Kijitonyama: Wananchi wanaokataa kulipia ulinzi shirikishi kupelekwa Mahakamani

Kijitonyama: Wananchi wanaokataa kulipia ulinzi shirikishi kupelekwa Mahakamani

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607
Maamuzi hayo yanatarajiwa kufanywa na Serikali ya Mtaa wa Bwawani Kata ya Kijitonyama, Dar es Salaam kwa wale watakaokaidi kulipa kutoa ushirikiano kwa ulinzi shirikishi.

Mwenyekiti wa Bwawani, Felicianus Kamkala amesema “Wapo baadhi ya raia wanaotaka kuleta mgomo wa kuchangia fedha za motisha kwa vijana wanaofanya zoezi la usalama mtaani, tumeandaa barua kwa Polisi Kata, tutawaletea hizo barua za kuwapeleka Kata kisha Mahakamani ili waone hili suala tupo nalo makini.”

Chanzo: EATV
 
Watoe risiti za EFD kwanza

Halafu ijulikane usimamizi wa hizo Fedha siyo kuleta Ujanja ujanja watanzania wa Leo siyo wa Jana

Michango imekuwa mingi mno aisee
 
Ndio tatizo lenu CCM. Hamuanzishi miradi ili kumsaidia mwananchi, mnaanzisha miradi ili mpige. Mbaya sana hii tabia
Haya Mambo yataigharimu CCM 2025

Huku kwetu nyumba 200 mchango 15000 Walinzi wako 6

15000x200= 3000000

Walinzi wanalipwa 100,000 kila mmoja = 600,000

2,400,000 inaenda wapi?
 
Kushindwa kufikiri kwa wajinga tuliowapa mamlaka kunadhidi kufanya gharama za maisha kuwa juu.

Hivi hawa walinzi shirikishi wakiwa ni casual workers wa serikali na kuwekwa mitaani kusaidiana na mapolisi kulinda watu na mali zao kuna shida gani?.

Kila mtaa wawepo na wawajibike kwa mkuu wa kituo cha polisi cha karibu kwa kupeleka report kila siku na kupewa msaada wa polisi kila wanapohitajika, kila kikundi kinakuwa na supervisor mwenye training za jeshi la polisi na hao vijana baadhi wanakuwa na mafunzo pia.
 
Maamuzi hayo yanatarajiwa kufanywa na Serikali ya Mtaa wa Bwawani Kata ya Kijitonyama, Dar es Salaam kwa wale watakaokaidi kulipa kutoa ushirikiano kwa ulinzi shirikishi.

Mwenyekiti wa Bwawani, Felicianus Kamkala amesema “Wapo baadhi ya raia wanaotaka kuleta mgomo wa kuchangia fedha za motisha kwa vijana wanaofanya zoezi la usalama mtaani, tumeandaa barua kwa Polisi Kata, tutawaletea hizo barua za kuwapeleka Kata kisha Mahakamani ili waone hili suala tupo nalo makini.”

Chanzo: EATV
Wananchi wanalipa. Kodi na tozo ili serikali iwapatie ulinzi na usalama wa mali zao hayo mambo ya shirikishi ni wizi wa maccm
 
Kwangu mbo haya nilisha piga malufuku sitaki mjumbe Wala msenge yeyote aniambie mambo hayo na wanajua
 
Maamuzi hayo yanatarajiwa kufanywa na Serikali ya Mtaa wa Bwawani Kata ya Kijitonyama, Dar es Salaam kwa wale watakaokaidi kulipa kutoa ushirikiano kwa ulinzi shirikishi.

Mwenyekiti wa Bwawani, Felicianus Kamkala amesema “Wapo baadhi ya raia wanaotaka kuleta mgomo wa kuchangia fedha za motisha kwa vijana wanaofanya zoezi la usalama mtaani, tumeandaa barua kwa Polisi Kata, tutawaletea hizo barua za kuwapeleka Kata kisha Mahakamani ili waone hili suala tupo nalo makini.”

Chanzo: EATV
Huyo Mwenyekiti wa Bwawani Felicius Kamkala hana akili kabisa.
Utampeleka mahakamani mtu kwa kutoshiriki sungusungu au kutolipia kwa sheria ipi?
 
Hili zoezi ni sawa na mpango wa kuwalipa wezi ili wasije usiku kuiba...ukiangalia sehemu nyingi wale wezi sugu ndiyo polisi jamii
 
Wizi mtupu... polisi wanakazi gani ? Wanaishi kwa kodi zetu .... kama ulinzi ni wa kila mtu watuelimishe tujilinde wenyewe maswala ya ulinzi shirikishi jeshi la polisi lilipie kwasababu kazi yao wameshindwa na sasa wanataka ku subcontract kwa wananchi tuifanye bila malipo, wao na serikali yao wanachojua ni kukamata magari tu mchana ulinzi wakiachia mateja yanayoiba na kukusanya rushwa usiku kwa mwavuli wa Ulinzi shirikishi. Nchi zote mbali na Africa zinazotumia community policing..serikali ndio inayolipa..sasa leo mtu anaela zake tayari analipia ulinzi Gardaworld mnaburuza mahakamani heti kagoma kulipia ulinzi kwa sheria gani na facts zipi ? Mna mkataba nae wa ulinzi ? Akiibiwa mnamlipa ?
 
Back
Top Bottom