Kijiweni na Mashabiki wa Ndala

Kijiweni na Mashabiki wa Ndala

Na mtu aliyeiandaa hiyo orodha ni mnazi wa mikia fc. Kichuya haiongozi hiyo orodha, anayeongoza ni Amis Tambwe akifuatiwa na Saimon Msuva.

Kwahiyo Mkuu hilo jambo linaifanya list hiyo kua batili? Na vipi kuhusu magoli ya Kiungo bora kwa sasa, Muzamiru Yassin.. nayo vipi yameongezwa?? [emoji1] [emoji1]
 
Hivi unapata vipi uthubutu wa kusema washambuliaji wa kigeni ni bora wakati;
1. Wote wamezidiwa magoli na wazawa.
2. Mshambuliaji ambaye kazi yake ni kufunga, anamzidi goli 2 kiungo ambaye kufunga si mambo yake.. kweli alafu unasema mna washambuliaji bora?? Hamuoni aibu!!

NB; Forward wa kigeni wa Yanga ni afadhali [na si bora].. Wa Mnyama mkali mwituni pengine kuliko wote, Simba .. bado wanaadapt mfumo wa mwalimu.. ila soon mtaona vitu vyao
Mkuu hii 9 ya Amisi Tambwe umeisoma juu-chini nini? Kama hivyo basi ni kweli kauli yako kwamba hata Tambwe mwenye magoli yako 6 anazidiwa na Kichuya mwenye magoli halisi 9!
 
Mkuu hii 9 ya Amisi Tambwe umeisoma juu-chini nini? Kama hivyo basi ni kweli kauli yako kwamba hata Tambwe mwenye magoli yako 6 anazidiwa na Kichuya mwenye magoli halisi 9!
Hapa nilikua namzungumzia forward bora kabisa ya kimataifa kuwahi kushuhudiwa katika, bwawa la Jangwani.. Donald Ngoma.
 
Kama kawaida yao wanajaribu kubadili ukweli kwamba Simba anaongoza tena kwa pointi 4.Kocha yeyote mzuri anapoanza kujenga timu ni lazima aanze na defence. Na kwa defence za timu zote hamna ubishi kwamba ipi ni bora mpaka sasa. Unaweza ukawa na washambuliaji wazuri ukawa una concede magoli ya hovyo. Pia unaweza kuwa na defence nzuri kama ya Simba ukashinda kwa sababu risk ya kufungwa inakuwa ndogo. Mourinho na Man United ni mfano hai wa ninayosema. Ameweza ku sort out defence timu imeanza kucheza kwa kujiamini hivyo hivyo kwa Conte ambaye baada ya kufungwa goli 3 na Arsenal alibadili mfumo na defence ikawa stable na matokeo yanaonekana . Arsenal wamekuwa na tatizo hilo miaka nenda rudi ya kuwa na viungo wazuri na washambuliaji wazuri bila walinzi wazuri.Ndio maana Wenger amejaribu kuimarisha defence .
 
Nilichokielewa hapa ni.. Ni dhahiri mwaka huu wapo vizuri.. ungemalizia tu, na mwali msimu huu ni wao, japo tunajilazimisha kubisha.

Kwamba mpo vizuri halina ubishi lakini halimaanishi ubingwa moja kwa moja.

Kuna vikwazo mbele yenu. Hamfungi magoli mengi. Kuna yellow/red card kwenye mchezo hasa ukizingatia mna first eleven nzuri lakini kwenye benchi la sub si wazuri sana. Kuna wachezaji kuumia pia.

Zote hizo ni factors muhimu kulelekea ubingwa.
 
Kama kawaida yao wanajaribu kubadili ukweli kwamba Simba anaongoza tena kwa pointi 4.Kocha yeyote mzuri anapoanza kujenga timu ni lazima aanze na defence. Na kwa defence za timu zote hamna ubishi kwamba ipi ni bora mpaka sasa. Unaweza ukawa na washambuliaji wazuri ukawa una concede magoli ya hovyo. Pia unaweza kuwa na defence nzuri kama ya Simba ukashinda kwa sababu risk ya kufungwa inakuwa ndogo. Mourinho na Man United ni mfano hai wa ninayosema. Ameweza ku sort out defence timu imeanza kucheza kwa kujiamini hivyo hivyo kwa Conte ambaye baada ya kufungwa goli 3 na Arsenal alibadili mfumo na defence ikawa stable na matokeo yanaonekana . Arsenal wamekuwa na tatizo hilo miaka nenda rudi ya kuwa na viungo wazuri na washambuliaji wazuri bila walinzi wazuri.Ndio maana Arsenal amejaribu kuimarisha defence .
Umeongea vyema sana Mkuu.. Mwenye macho ameona.. Mwenye uelewa kaelewa.
 
Kingine kinachofurahisha na kushangaza ni kwamba magoli ya penalti kwa timu fulani yamepungua msimu huu ukilinganisha na msimu uliopita. Sijui sababu ni mkwara wa Saanya umesababisha au miamala imepungua nguvu?
 
Hapa nilikua namzungumzia forward bora kabisa ya kimataifa kuwahi kushuhudiwa katika, bwawa la Jangwani.. Donald Ngoma.
Basi kama ni hivyo basi ya Jangwani waachie Jangwani wenyewe, wao wanajua zaidi nani ni forward bora zaidi wa kigeni kuwahi kuwa naye: Mwalala, Ambani, Nonda, .......
 
Kwamba mpo vizuri halina ubishi lakini halimaanishi ubingwa moja kwa moja.

Kuna vikwazo mbele yenu. Hamfungi magoli mengi. Kuna yellow/red card kwenye mchezo hasa ukizingatia mna first eleven nzuri lakini kwenye benchi la sub si wazuri sana. Kuna wachezaji kuumia pia.

Zote hizo ni factors muhimu kulelekea ubingwa.

Hivi ulitegemea kama banda atacheza mpira mwingi kama ule jana.. na huyo ni sub.. mwinyi kazimoto.. hua napenda kumuita ball dancer.. sasa naye ni sub.. nadhani mnamtambua vizuri hasa hasa juma seif kijiko.. kuna mavugoal.. huyu rekodi zake tu zinatosha kujigamba.. japo yupo kwenye mapito.. kuna beki kisiki murshid.. ukitaka kupata habari yake muulize ayew wa Ghana alichomfanya katika mechi za kufuzu CAF.. kuna kiberenge hamad juma.. what more can I say.. kuna manyika jr n.k dah Sub wametimia sana.. Hivyo hilo suala la red card, sijui majeruhi havitatuzuia kamwe.
 
Ushindi wa kusua sua kila siku kigoli kimoja afu angalia yanga wana wafungaji wangapi....!!! Apo utajua ata mkichukua ubingwa... mwsho wenu chalinzeee
 
Kwamba mpo vizuri halina ubishi lakini halimaanishi ubingwa moja kwa moja.

Kuna vikwazo mbele yenu. Hamfungi magoli mengi. Kuna yellow/red card kwenye mchezo hasa ukizingatia mna first eleven nzuri lakini kwenye benchi la sub si wazuri sana. Kuna wachezaji kuumia pia.

Zote hizo ni factors muhimu kulelekea ubingwa.
Umeandika kama mwanamichezo. Factors ulizozisema zina athiri timu zote na sio special kwa Simba. Mfano hai mlipomkosa Ngoma kwa sababu ya kadi 3 njano dhidi ya African Lyon pengo lilionekana wazi kwani hamkuwa na plan B ya kutafuta magoli .
 
Kingine kinachofurahisha na kushangaza ni kwamba magoli ya penalti kwa timu fulani yamepungua msimu huu ukilinganisha na msimu uliopita. Sijui sababu ni mkwara wa Saanya umesababisha au miamala imepungua nguvu?
[emoji1] [emoji1] [emoji1]
 
Ushindi wa kusua sua kila siku kigoli kimoja afu angalia yanga wana wafungaji wangapi....!!! Apo utajua ata mkichukua ubingwa... mwsho wenu chalinzeee
Kajifunze kuandika ueleweke halafu rudi ujaribu kuandika tena.
 
Mkuu Sibonike gazeti bora la michezo kwa sasa linaloandikwa kwa lugha ya kiswahili duniani.. Msimbazi limezungumzia inshu ya upana wa kikosi.. Nawanukuu.. "Kinatoka Chuma kinaingia Chuma Kwa Sasa"
a8ed36472e06f42f313641c07f603364.jpg

... kwa habari zaidi jipatie nakala yako leo.
 
Hilo gazeti hata bure sichukui.

Kwani Mkuu, unategemea hilo gazeti litaandika nini zaidi ya ushabiki?

Wewe unasoma gazeti la Jangwani?
 
Hilo gazeti hata bure sichukui.

Kwani Mkuu, unategemea hilo gazeti litaandika nini zaidi ya ushabiki?

Wewe unasoma gazeti la Jangwani?
Mkuu mimi hua nadili na vitu bora.. Msimbazi ni gazeti bora kwa sasa kutokana na utafiti uliofanyika hivi punde.
Jagwani nilikua nalinunua sana hadi hivi sasa nalinunua.. si kwa kulisoma, bali hua nampelekea mama sayuni awafungie wateja wake vitumbua na chapati anazouza.
 
Kwamba mpo vizuri halina ubishi lakini halimaanishi ubingwa moja kwa moja.

Kuna vikwazo mbele yenu. Hamfungi magoli mengi. Kuna yellow/red card kwenye mchezo hasa ukizingatia mna first eleven nzuri lakini kwenye benchi la sub si wazuri sana. Kuna wachezaji kuumia pia.

Zote hizo ni factors muhimu kulelekea ubingwa.
Mkuu sibonike achana na hao malimbukeni , hawajui chochote zaid ya mihemko, Yanga itawadhihilishia soon ubora wake
 
Jifunze kiswahili kabla ya kudiriki kuwaita watu limbukeni.
Itawadhihilishia ndio nini?
 
Mkuu sibonike achana na hao malimbukeni , hawajui chochote zaid ya mihemko, Yanga itawadhihilishia soon ubora wake
Mda unaenda Mkuu.. hiyo soon itafika lini? Endeleeni kusubiri kutudhihirishia wakati sisi tunachanja mbuga.. Hadi hiyo soon yenu ifike.. sisi tutakua tushatangaza ubingwa kitaaaaaambo.
 
Back
Top Bottom