Kijiweni na Mashabiki wa Ndala

Mkuu.. hili kombe mwaka huu ni la mnyama, tusalimu amri tu

Kwasababu sisi Vyura FC tunarukaruka tu uwanjani yaani hakuna mvuto kabisa
Kusalimu amri mpaka iwe mathematically impossible.
Hata muongoze point tisa with three games to spare, lolote laweza kutokea.
Bingwa ataptikana filimbi ya mwisho, mwisho wa msimu.
 
Kusalimu amri mpaka iwe mathematically impossible.
Hata muongoze point tisa with three games to spare, lolote laweza kutokea.
Bingwa ataptikana filimbi ya mwisho, mwisho wa msimu.
Mathematically speaking, mwenye nafasi zaidi ya kubeba kombe ni Yanga. Kwa nini? Kwa sababu ushindi wa mechi unategemea ufungaji magoli. Mwenye uwezo wa kufunga magoli mengi ndiye mwenye uwezo wa kushinda mechi nyingi. Kufunga magoli machache na kushindaa mechi nyingi kunategemea mambo mawili tu, bahati (muda gani umefunga goli lako) na ukuta usiofungika hata iweje (mara nyingi kwa kuegesha basi kwenye ngwe yao). Simba haina ukuta wa aina hiyo, ndiyo maana wapinzani wanafika golini kwake na wakakosa magoli ya wazi. Yanga nao hali kadhalika. Tofauti yao ni kwenye ufungaji. Angalia takwimu uone nani anafunga zaidi. Hata kwa mantiki ya kawaida, mwenye kisu kikali ndiye anayekula nyama!
 
Hawa mikia hamnazo kabisa, wanaamini watakuwa mabingwa msimu huu kisa point 4 mbele. Timu yenu ya kawaida sana tena na mnashinda kibahati na siku zenu zinahesabika mrudie majuto yenu.
Tunachotaka kufanya kwa namba tunayoijua ni kutimiza lengo la serikali kupiga marufuku kusafirisha wanyamapori nje ya nchi kwa miaka 3 kuanzia sasa hivi, na hili tutawasaidia serikali kwa namna tunayoijua sisi.
Simba akiwa bingwa nitajitoa kwa mwezi kushabikia mpira.
 
Issue hapa siyo chura wala Snura au nani atabeba kombe, ila ni ubora wa washambuliaji wa kigeni wa Mnyama dhidi ya wa Wanajangwani.
1. Kama mngekua na washambuliaji bora wa kigeni si mngekuwa mnaongoza ligi.. Mbona tumewaacha pointi 4 mpaka sasa?
2. Kama mnaforward wakali kupitiliza si mngetufunga goli 100 tulipokutana.. kwanini mpaka msubiri mbeleko za refa??
3. Na hao forward wenu bora.. ndo wanaongoza chati za ufungaji katika VPL? Au katika litimu lenu, hao wageni ndo wana magoli mengi kuliko wazawa??

Hint;


NB: Kinachonipa furaha juu ya Mnyama.. ni tuna defence bora kabisa kwa sasa katika VPL, kutufunga imekua kazi ngumu sana... midfield tuliyonayo ni bora mpaka inakera.. mara mwisho mido kama hii ilionekana katika ukanda huu wa CECAFA miaka ya 2000 ambapo ilimuwezesha mnyama kuingia nane bora katika CAF.. Forward yetu ni nzuri.

cc Nyenyere na ndugu yako @ Sibonike
 
Mkuu sembo usiniwekee maneno yako mdomoni mwangu, tena ukome kabisa!

Mimi naamini kabisa mnyama hawezi kupiga ligi hadi mwisho akiwa salama, ataanguka tu. Kwa taarifa yako tukikutana tunachukua pointi zetu 3, pointi moja iliyosalia wataichua akina Toto, Mbao na Kagera huku Kanda ya Ziwa.

Piga ua garagaza, Yanga ndiye Bingwa 2016/2017! Mikia haina washambuliaji wa kuweza kufunga mechi zote zilizosalia, sasa hivi inabahatisha bahatisha tu kupata kigoli kimoja kimoja kupitia viungo Mzamiru Yassin na Mohamed Ibrahim. Kichuya tayari ame_carrass!

Nayaweka muhuri maneno haya ili yatakapotimia wewe sembo na wenzako wenye msimamo kama wako mje mtoe ushuhuda hapa. SIGNED AND SEALED by Makoye Matale this 30th day of December, 2016 at Mabuki, Mwanza Tanzania.
 
Narudia tena kwa HesabuKali tulizozichonga kabla ya msimu kuanza, kama hadi sasa hakuna aliyejaribu kutupa changamoto.. basi huu ubingwa tunauchukua asubuhi sana.

Ligi kuu inaisha mwezi wa 3.. kama ratiba ikifuatwa.. Sasa mkuu naona umepiga HesabuKali kua kipindi unaposataafu soka ligi itakua ishaisha.. na hadi inapoanza utakua ushatoka kifungoni.. Hongera kwa HesabuKali ulizopiga.
 
Namwona Hamis Tambwe na Donald Ngoma katika orodha uliyoiweka. Siwaoni Mavugo, Blagnon na Chirwa. Hao ndio washambuliaji wa kigeni wa Simba na Yanga. Kati ya hao watatu wasioonekana kwenye orodha, Chirwa anaongoza kwa magoli ya kufunga. Na hiyo ndiyo hoja yangu ya msingi, kwamba mastraika wa kigeni wa Yanga wako vizuri zaidi kuliko wa Simba. Nakushukuru kwa kusaidia kuthibitisha hilo kupitia hii orodha yako, ambayo - tofauti na aliyetuwekea - haina ushabiki maandazi!
 
[emoji1] [emoji1] [emoji1] ... Samahani sana Mkuu.. Ila ukimya wako ulinifanya nipigie msitari.. msemo wa wahenga kua.. "silence means aggreament".. na hiyo aggreament ni Simba Sports Club ndiyo bingwa wa VPL msimu huu.
 

Excellent analysis, lakini subiri waje.

Mwaka huu wanaamini lazima wachukue kombe, come sun, come rain. Mpira hauko hivyo. Imani yao inaweza kuwa faida kwa Yanga. Wanajitengenezea tension ambayo wanaweza kushindwa kuhimili kadri siku zinavyokwenda.

Ni dhahiri mwaka huu wapo vizuri. Lakini, to win games, you have to score. Defending without scoring enough goals is not enough to win games.
 
Polite advise:

Christmas imekwisha jamani, tafadhali mods naomba muondoe hicho kidude kama kimkia cha Santa Cruz katika avatar yangu, kinanikera sana kuliko maelezo maana kina rangi nisizozipenda hata kidogo.

Kama haiwezekani kukiondoa basi naomba mnipumzishe kwa kunipa Voluntary Ban, mtakapokiondoa, mkumbuke kunirudhisha kundini ili nipambane na sembo et al.

CC. Invisible.
 
[emoji1] [emoji1] [emoji1] ... Samahani sana Mkuu.. Ila ukimya wako ulinifanya nipigie msitari.. msemo wa wahenga kua.. "silence means aggreament".. na hiyo aggreament ni Simba Sports Club ndiyo bingwa wa VPL msimu huu.
Mkuu majukumu yamekuwa mengi sana, si unafahamu kuwa [HASHTAG]#Hapakazitu?[/HASHTAG]
 

Yanga mwenzangu big up. Kuweka et al. in italics kunaonyesha level yako ya juu.
 
Na mtu aliyeiandaa hiyo orodha ni mnazi wa mikia fc. Kichuya haiongozi hiyo orodha, anayeongoza ni Amis Tambwe akifuatiwa na Saimon Msuva.
 
Hivi unapata vipi uthubutu wa kusema washambuliaji wa kigeni ni bora wakati;
1. Wote wamezidiwa magoli na wazawa.
2. Mshambuliaji ambaye kazi yake ni kufunga, anamzidi goli 2 kiungo ambaye kufunga si mambo yake.. kweli alafu unasema mna washambuliaji bora?? Hamuoni aibu!!

NB; Forward wa kigeni wa Yanga ni afadhali [na si bora].. Wa Mnyama mkali mwituni pengine kuliko wote, Simba .. bado wanaadapt mfumo wa mwalimu.. ila soon mtaona vitu vyao
 
Mkuu ligi inaisha mwezi Machi, 2017 si zaidi ya siku 92 kuanzia leo. Tusubiri hadi lini Mkuu?
 

Nilichokielewa hapa ni.. Ni dhahiri mwaka huu wapo vizuri.. ungemalizia tu, na mwali msimu huu ni wao, japo tunajilazimisha kubisha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…