Kijiweni na Mashabiki wa Ndala

Simba Jana imeonesha Mpira Mbovu Mukiendelea Kucheza style ile Yanga atawapiga Hata goli 8

Ruvu Jana imeonekana Timu Bora Kuliko Simba Sawa Mumeshinda Lakini Simba ya Jana siyo Simba ile niliyoiona Mzungo wa Kwanza.
 
Mda unaenda Mkuu.. hiyo soon itafika lini? Endeleeni kusubiri kutudhihirishia wakati sisi tunachanja mbuga.. Hadi hiyo soon yenu ifike.. sisi tutakua tushatangaza ubingwa kitaaaaaambo.
Kwa ulimbukeni wako unaona kama ligi imekwisha so siwezi kukushangaa, maana umekunya kichakani halafu unageuka kuyatazama
 
Tuko pamoja kwa jambo moja. Msimbazi likiingia anga zangu ni kuwapa akina mama ntilie wafungie mandazi.
 
Bila shaka umeelewa kinachomaanishwa by the way hili si jukwaa la kiswahili
Mkuu hili ni jukwaa mtambuka.. tunatumia lugha zote, kiswahili na kingereza. Sharti ziwe lugha fasaha.

Alafu Mkuu huoni kua kupitia hili hili jukwaa wewe na mwenzako mnaua ndege wawili kwa jiwe moja?
Mnapata darasa la mpira na darasa la lugha adhimu ya kiswahili??
 
Tuko pamoja kwa jambo moja. Msimbazi likiingia anga zangu ni kuwapa akina mama ntilie wafungie mandazi.
[emoji1] [emoji1] [emoji1].. Mimi sisubiri mpaka liingie.. nalifata huko huko kwenye chanja za magazeti.
 
Na mzunguko wa kwanza uli comment kuhusu hiyo Simba unayodai ilikuwa vizuri?Mzunguko wa pili hiyo timu yako unayoishabikia imeshapoteza pointi 2 na hiyo Simba unayoishangaa imeshinda mechi 3 mfululizo.Baada ya mechi 3 mzunguko uliopita Simba ilikuwa na pointi 7 sasa ina pointi 9 baada ya mechi 3.Hiyo tathimini yako umeijenga kwa mantiki gani?Kufungwa Simba goli 8 ni ndoto tena ya mwendawazimu. Mliongoza 3 bila tena kwa Simba dhaifu kwa miaka ya karibuni zikarudi zote. Nyie bila msaada wa warefa hamna timu hata ya kutoa droo na Simba wachezaji 11 kwa 11.Mlihemeshwa na wachezaji 10 mkabadili kocha.
 
Sio kweli simba sio nzuri kwenye defence. kinacho ibeba simba na kuoneka kama simba ina ulinzi imara ni mfumo anao tumia kocha uwanjani..

Simba wanavyo cheza wamejaza viungo wengi katikati wenye nguvu. kuweka viungo wengi katikati timu ikicheza huwezi ukaona udhaifu wa Defence..

Ukitaka kuona Simba kama safu ya ulinzi sio nzuri simba inapo kutana na timu ambayo inacheza kama wao na kupita kwake wanatumia pembeni. utaona safu ya Simba inavyo pata shida.

Mfano mzuri LIVERPOOL tunayo iyona sio kana kwamba ni nzuri. ila defence ni dhaifu kinacho ibeba ni uwepo Viungo wazuri katikati. ukiwa na viungo wazuri wanaweza waka kupa vitu viwili kwa wakati mmoja.

Turudi kwa Simba ukitaka kujua kana Viungo wanafanya kazi zote angalia magoli mengi wanayo funga Simba yanafungwa na viungo na sio washambuliaji..
 
hii mechi ina kumbukumbu mujarabu katika maisha yangu

cc galatia
 
Jukwaa mtambuka ungeongea upuuzi kiasi hiki? Nakuona kama limbukeni mmoja hivi
 
Kwa ulimbukeni wako unaona kama ligi imekwisha so siwezi kukushangaa, maana umekunya kichakani halafu unageuka kuyatazama
soka tunalotandaza linatosha sisi kujigamba.. haaaa
 
Jukwaa mtambuka ungeongea upuuzi kiasi hiki? Nakuona kama limbukeni mmoja hivi
lazima unione hivyo.. maana tunaongoza ligi tangu msimu umeanza.. timu imeimarika tofauti na mtegemeo yenu.. haha.. pole sana binti.
 
Mkuu sibonike achana na hao malimbukeni , hawajui chochote zaid ya mihemko, Yanga itawadhihilishia soon ubora wake
Mkuu, hao ni SHILAWADU. Wanaongea balaa. Kuongoza ligi imekuwa nongwa mtaani hatunywi maji.
 
Simba Jana imeonesha Mpira Mbovu Mukiendelea Kucheza style ile Yanga atawapiga Hata goli 8

Ruvu Jana imeonekana Timu Bora Kuliko Simba Sawa Mumeshinda Lakini Simba ya Jana siyo Simba ile niliyoiona Mzungo wa Kwanza.
Ondoa fikra butu kichwani mwako Simba SC hata iwe na wachezaji pungufu, Mkodisho FC hawawezi kupata ushindi

Labda kwa msaada wa Martin Sanya, na mkono wa Netball uwanjani, bila shaka unalijua hilo

Tafakari..!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…