Kijiweni na Mashabiki wa Ndala

Kijiweni na Mashabiki wa Ndala

Mkuu unataka kutugonganisha kama mpira wa kona. Hapa tunatumia fake IDs, hilo unalijua fika. Unapotaka tujiunge kwenye makundi ya Whatsapp huoni kwamba tunafahamiana kiuhalisia? Unaweza ukafahamu kuwa kumbe mimi Makoye Matale ni jirani yake kabisa na Mkuu sembo lakini tukiwa hapa JF ni kurushiana madongo juu ya madongo!

Namsapoti Mkuu sembo, JF ni zaidi ya Whatsapp.
Atakuwa katumwa huyo. Atafute njia nyingine siyo hii ya bei rahisi kihivyo.
 
Acha kuuaminisha umma na uongo..Mfumo wa uendeshaji kabla za soka duniani ni mitatu tu

1.Ni mfumo wa wanachama, kama ilivyo Simba SC na Yanga Afrika

2.Ni umiliki, kama ilivyo kwa Moise Katumbi na Mazembe au Abromovch kwa Chelsea

3.Ni mfumo wa hisa, kama Manchester United kwa wamarekani

Ukondishaji hakuna, na kama kuna timu inafanya hivyo lete ubaoni hapa na data zake.. mimi ntaomba ban ya wiki moja JF.

Ingia kwa undani uone nini hawa wawekezaji wanachotaka hasa kwa hizi team, Mooo na Manji tofauti yao ni ndogo sana kijana, kiujumla mm siafiki anachotaka kukifanya Mo wala Manji kwa hizi team mbili kubwa Tanzania.!
 
Mkuu.. wewe jenga wasiwasi upande wako na Manji..ama kwangu sina shaka na MO kwasababu nafahamu uendeshaji klabu mfumo HISA ndo chagizo duniani kote kwa sasa

Kuhusu maslahi kila mmoja anapata kuanzia mwenye HISA, Klabu yenyewe vitu kama majengo, viwanja na wachezaji pia na wanachama

Sasa kama hivi sasa mimi ni mwanachama wa Simba SC je napata faida gani zaidi ya kushangilia tu.. Mkuu haturudi nyuma kwa mpango wa Hisa

Tafakari...!
 
Mkuu mwaka huu mbeleko hakuna na ikitokea point za mezani basi wewe utaathirika mno kuhusu Kessy na vibali vya Makocha

Cheza mpira acha ndoto..utapoteza muda
Mbeleko hununuliwa na abebaye, na kwa Yanga inajibeba yenyewe. Kwa hivyo wataendelea kujibeba kwa mbeleko walizonunua wenyewe: Lwandamina, Pluijm, Ngoma, Niyo, Tambwe ....... mpaka mwisho. Pointi za mezani si mbeleko, ni ukiukwaji wa kanuni bila ya kujali dhidi ya nani. Unapochezesha mchezaji ambaye hajakamilsha taratibu, ukikatiwa rufaa mbeleko unakuwa ni wewe uliyekiuka taratibu. Na kwa hilo mbeleko kuelekea ubingwa Jangwani ni Simba na Leone. Ya Kessy hayahusiki kwa sababu inayotakiwa ni rufaa iliyokatwa kwa wakati, si porojo za Rage. Au kama unahisi maneno yake ni kuntu basi usiishie hapo, kubaliana naye pia kwa kauli yake kwamba Wanasimba ni mb.......
 
Kiongozi, post yako hii inadhirihirisha unyonge na kukata tamaa kwako na pengine timu yako. Kusubiri pointi za rufaa a.k.a mbeleko kutoka timu kama African Lyon ni dhihirisho la kuonyesha mmeshakubali matokeo. Hata hivyo kila heri
Mbeleko hununuliwa na abebaye, na kwa Yanga inajibeba yenyewe. Kwa hivyo wataendelea kujibeba kwa mbeleko walizonunua wenyewe: Lwandamina, Pluijm, Ngoma, Niyo, Tambwe ....... mpaka mwisho. Pointi za mezani si mbeleko, ni ukiukwaji wa kanuni bila ya kujali dhidi ya nani. Unapochezesha mchezaji ambaye hajakamilsha taratibu, ukikatiwa rufaa mbeleko unakuwa ni wewe uliyekiuka taratibu. Na kwa hilo mbeleko kuelekea ubingwa Jangwani ni Simba na Leone. Ya Kessy hayahusiki kwa sababu inayotakiwa ni rufaa iliyokatwa kwa wakati, si porojo za Rage. Au kama unahisi maneno yake ni kuntu basi usiishie hapo, kubaliana naye pia kwa kauli yake kwamba Wanasimba ni mb.......
 
Mkuu mlikata rufaa pia dhidi ya Stendi United. Rufaa iliishia hewani. Kila mkipoteza pointi lazima kuwe na rufaa. Kuna muda wa pingamizi timu ipinge mchezaji kwenda timu nyingine bila kufuata taratibu.Jaribuni kupindisha sheria ili kukidhi mahitaji yenu kwa msaada wa TFF. Mlijaribu kwenye suala la Kessy ikabidi msalimu amri pamoja na kupata msaada kutoka TFF.
Huoni ajabu kila kesi ikiwa na maslahi na Yanga basi hiyo kamati inakutana haraka lakini ikiwa dhidi ya Yanga basi lazima ichukue miezi 6 tena timu husika ikomae kweli kweli.
 
Kumbe ya Kessy huyajui, alianza kulalamikiwa pale mlipo msajili na mkamchezesha hiyo ni kinyume na utaratibu za soka mjadala point hauna tija.. na kama utang'ang'ania ntakuacha tu kama mnavyong'ang'ania kukodisha timu, kwani maturubai yale (nukuu) Akilimali
 
Ha ha ha.. hadi hapo atakuwa ameelewa somo
 
Kumbe ya Kessy huyajui, alianza kulalamikiwa pale mlipo msajili na mkamchezesha hiyo ni kinyume na utaratibu za soka mjadala point hauna tija.. na kama utang'ang'ania ntakuacha tu kama mnavyong'ang'ania kukodisha timu, kwani maturubai yale (nukuu) Akilimali
Jawabu (response) ya malalamiko yenu kwa Kessy ni kifuta-machozi cha 50,000,000/-. Hata zikilipwa Karne ijayo, bado Kessy ni mchezaji halali wa Yanga. Kamati iliyotoa 'dau' hilo haikusema kwamba Kessy si mchezaji halali wa Yanga. Hii ya Ndanda na Leone subiri machungu yake, halafu Mzee Kil(i)omoni(ni) hamjui kiliomo nini kichwani mwake ddhidi ya njama za Mdosi kutaka kuitwaa timu kwa 'show money'!
 
Mathematically speaking, mwenye nafasi zaidi ya kubeba kombe ni Yanga. Kwa nini? Kwa sababu ushindi wa mechi unategemea ufungaji magoli. Mwenye uwezo wa kufunga magoli mengi ndiye mwenye uwezo wa kushinda mechi nyingi. Kufunga magoli machache na kushindaa mechi nyingi kunategemea mambo mawili tu, bahati (muda gani umefunga goli lako) na ukuta usiofungika hata iweje (mara nyingi kwa kuegesha basi kwenye ngwe yao). Simba haina ukuta wa aina hiyo, ndiyo maana wapinzani wanafika golini kwake na wakakosa magoli ya wazi. Yanga nao hali kadhalika. Tofauti yao ni kwenye ufungaji. Angalia takwimu uone nani anafunga zaidi. Hata kwa mantiki ya kawaida, mwenye kisu kikali ndiye anayekula nyama!

Kuna udhaifu kwenye uwiano wa hoja yako na uhalisia. KWANZA wewe mwenyewe unajua kuwa Simba ndio timu pekee iliyoshinda mechi nyingi. Wewe mwenyewe ni shahidi kuwa Simba ndio timu iliyoshinda mechi nyingi hadi sasa kuliko timu yoyote ktk ligi huku ikiwemo hiyo timu unayodai imeshinda magoli mengi. PILI wewe ni shahidi kuwa Simba ndio timu iliyokusanya pointi nyingi kutoka timu shindani katika kuwania ubingwa kwa maana ya Yanga na Azam.

Kama hiyo haitoshi, Simba ndio timu iliyokuwa na possession kubwa kuliko timu hizo mbiliza Yanga na Azam an pia kwa timu nyingine zote za ligi. Kwa uthibitisho rejea takwimu za mechi baina ya Yanga na Simba pungufu, Simba na Azam. Hoja yako ya kujilinda au bahati inakufa kifo cha mende. Leta hoja nyingine hii imepauka.

Mbeleko hununuliwa na abebaye, na kwa Yanga inajibeba yenyewe. Kwa hivyo wataendelea kujibeba kwa mbeleko walizonunua wenyewe: Lwandamina, Pluijm, Ngoma, Niyo, Tambwe ....... mpaka mwisho. Pointi za mezani si mbeleko, ni ukiukwaji wa kanuni bila ya kujali dhidi ya nani. Unapochezesha mchezaji ambaye hajakamilsha taratibu, ukikatiwa rufaa mbeleko unakuwa ni wewe uliyekiuka taratibu. Na kwa hilo mbeleko kuelekea ubingwa Jangwani ni Simba na Leone. Ya Kessy hayahusiki kwa sababu inayotakiwa ni rufaa iliyokatwa kwa wakati, si porojo za Rage. Au kama unahisi maneno yake ni kuntu basi usiishie hapo, kubaliana naye pia kwa kauli yake kwamba Wanasimba ni mb.......

Naona umechanganya madawa. Issue ya Rage imeingiaje hapa? Na kama kauli ya Rage kwenu inaonekana kuwa na maana kiasi cha kupigiwa upatu kila mara kwa nini mnachagua kauli hii pekee katika nyingi alizosema?

All in all kitendo cha kupigia hesabu pointi za mezani kutoka timu kama African Lyon na hapo hapo kuombea pointi za Simba zipokwe eti ndio Yebo ndio wawe matumaini ya ubingwa ni dalili ya kufisika kiushindani. Ngoja tuone mwendelezo wa ligi ya mezani naona uwanjani watu washaanza kukata tamaa.
 
Kuna udhaifu kwenye uwiano wa hoja yako na uhalisia. KWANZA wewe mwenyewe unajua kuwa Simba ndio timu pekee iliyoshinda mechi nyingi. Wewe mwenyewe ni shahidi kuwa Simba ndio timu iliyoshinda mechi nyingi hadi sasa kuliko timu yoyote ktk ligi huku ikiwemo hiyo timu unayodai imeshinda magoli mengi. PILI wewe ni shahidi kuwa Simba ndio timu iliyokusanya pointi nyingi kutoka timu shindani katika kuwania ubingwa kwa maana ya Yanga na Azam.
Ningekubaliana na hoja yako ya kwanza kama ushindi wa Simba ungekuwa si wa bahati, au Yanga isingekuwa inatoka sare kwa bahati.

Unapocheza na timu inayofika golini kwako kama unavyofika kwake (bila ya kujali umepiga pasi ngapi) ukakosa magoli ya wazi kama unavyokoswa wewe, ukakiuka misingi ya mchezo wa kiungwana (fair play) kwa kufunga goli pekee huku kipa akiwa anaugulia maumivu muda mrefu kaabla, ushindi wake haupaswi kuingizwa kwenye takwimu za kukadiria ushindi. Kwa nini? Kwa sababu hiyo siyo hali itayojitokeza kila mechi na kwa hivyo haipaswi kuwa ni sampling sahihi. Isitoshe, kama hiyo ni sampling sahihi, basi usiishie hapo.

Piga hesabu unafungwa kila baada ya mechi ngapi za mikoani na umebakiwa na ngapi za huko, piga hesabu unafunga goli kila baada ya dakika ngapi na unafungwa kila baada ya dakika ngapi na kwa hivyo unatarajia kupata magoli mangapi kwa mechi zilizobakia na utapoyagawanya kwa wastani utaishia na ushindi wa mechi ngapi. Fanya hivyo kwa timu zilizosalia na utaona unasimama nafasi gani.

Ama kuhusu Rage, kunukuliwa kwake kunaendana na maudhui ya hoja iliyopo. Itakuwa kichekesho nikimnukuu akisema maoni yako ni kikao cha arusi! Swala la pointi za mezani ni utaratibu wa msingi unaomhusu kila aliyeshiriki mashindano ya VPL, ndiyo sababu ya kuwa na kanuni.

Hata kwenye mashindano ya Kombe la FIFA linalostahili umri maalum, timu inayokiuka umri huo itapokwa ushindi hata kama ilishinda mabao mangapi. Umesahau yaliyotupata kwa Serengeti Boys?

Umahiri wa uwanjani unaanza na umahiri wa kuzijua kanuni za mashindano husika na kuizfuata itakiwavyo. Usipofanya hivyo utakuwa ndiye mbeleko ya kumbebea anayepewa ushindi.

Ila kwa taarifa yako, kwa uwezo wa Yanga, na kwa takwimu nilizokudokezea hapo juu, pointi hizo za mezani ni sunna (optional) tu, sio faradhi (compulsory) kwa Wanajangwani kuzidi kuumia kwapa kwa kuinyanyua tena ndoo ya ubingwa wa VPL kwa mara ya tatu.
 
Sheria za fair play zinawahusu Simba pekee yake?.Umefunga goli la mkono dhidi ya Simba,umefunga goli la mkono dhidi ya Mbao umefunga lingine kipa akiwa chini baada ya kusukumwa tena kwenye kisanduku chake.

Jifunze sheria za mpira ungezijua goli la Simba dhidi ya Ruvu JKT lisingekusumbua. Kipa katoka kwenda kucheza krosi kaupiga mpira akiwa chini imepigwa krosi goli likafungwa. Akitoka nje ya eneo lake ambako marefa wanapaita six anakuwa hana advantage ya kulindwa kama akiwa kwenye eneo lake la six.
 
Kwanza ujue tofauti bina ya fair play na technical foul. Wachezaji wanapon'gan'gania mpira popote uwanjani, inatokea mmoja kukiuka sheria, hata kama haitaishia kwenye goli. Mara nyengine hulazimika kufanya hivyo kama njia pekee ya kuziwia timu yake isifungwe au kuipatia goli timu yake. Ndio pale unapoona faulo fulani inashangiliwa na uwanja mzima. Ingawa ni faulo, uchezaji wa aina hiyo ni fair play.

Lakini mchezaji anapoanguka kwa maumivu popote pale, fair play inataka mwenye mpira autowe nje ili mwenzake agangwe. Kutofanya hivyo ndiyo kinyume na falsafa hiyo. Na huwa vibaya zaidi utovu huo wa uungwana (unfair play) unapoishia kuwa goli - hasa aliyeumi(zw)a anapokuwa ndiye mlinda mlango.

Goli la mkono la Tambwe linapaswa kukuzindua kwamba mchezaji yeyote anayejikuta kwenye mazingira kama yale anaweza kufanya hivyo na asibainike, kama alivyofanya Maradona dhidi ya Uingereza kwenye goli linaloitwa la Mkono wa Mungu. (Kutojiamini kwa TFF - sio utata wa goli lenyewe - ndiko kulikomfanya mwamuzi afungiwe, mbona aliyeruhusu la Maradona hakufungiwa?)

Hili la Tambwe linadhihirisha ninachokisema kwamba beki ya Simba si imara kama mnavyodhania. A chain is only as strong as its weakest link. Lifungwe kwa mkono au pua, beki ilimpa fursa Tambwe ya kufikiwa na mpira akiwa katikati yao, na hatimaye akawafunga. Ndio, akafunga bao; si limekubaliwa na refa? Au mnajidanganya kuwa silo kwa sababu hatimaye refa alifungiwa? Kwa tafsiri hiyo hata refa aliyechezesha Yanga na Prisons alifungiwa - ndio tuseme goli alilolikubali dhidi ya Yanga si halali?

Hiyo ya juu ni elimu ndogo niliyoona nikupe kwa kuwa ushabiki unaonekana kukutoa darasani kwa nguvu. Lakini fair play haikuwa hoja yangu ya msingi. Hoja yangu ya msingi ni kwamba takwimu zinaibeba zaidi Yanga kwenye ubingwa kulko timu nyengine yoyote.

Hata ukitoa hizo mechi za Yanga unazozilalamikia kwamba si sampuli wakilishi (representative sample) na ukaongeza hizo za Simba ninazosema nazo si sampuli wakilishi, basi bado takwimu zinaibeba Yanga. Yeyote anayetaka kuendeleza mjadala dhidi ya hilo, hoja yake iwe takwimu haziibebi Yanga.

Vinginevyo sitakuwa na haja ya kujibizana naye. Najua tayari wengine wameshaanza kukalia keyboards kuanza kulalamika kwamba hata huyo takwimu ni mpenzi wa Yanga! Washabiki wa Mnyama kwa kulalamika bhana!
 
Nikiwa nishaanza shamra za kusherekea ushindi mzito wa leo wa Simba S.C dhidi ya Ruvu.. Nipo kijiweni na mashabiki wa Ndala wakiwa wamenyong'onyea.. Kisa.. Mkata Umeme!!

Nasikia wakijadili kauli ya Kocha wao.. Kua Ndala wawe na uvumilivu na Mkata Umeme.. kwani jamaa alikua nje ya uwanja kwa mda wa miezi 6.

Hawa jamaa wamejiuliza maswali haya, wakakosa majibu;
1. Kabla ya kumsajili, Je walifahamu kua kwanini jamaa alifungiwa kucheza soka kwa mda wa miezi 6?
2. Kama walifahamu, kwanini walimsajili mtu ambaye hakua uwanjani mda mrefu?
3. Inakuaje Mkata Umeme analipwa zaidi ya milioni 5 akiwa benchi.. Huku wanaowapa ushindi mkiwalipa laki 8?
4. Twite alitimuliwa kisa umri.. Je mna taarifa Mkata Umeme ni kinda la miaka 36?

Wakuu zangu Sibonike Belo Nifah Guasa Amboni demigod Nyenyere juan de otaru libeva Blank page Konaball Mwana Mtoka Pabaya Bailly5 babake nasreen Frank Wanjiru Ulimakafu bila kumsahau ndugu yenu Makoye Matale... naomba mnipatie majibu.. niwape hawa Ndala kindakindaki wenzenu.

Muhudumu fanya mambo haya mawili mda huu, kipindi nasubiri majibu;
1. Niongezee kinywaji
2. Ongeza sauti ya huo wimbo... "... ama kweli wajinga ndo waliwao.. kekundu.. kekundu.. kekundu... ".
Afazali mkate umeme amesema miaka yake ya ukweli kuliko huyu mkata maji mwenye miaka 22!!!
 
Attachments

  • images.jpg
    images.jpg
    4.1 KB · Views: 20
Tatizo lako unaandika uongo ili kushibisha hoja yako. Refa aliyechezesha Yanga na Prisons alifungiwa lini?
Yanga alishinda hiyo mechi iliyochezwa Mbeya kwa goli 1.Prisons walikosa penalti kwenye mechi hiyo.Hilo goli la Prisons lilitoka wapi mpaka refa afungiwe?
Takwimu hazifanyi timu ipate ushindi kama unavyotaka wewe. Matokeo ya uwanjani ndio yanaamua nani awe bingwa.Ndio maana Leicester kawa bingwa wa Uingereza na Ureno bingwa wa Ulaya licha ya takwimu kuonyesha kwamba ni underdogs.
 
Samahani Mkuu kwa kuteleza, ingawa naamini kwamba hoja yangu umeielewa kwamba miongoni mwa marefa waliofungiwa ni wa Mbeya City dhidi ya Yanga. Mantiki na maudhui ya hoja mama inabaki palepale.

Kuhusu takwimu kwamba sizo zinazoamua mshindi, unapaswa kuliona hilo kwa pande zote mbili. Maana hata nyinyi wapenzi wa Mnyama mnajinasibu kutwaa ubingwa kwa sababu ya hizohizo takwimu.

Kwa taarifa yako, huku kushinda mechi nyingi kuliko timu zote, kufungwa mabao kidogo kushinda timu zote mnakojisifia ndio takwimu zenyewe. Ushindi haupatikani kabla ya mechi kuchezwa, na kwa hivyo - kwa maelezo yako - tungojee mpaka mechi zichezwe ndio tutangaze ushindi. Uko sahihi.

Lakini kama washabiki huwa tuna hamu ya kukadiria nani atakuwa mshindi. Na bila ya takwimu, utabiri huo unakuwa ni matamanio zaidi kuliko makisio. Kwa hivyo kwa matamanio ya Wanasimba, Mnyama ni bingwa. Kwa makisio yatokanayo na takwimu, Yanga ni bingwa.
 
Mkuu mlikata rufaa pia dhidi ya Stendi United. Rufaa iliishia hewani. Kila mkipoteza pointi lazima kuwe na rufaa. Kuna muda wa pingamizi timu ipinge mchezaji kwenda timu nyingine bila kufuata taratibu.Jaribuni kupindisha sheria ili kukidhi mahitaji yenu kwa msaada wa TFF. Mlijaribu kwenye suala la Kessy ikabidi msalimu amri pamoja na kupata msaada kutoka TFF.
Huoni ajabu kila kesi ikiwa na maslahi na Yanga basi hiyo kamati inakutana haraka lakini ikiwa dhidi ya Yanga basi lazima ichukue miezi 6 tena timu husika ikomae kweli kweli.
Kweli Mkuu. Yanga ndio timu pekee hapa nchini iliyonufaika na kanuni ambayo hata kupitishwa kwake kulikuwa hakujatangazwa: kanuni ya kuchagua mechi za kupisha adhabu ya kadi tatu za njano au moja nyekundu. Baada ya kunufaishwa nayo tu, kanuni hiyo ikafutwa. Ni bahati mbaya tu kwamba hawakufanikiwa kutwaa ubingwa, ulioenda kwa watani zao badala yake!
 
Back
Top Bottom