Kikao cha CCM: RA Atema Cheche "Nitajiuzulu...."

.

Keil umenena, niko nyuma yako kwa asilimia 100% but only if Watanzania wa vijijini nao watafunguliwa macho na masikio yao, kwanza kwa kuelimishwa kuwa CCM haina hati miliki ya kuitawala nchi hii na mwenye uamuzi wa mwisho ni mwananchi mwenyewe. Watu waone madudu ya CCM na Kusikia huyo mbadala anakuja na ahadi gani.

Kama mpenda demokrasia ya dhati, bado nasikitishwa na upinzani uliopo, ndio maana nasema, kama upinzani wenyewe ni huu, basi CCM itatawala milele!.

Naungana na wewe pia kwenye hoja ya wale wenye fikra za mageuzi ya kweli, hatathubutu kugombea CCM kwani kwa hapa CCM ilipotufikisha, chama chochote kikija na sera nzuri za kueleweka, kampeni kubwa ya changing mind set za Watanzania kama ile ya Obama ya 'Change we can Belive in'.. 2 Wapinzani wote wakamkubali Dr. Slaa akasimama na Muungwana, 2010 CCM Chali!. Very unfortunately chama kama hicho bado hatuna.

Hivyo katika mazingira yaliyopo ya upinzani legelege, CCM bado ni Chama dola. Hivyo kwa maeneo ambayo hayana chachu ya mageuzi, then the right forum ni kugombea kupitia CCM halafu wachange from within kwa kuitumia ile formular ya 'if you can't beat them, join them'.
 
RA, kuwa mwangalifu na kile unachokiomba. Yanaweza kuja mengi zaidi ya Kagoda na Richmond......then what? Watanzania hawaitaji tu ujiuzuru bali utumikie kifungo na kurudisha pesa zetu, kisha urudi Iran. That's all.
 
DAWA ya mpasuko wa wabunge ndani ya CCM inaonekana kuwa ngumu, kutokana na kamati ya wazee wa CCM kushuhudia uhasama wa wazi, huku wakiendelea ‘kupashana’ kwa lugha kali.

Kamati hiyo inayoongozwa na Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi imemaliza kazi yake, lakini wadadisi wa mambo ndani ya chama hicho wamekiri kuwa chuki na uhasama huenda visimalizike.

Habari kutoka ndani ya kikao hicho zilisema Katibu wa Itikadi na Uenezi, John Chiligati, alisema chanzo cha mpasuko ni wanamtandao ambao wamepasuka katikati hivyo kuwepo kundi la Edward Lowassa na Samuel Sitta.

Inadaiwa alisema watu hao ndio wamesababisha mpasuko mkubwa hivyo akashauri kamati hiyo ya wazee wa CCM, iwaite Lowassa, Sitta na watu wao wa karibu, Rostam Aziz na Katibu Mkuu, Yussuf Makamba.

Mpasha habari huyo alidai kuwa iwapo kamati hiyo itakaa nao ili kupata ufumbuzi wa kudumu, pia mmoja wa wajumbe, Abdulrahaman Kinana, asaidie kwa karibu. Ilielezwa kuwa Chiligati anaamini kuwa Kinana anaweza kusaidia kuondoa mpasuko huko kutokana na kuyajua makundi hayo vizuri.

Lakini wapasha habari hao walidai kuwa mbunge wa Nzega, Lucas Selelii alisema chanzo cha mpasuko huo ni Bunge kukubali kuunda kwa tume ya kuchunguza kampuni ya kufua umeme ya Richmond. Alisema wabunge tangu wakati huo waligawanyika wakiwamo waliounga mkono kuundwa kwa kamati na wengine wakawa wanapinga na akatoa mfano wa hoja ya mbunge wa Ukonga, Dk Makongoro Mahanga.

Mbunge huyo pia alisema kutokana na mgawanyiko huo ndiyo maana kamati ilipata wakati mgumu wa kutimiza majukumu yake ikiwamo kunyimwa baadhi ya nyaraka na watendaji wa Serikali kwa kile anachoamini kuwa yalikuwa maagizo kutoka kundi la Lowassa.

Inadaiwa alimtetea Spika Sitta kuwa hakuwa na hila kuunda kamati hiyo na akaeleza kuwa hata baada ya kamati kukamilisha kazi yake ilipeleka kwa Rais ripoti hiyo kabla ya mwezi mmoja kuwasilishwa bungeni. Alisema hata vyombo vya ulinzi na usalama vilikuwa vinajua kinachofanyika na kamati hiyo, hivyo akasema hakukuwa na mipango ya kuwaonea baadhi ya watu kama ambavyo baadhi ya wabunge wanataka jamii iamini.

Mbunge wa Kishapu, Freddy Mpendazoe, inadaiwa kwamba alishangaa kuwapo viongozi ndani ya CCM ambao wanapinga wabunge wanaopigia kelele ufisadi na akasema kama kufanya hivyo kwa mbunge wa CCM ni dhambi, basi chama hicho kibadilishe Katiba inayotamka kuwa rushwa ni adui wa haki, sitatoa wala sitapokea rushwa. Mbunge huyo pia alishangaa viongozi wa CCM ambao wanamshambulia Mwenyekiti Mtendaji wa IPP Reginald Mengi kuwa si wanachama wa CCM wakati wanakwenda kumwomba fedha za uchaguzi.

Wakati Mpendazoe anatoa shutuma hizo, Makamba alisimama na kutaka thibitisho wa madai hayo ndipo mbunge huyo inadaiwa akasema anazo taarifa zote. Lakini Mwanasiasa mkongwe Kingunge Ngombale-Mwiru aliomba mwongozo wa Mwenyekiti na kuhoji sababu ya mbunge huyo kumtukuza Mengi kwenye kikao hicho, wakati si mbunge ndipo Mpendazoe akajibu kuwa anafanya hivyo kwa vile kuna viongozi wa chama hicho walipinga wabunge wanaochangiwa fedha za Vicoba na Mwenyekiti huyo wa IPP.

Naye Mbunge wa Kigoma Mjini, Peter Serukamba alisema chanzo cha mpasuko wa wabunge ni madaraka na lengo ni kuwaondoa baadhi ya watu kama Lowassa kwenye ulingo wa siasa.

Naye Rostam Azizi alisema ni jambo la aibu wabunge wa CCM kuitwa mbele ya kamati ya wazee wa CCM na jambo hilo akasema halifai kujivunia kwani linaonesha namna chama hicho kilivyogawanyika. Alisema tuhuma juu ya kampuni ya Kagoda inayodaiwa kuwa ni yake hazina ukweli wowote na wanaofanya hivyo wanamsulubu bure kwani si ajenda ya CCM bali ni ya Chadema, akashangaa iweje wabunge wa CCM washikie bango jambo ambalo si ajenda yao. Alisema kwamba yeye anaamini kuwa kumsulubu yeye au Lowassa juu ya suala la Richmond ni kukikusulubu chama.

Rostam pia anadai kusema kwamba mpasuko kati ya wabunge na wabunge wa chama hicho ni uchaguzi wa mwaka 2005 baada ya watu kushindwa kupata urais ndipo wakaanzisha vita na kundi la watu ambao waliingia madarakani.

Mpasha habari alisema Rostam alisema kwa masikio yake aliwahi kuwasikia baadhi ya wabunge wakiapa kuwa wataiaibisha Serikali ya sasa wakati wakinywa chai kwenye mgahawa wa Bunge. Kada huyo wa CCM anadai pia kueleza kuwa kutokana na hali hiyo Sitta akawa adui mkubwa wa Lowassa na yeye mara kadhaa alijaribu kuwapatanisha, lakini ilishindikana
hivyo Sitta na wabunge wake wakawa na kasi ya kumfanyia hujuma Lowassa likiwamo suala la Richmond.

Kuhusu ripoti ya Richmond, Rostam alisema tangu mwanzo kulikuwa na hila mbaya ndio maana yeye alinyimwa fursa ya kutoa maoni yake mbele ya kamati hiyo.

Lakini Rostam pia alienda mbali na kutaka chama kuanzia sasa kiwachukulie hatua kali wabunge wanaoikosoa Serikali. Kuhusu kuumizwa kwake kisiasa alisema licha ya kuwa ameumizwa sana kuhusu jambo hilo yeye tayari ameshasamehe, kwani Mungu amemjaalia moyo wa kusamehe.
 

Mkuu wa idara,

Wakati sisi tunakazania kukabana makoo na kulipiza visasi, waungwana Maalim na A.K wameamua kukutana faragha na kupata gahawa kidogo! (tutazamie Azimio la Zenji Party II?) nadhani washajionea kuwa nchi hii haina mwelekeo tena mara leo E.L kesho R.A kesho kutwa lioness Sofia. Hivi nani ni nani? nani wakuleta order katika nchi hii kwa sasa? inasikitisha kwakweli..

Amani.
 
Bantugbro haya ya kuanza kupachikana majina ya Mkuu wa idara yanatokea wapi?.

Hili la kukutana Maalim na AK ni ishara nzuri sana kwa siasa za Zanzibar. CUF itangaze kumtambua AK kama rais wa ZNZ, Karume awateu wale wawakilishi wawili wa CUF barazani akiwemo Juma Duni kwa kipindi kifupi kilichobakia, utekelezaji wa muafaka uridhiwe, ZNZ mambo mswano, kazi sasa ni huku kwetu bara, 2010 moto!
 
kitu mhimu cha kujiuliza ni kwanini mambo haya yote yaibuke baada ya taarifa ya dr mwakyembe? in maana haya hawakuyaona kabla ya Februari 2008? hamuoni kwamba chimbuko la yote ni baada ya wakubwa kukamatwa pabaya na kwamba wanachokifanya ni kujaribu kuzinusuru nafsi za walioguswa na maazimio hayo 23 ya bunge?
 
Jamani bunge lilitoa muda ktk kujadlili wengine walilia wameonewa. Lakini kwakuwa mkulu yumo hili ngonjera halitaisha isipokuwa km tukimweka raisi mwingie 2010
 

mmmh! jamani haya maneno ya Rostam yanaonyesha kuwa jamaa ni mtu hatari sana, either ni mjinga sana au ame-capitalize ktk ujinga wa wabunge wetu. Haya maneno anatamka mbele ya Mwinyi na wabunge.
 
.


Huyo samwel sita na john malecela wamekuwa madarakani kuanzia lini? wamefisadi kiasi gani?
na leo nini kilichowagusa na kujiita wapiganaji?hamuoni kwamba ni interest binafsi.

huyu mwakyembe,usafi wake nini?kama ni msafi basi ahamie chadema.hizo kelele zake kwenye vyombo vya habari vitatusaidia au ndiyo anaendelea kuwaangamiza wana kyela.Jaman achen utani,kyela iko chini sana.hakuna kitu kule.hakuna ata A'level moja.taabu.
 
Mkandara, sisi wana JF tunagombea kipande cha mkate na nani ili tushibe?mbona tunapiga kelekele kila siku?

Hasikudanganye mtu kaka yangu.hakuna anayekuwakisha wewe pale.wewe mwenyewe umekiri kuwa ccm sio wasafi na leo hii hao hao unasema wanakuwakilisha wewe kitaifa?kwali hapa kuna kazi.samwel sitta amekuwa kwenye madaraka kuanzia lini?alishindwaje kukuwakilisha wewe tangu mwanzo?ameshituka nini?amuka ndugu yangu.

Hakuna taabu usipo support,lakini mtu anapimwa kwa matendo yake na si vinginavyo.wananchi wengi wameelewa na wameishaona kuwa wanadanganywa na ukomedy wa waheshimiwa.
 
Huyu ROSTAM AZIZ ndiye aliyeifikisha nchi hapa ilipo. Ni mgeni aliyekuja kutoka Uajemi ili kuwaangamiza watanzania baada ya kuwapora raslimali zao akishirikiana na watu wenye uroho wa utajiri wa kupindukia kama vile LOWASSA. Hawa wengine wanaom-support kama Sofia Simba, Makongoro Mahanga, Kingunge, n.k. wanaambulia makombo tu ya akina ROSTAM na LOWASSA.
Tunafahamu 'war chest' yao ni kubwa na ndio maana unaona watu kama akina Sofia Simba wanaropoka ovyo na kujishushia hadhi kwani wana uhakika wa malipo mazuri kwa kazi yao chafu.
Sasa sisi wana wa nchi hii tunasema hivi: Enough is enough! Tunaingia rasmi kwenye mapambano ya kutetea uhuru wetu na raslimali zetu. Kwa wale wapiganaji wa kweli maelekezo yatafuata... Stay tuned.
 

Haya ndugu yangu Pasco umekataa ukuu wa idara basi wee!

Kwakweli tuwaache tu huko zenji waendelee na shughuli zao maana bara kazi ni nzito sana kipindi hiki. Soon tutaanza kutoana macho, ni kiasi cha mwendawazimu mmoja tu kulianzisha!. Juma Duni ni mwanasiasa mzuri sana chuki tu ndo zinatufanya tushindwe kumtumia kwa maendeleo yetu wote.

Amani
.
 

na ni uumbavu wa viongozi na waasisi wa taifa hili kuyajua haya yote na kumuacha mpaka leo anafika hatua hii..we need to blame ourselves first
 
Kwako wewe huo utumbo aliosema rostam ndio AMETEMA CHECHE!!! and you invite us to share that gabbage!you r so foolish!!!
 
this is so insane, Hizo tume zote zilizoundwa na kutoa report zimeishia wapi!! watanzania tunafanywa wajinga!!
 
Hizo pesa zote zinazotumika kuunda tume ambazo hata matokeo ya uchunguzi wao yakitolewa hayakubaliki/kufanyiwa kazi, si zingetumika kuboresha huduma ya jamii? Kwa mfano kuweka CT-scanners katika hospitali zote za mikoa? MRI scanners katika hospitali zote za rufaa? Na mambo madogo tu kama gloves, nyuzi nk?

Ni aibu mtu unapofanya kazi huku katika hospitali za nchi za nje, na kuona mambo ambayo kwa kweli serikali ya TZ ingekuwa na nia tu, na nyumbani yangewezekana.

Kweli tunahitaji "damu mpya"...

Hivi mashuleni watoto wanapofundishwa uraia (civics) huwa swala la "patriotism" linagusiwa? Maana hio ndio namna ya kuandaa damu mpya itakayogeuza mwelekeo wa Tanzania
 
hata hao wa mjini wenye uelewa mkubwa hawapigi kura na wakienda kupiga kura wanasema sasa mimi nimpigie nani "bora zimwi ulijualo"
 
..halafu jifunze kuandika majina ya watu vizuri!! ulisoma wapi wewe darasa la kwanza??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…