoma Biblia.

Baada ya uhuru wa Slovakia mwaka 1993, wamishonari mbalimbali walianza kuja kwenye makazi hayo ya Rakusi, wanakoishi hao watu wa kale wenye asili ya India (wajulikanao kama Roma). Mmishonari mmoja, aliyewasili pamoja na mkewe, walianza kuhubiri mitaani kila Jumapili. Watu walikusanyika kuwasikiliza ila hawakuwa na uelewa mpana kwa vile kamwe hawajawahi kuisoma Biblia.

Mwanakijiji mmoja, Peter Miziga, alifurahia kupiga vyombo vyake vya muziki kuliko kusikiliza mahubiri. Alipiga gitaa vizuri wakati wa harusi na misiba. Kwa kawaida, washirika wake kwenye kikundi chake cha uimbaji, akiwepo mdogo wake aitwaye Pavol, walitumia kipato chao cha muziki kwenda kulewa pombe. Lakini Peter kamwe hakulewa wakati akipiga muziki. Alikuwa dereva wa kikundi hicho.

Alipokuwa hakulewa, Peter aligundua yapo makundi mawili ya watu miongoni mwa hao wenyeji wa asili ya kihindi: kundi moja walikuwa wenye nidhamu na akili sana; wakati kundi la pili walikuwa duni, washamba, wasio na elimu. Wanamuziki wengine hawakutambua utofauti huo kwa vile walikuwa wamelewa.

Peter alizidi kuona tofauti za makundi hayo mawili zilivyoyeyuka pale walipolewa. Wenye elimu na waungwana walivua mavazi yao na kuenenda kama wale watu duni. Mwisho wa kila tukio ilikuwa kupigana ngumi; hata kama ni wakati wa mazishi.

Peter na wapiga muziki wenzake walipoona wehu wanaokuwa nao hao watu wenye asili ya kihindi baada ya kulewa huko katika Jamhuri ya Czech (hutamkwa Cheki), Peter na kaka yake wakaamua kuachana na muziki. "Nimeamua sasa kushiriki muziki wa kumsifu Mungu.

Pavol amekuwa akisikiliza muziki wa Kikristo uliofundishwa na wamishonari. Muda si mrefu Peter, Pavol, na kikosi chote cha waimbaji hao kikawa kinaimba nyimbo za Kikristo nyumbani kwao Pavol. Siku moja wakiimba Peter aliona Biblia mezani.

"Je hiki ni kitabu cha jinsi gani?" aliuliza, huku akikichukua. Pavol alimnyang'anya na kumwambia akiweke hapo mezani kitulie. "Hicho siyo kwa ajili yako."

Pavol alikuwa akijifunza Biblia, na hakutaka kumpatia mwingine asome. Wakati Pavol na wengine wakicheza, Petro aliichukua taratibu Biblia hiyo na kuondoka nayo. Alipofika nyumbani aliisoma kwa mwezi mzima uliofuata, akisoma sana kitabu cha Ufunuo na hatimaye vitabu vya injili.

Baada ya muda ndipo alimweleza ndugu yake kuwa alikuwa na Biblia hiyo. Pavol kwa unyenyekevu alimsihi amrejeshee atakapomaliza kuisoma.

Siku moja Peter akasoma Marko 16:16 ambapo Yesu asema, "Aaminiye na kubatizwa ataokoka; asiyeamini, atahukumiwa." Aliifunga Biblia na hatimaye kuifungua upya. Biblia ikawa wazi kwenye aya hiyo hiyo "Aaminiye na kubatizwa ataokoka; asiyeamini, atahukumiwa." Alifanya hivyo mara tatu, na fungu hilo hilo ndilo lililojitokeza.

Peter alinyanyua Biblia yake na kumkimbilia kaka yake, Pavol alikuwa na marafiki zake wawili. "Tafadhali njoo, unibatize," alisihi Peter.

Hakujua lolote kuhusu ubatizo. Shauku yake ilikuwa kutii agizo la Yesu. "Unataka mimi nipate kukubatiza?" alijibu Pavol. "Ndiyo, kumeandikwa hapa kuwa kila abatizwaye ataokoka," alijibu Peter.

Pavol alisita, ila Peter alikuwa hana utani, hakika anataka abatizwe. Ndugu hao wawili pamoja na rafiki zao wawili walienda nje ya makazi yao ya Roma, wakaelekea kwenye kijito, wakatafuta eneo lenye dimbwi lipatalo kina cha maji cha mita moja, wakabatizana.

Waliungama dhambi zao kwa Mungu na kutafuta msamaha. Tendo hilo liliwapatia uzoefu wa furaha kubwa na kushangilia vile mbingu zote zilivyofurahia ubatizo huo.

Baada ya siku hiyo wanaume hao wanne waliacha kabisa lugha chafu, ulevi na uvutaji sigara. Majirani walishangaa. Zamani watu hao walipolewa walikuwa tishio la amani.

Marafiki hao wanne waliamua kujifunza Biblia pamoja kila siku. Wakati mwingine walianza usiku na kuendelea hadi asubuhi. Watu wengine walijiunga na kundi hilo la Biblia. Watu 50 hadi 100 walikusanyika sebuleni nyumbani kwao Peter.

Wakati wa usiku walipokuwa wakijifunza, Peter alisoma Marko 16:9 ambapo yasema: "Naye alipofufuka alfajiri siku ya kwanza ya juma." Peter akakumbuka kuwa Yesu na wafuasi wake walipumzika siku ya saba ya juma, Sabato ( yaani Jumamosi) soma Kutoka 20:8-11 na Luka 4:16 na kushangaa kwa nini wamishonari waliotembelea makazi hayo ya Roma waliabudu siku ya Jumapili.
Hakuna mmishonari aliyeweza kumjibu Petro swali lake.

Kikundi hicho cha kujifunza Biblia kiliendelea kusoma na kuigundua amri ya nne, nao wakaanza kutunza Sabato.

Siku moja Peter alitaja wasiwasi wa uhalali wa Jumapili kama siku ya ibada kwa mgeni mmoja aliyekuwa anatembelea makazi hayo ya Roma. Mtu huyo aitwaye Josif, alikuwa Mwadventista, naye akamjulisha Peter kuwa lipo kanisa lenye kutunza sheria za Mungu (Amri Kumi soma Kutoka 20:1-17) lenye kutunza Sabato ya kibiblia.

Peter alimwalika mgeni huyo aje kukihutubia kikundi chake cha kujifunza Biblia. Baadaye Josif alimchukua Peter na marafiki zake kutembelea kanisa la Waadventista lililoko kwenye eneo hilo. Peter alifurahia utulivu na kicho kwenye huduma za ibada za Waadventista. Hapakuwa na makelele na fujo.

Sebule nyumbani mwa Peter ikawa nyumba ya ibada kwa Waadventista wakaendesha ibada za kila sabato na programu zingine. Peter, kaka yake, na waumini wengine 24 wa kikundi chao cha kujifunza Biblia walibatizwa mwaka 2015 na kujiunga katika kanisa la Waadventista wa Sabato.

Miaka miwili baadaye watu wengine 10 walibatizwa. Mwaka 2018 kanisa lilijengwa nje ya makazi hayo ya Roma, na kila Sabato (Jumamosi) watu zaidi ya 100 hukutanika kwa ibada. Hilo ndilo kanisa lililoanzia sebuleni nyumbani kwao Peter.

Barikiweni nyote na Mungu wa mbinguni!!
 
Hivi wasabato ndio walienda airport bila passport kutaka kwenda marekani bila hata kuwa na ticket sasa naamini wajnga wanapungua na wengine wanazaliwa hivyo hawatakaa watoweke duniani
 
HAKUNA wasabato waafrika ulete hadithi zao mbona kila siku ni Hadithi za Wasabato wazungu tu?
 
Back
Top Bottom