Kama unataka kugombea Ubunge kwa sababu huridhiki na hali halisi ya Utawala uliopo na unataka kuleta mabadiliko ktk utawala basi jiunge na Upinzani wa sio kuwaletea wananchi mfumo ule ule wanaoupiga vita..Kyela haikuanza kutawaliwa na Mwakyembe, mapungufu ya Kyela hayakuanza miaka mitano iliyopita isipokuwa ni mlolongo wa viongozi wa CCM waliwakilisha wananchi wa Kyela kushindwa kuwaletea mabadiliko..And I believe wee pia utakuwa katika hesabu ya viongoz hao kwani changes haziletwi na kichwa kimoja isipokuwa policies za chama za chama kinachoongoza
Mkuu Mkandara,
Hoja yako ndiyo niliipigia sana kelele zama zile za msuguano wa wana-Kyela mara baada ya mwana JF kutangaza nia ya kugombea.
Kwa mazingira yaliyopo ndani ya CCM hivi sasa, kweli mtu ambaye ana nia ya dhati ya kuleta mabadiliko anaweza kwenda kugombea kupitia CCM? How many times wabunge wa CCM wamefungwa midomo wasiseme maovu ya wenzao ama ya serikali? Tena wengine kwa kutishiwa maisha.
Hivi kweli tuhuma inamhusu Makamba, ama RA au EL, utaingia kwenye vile vikao vya wabunge wa CCM uombe ridhaa ya kuongelea hoja hiyo Bungeni na uruhusiwe? Nape Nnauye isingekuwa huruma ya Muungwana leo hii asingekuwa mwana UVCCM wala mwana CCM, kisa aligusa tuhuma za kigogo wa CCM. Chama kimejaa untouchables (miungu watu) ambao hutakiwi kuwasema wala kwenda kinyume nao vinginevyo unaweza kufungishwa virago.
Hao wanaoitwa wapiganaji wameibuka kuinusuru CCM baada ya kuona chama kinapoteza umaarufu mbele ya wananchi. Baada ya Dr. Slaa kumwaga radhi ya LIST OF SHAME na Zitto kupeleka hoja ya Buzwagi ndipo akina Mama Kilango wakaibuka. Mama Kilango akiwa Bungeni alisema hawezi kukubali akae kimya awaachie akina Slaa na Zitto wapate umaarufu kwa kuibua kashfa na hoja nzito nzito, kisa anaogopa kushughuliwa na Chama ama serikali. Je, leo hii hao wapiganaji wanaitwaje ndani ya CCM? Hata kama una ka-doa kidogo, unaweza kujikuta unatwishwa kashfa ya mwaka 1947 ili kukunyamazisha usiseme. Ukiwauliza walikuwa wapi hawakukushughulikia, hawana jibu la kukupa.
Sasa hivi kamati ya Mzee Mwinyi inatapatapa tu, hawajui watachukua kipi waache kipi.
Mama Simba tayari ameishasema ndani ya CCM hakuna aliye msafi, kwa hiyo hata yeye mwenyewe ni mchafu na JK nae ni mchafu. Kauli hiyo ina maana kubwa sana kwa wale wenye nia ya kuingia kwenye siasa.
Nikimsikia kijana anasema anakwenda kugombea Ubunge kupitia CCM ninamuona ni opportunist tu kwa kuwa kama yeye ana nia safi na dhamira njema, hawezi kwenda kujichanganya na waliovunda ama kuoza kabisa. Hivi kweli kama mtu ni msafi anaweza kwenda kukaa jalalani ama kujichanganya na wachafu? Umeambiwa kabisa hili ni jalala, ni sehemu iliyojaa takataka, bado mtu anakwenda kukaa hapo hapo. Hapo lazima ujiulize sana kama kweli mtu huyo ana nia na dhamira ya kweli ya kuwatumikia wananchi.
Hivi, ili ushinde Ubunge ni lazima upitie CCM? This is the opportune time for young men and women who wish to vie for MP posts kuingia kazini kumwaga sera za kueleweka. Unajua huu uchafu ambao CCM wanapakana sasa hivi utakuja kuwasumbua sana kuusafisha ikifika 2010, labda kwa kuwa ni mafisadi watatumia hela za ufisadi ili washinde. Lakini kama kuna mtu yuko serious na mapambano ya kweli, watanzania wa sasa wanasomesheka vizuri tu na wanaelewa. Ujinga unaoendelea ndani ya CCM ni faida kwa upinzani na wale wanaotaka kuingia kwenye siasa kupitia upinzani.
Mabadiliko ya kweli hayataletwa na hii CCM ya JK, EL na RA. Basically naweza kusema ni CCM ya RA na EL. JK ni boya tu amewekwa pale kama Mwenyekiti, lakini wenye final say ni akina EL na RA. Ndiyo maana hakuna lolote la maana linalofanyika, mikutano yao imekuwa ni kumbi za mipasho utadhani watu wako rusha roho pale Lango la Jiji.
NB: Kumradhi mwana JF ambaye ulitangaza kugombea kupitia CCM. Niliahidi kwamba ukishinda Ubunge nitaendelea kukumbusha mabandiko yako ya hapa ndani, unless na wewe upotee kama akina Dr. James Msekela ambao kwenye TANZANET walionekana wafurukutwa na walipoingia kwenye system wamemezwa na wamekuwa mute kama hawapo.