Kikao cha CCM: RA Atema Cheche "Nitajiuzulu...."

Kikao cha CCM: RA Atema Cheche "Nitajiuzulu...."

Mh. Zito please don't do this. Hawa wabunge wa viti maalumu wengi ni mamluki na mnavyozidi kuwaongeza mjue mna punguza nguvu ya wabunge wawakilishi wa majimbo linapokuja suala la ku-vote.

ndio haswa maana yake...viti maalumu wanatoka CCM, hao wa majimboni na wapinzani wakileta matata, viti maalumu wana sawazisha
 
ndio haswa maana yake...viti maalumu wanatoka CCM, hao wa majimboni na wapinzani wakileta matata, viti maalumu wana sawazisha

Tupo 44 kati ya 322. Twafanyaje?
 
kwa hiyo bora ufe hata leo ili RA asiendelee kuwepo? I hope God is not in the listeni mood right now.

Mkuu Carmel,

No please, I did not say God should listen and act now!!! I need this to happen when it is closer to 2015 and on condition that RA is likely to become our next top boss!!!!

Tiba
 
You are very wrong. It is more to that. Line up towards 2015. Hafi maji yule, japo kwa sasa!

Mhe. Zitto kumbe hata wewe unalikubali hili kuwa RA ni King Maker?. Wakati ulipotishia nyau kwa Mbowe, mengi mabaya yalisemwa juu yako likiwemo la kupokea kitita toka kwa jamaa huyu kilichokupatia makazi eneo la vibopa na kutesa na mashine za ki hollywood. Are you part and parcel?.
 
Kwa mtaji huu CCM wanako elekea ni kuuza nchi kama pesa ina nguvu kiasi hiki mpaka wabunge walio chaguliwa na wananchi kihalali wanakubali kununuliwa kwa fedha za kifisadi basi tunako elekea tutaanza kuchapata makonde.

Mkuu Fidel, heshima mbele. Hawa wabunge wetu si lolote si chochote wote ni waganga njaa tuu na ndio maana hawaoni kuwa kuna conflict of interest wao kuwa wajumbe wa bodi za mashirika na kung'ang'ania kwenye bodi za benki against laid down BOT regulations yote inaonyeshsha jinsi wasivyokuwa na maadili na waroho wa pesa. Mafisadi watamwaga fedha na Mr. Six hatajua kitu kilichompiga!!

Huyo EL kutokuwapo bungeni wakati huu ni mkakati tu, hana ugonjwa wowote.
 
Hapa sio Rostam au Rowasa hapa,Hapa ni je tume ya Mwakyembe ilisema kweli au?
Maana hawa kina Mwakyembe nao walikuwa na maslahi yao ktk umeme wa upepo singida sasa iundwe tume kuwachunguza hao kina mwakyembe
Mwenyekiti awe Slaa au Zitto
 
Mhe. Zitto kumbe hata wewe unalikubali hili kuwa RA ni King Maker?. Wakati ulipotishia nyau kwa Mbowe, mengi mabaya yalisemwa juu yako likiwemo la kupokea kitita toka kwa jamaa huyu kilichokupatia makazi eneo la vibopa na kutesa na mashine za ki hollywood. Are you part and parcel?.

Siasa za Tanzania zina mengi tusiyoyajua na wengi tunajadali tunayoyasoma kwenye magazeti ambayo huwa yamechujwa na hata kutiwa chumvi. Nakubaliana na mengi unayoyasema humu kwani unasema realities na sio hisia.

On me, sitaki kujitetea. wenye proof waweke tu hapa! Uzushi, Majungu na fitna ndio utamaduni wa siasa za Tanzania. Mtu aweza kuanzisha uwongo na ukazunguka mpaka yeye mwenyewe akauamini na kusahau alitunga yeye!
 
Mkuu Carmel,

No please, I did not say God should listen and act now!!! I need this to happen when it is closer to 2015 and on condition that RA is likely to become our next top boss!!!!

Tiba
offcourse he can never be a top boss but a ccm sponsor, he will always be.
 
Hapa sio Rostam au Rowasa hapa,Hapa ni je tume ya Mwakyembe ilisema kweli au?
Maana hawa kina Mwakyembe nao walikuwa na maslahi yao ktk umeme wa upepo singida sasa iundwe tume kuwachunguza hao kina mwakyembe
Mwenyekiti awe Slaa au Zitto

Sitaki. Hayo mambo ya CCM wayamalize wenyewe. Bunge tulimaliza kazi yetu
 
Ulipuaji wa RA kwa spika sita hauna tofauti sana na wa Sophia Simba kwa Kilango. Wote (RA na Simba) wanazungumzia maisha binafsi ya Sita na Kilango.Wakati Sita na Kilango wanatilia mkazo maazimio ya kamati ya Richmond ambayo ni faida kwa Taifa. Nionavyo RA na watu wake wameamua kuja na "character assasination" Kama mbinu ya kujisafisha wa waTZ....lakini is too late!

Mwisho..Hivi RA ni nani kwa taifa mpaka aombe kuundiwa Public inquery ndio ajiuzuru? naomba kutoa hoja
 
ndugu zangu hawa wanasiasa wanatuchanganya sana
wameiba sasa wameona ndio wakati wa kutueleza ni kwa vp walivyo chota mahela
na nani aliiba alipewa na nani, na kwa stail hii hakuana mtu anaye aminika hata mmoja nchii hii. nyerere peke yake ndo alikua safi na ataendelea kua safi hawa waliopo sasa ni wachafu tu .ndio maana hata chama cha wakulima na wafanyakazi kinachukua misaada na magari kutoka kwa mafisadi halafu wanajifanya wanamfungulia mashitaka hapa hata fumgwa mtu mwisho wa siku uchaguzi utapita then tutabadilishiwa nyimbi tutasaha
 
RA too late mkuu jipange upya
.

heheh. Huu ndiyo muda wenyewe,hakuna msafi pale ndugu yangu.wote ni njaa kali na hao wapiganaji ni kwamba wamekosa nafasi ya kufisadi.
 
uzushi ule ule. Simply prove.

sijui ni lini na ilikuaje Mh. Zito ukaanza kuhusishwa na hizi Blah blah, kwa kweli zinakinaisha na zinafifisha juhudi zako zakuaminiwa na wadau katika siasa, labda kwenu kigoma ambako jana ulieleza kua bado unnanguvu na unaaminika. hongera.

Dunia nzima siasa ni mchezo wa wajanja, kosa dogo hukughalimu sana, mimi nakushauri jitahidi kukwepa mabalaa yanayoweza kuondoa imani ya wadau wa siasa kwako.

Kiburi cha Lowasa, RA na sasa Sofia Simba ni matokea ya mfumo wa kuleana, na kuogopana uliosababishwa na siasa za kupendeleana , kwa kweli Sofia ni mama alieprove namna gani pesa huondoa haya , anaposimama na kujeli watu wote wanaopiga kelele za ufisadi anamtukana hadi Rais wa Jamuhuri.

Mwishoni anamalizia kwa ksema kwenye CCM HAKUNA ASIE FISADI, HAPA NDIPO ANAPOUTUSI MFUMO WOTE ULIOWAWEKA MADARAKANI, KUANZIA rAIS HADI MWENYEKITI WA SERIKALI YA MTAA WA CCM.
 
Siasa za Tanzania zina mengi tusiyoyajua na wengi tunajadali tunayoyasoma kwenye magazeti ambayo huwa yamechujwa na hata kutiwa chumvi. Nakubaliana na mengi unayoyasema humu kwani unasema realities na sio hisia.

On me, sitaki kujitetea. wenye proof waweke tu hapa! Uzushi, Majungu na fitna ndio utamaduni wa siasa za Tanzania. Mtu aweza kuanzisha uwongo na ukazunguka mpaka yeye mwenyewe akauamini na kusahau alitunga yeye!

Asante Mhe. Zitto, keep on being you, credibility yako iko juu na itaendelea hivyo kama nawe utaendelea kuwa hivyo, tatizo siasa ni mchezo mchafu, hata usipowachafua wengine, wewe utachafuliwa. Nimeumiss sana uwepo wako Dodoma bunge hili, lakini tuko pamoja.
 
Bhaghosha,

Napenda kujua kitu hapo kwani mie nadhani hawa wana CCM wana lao jambo ndani ya serikali hii maaana tokea marumbano yaanze the maini Issue hapo na inayotawala sana ni UCHU WA MADARAKA na UTAWALA MBOVU WA VIONGOZI ni dhahili ilo sawala liko wazi:

Sophia Simba kasema hoooo wabunge wengine waliahaidiwa Uwaziri na wengine vyeo mbali mbali sasa hawakuvipata na ndio chanzo cha kuumbuana na kuharibiana hapo ni dhahiri kuwa viongozi wetu hawana uadilifu wa kuwa viongozi hata kidogo na hilo ukimuuliza sophia simba alithibitishe wazi kwa wananchi na nashindwa kumwelewa mpaka leo anapiga domo tu hatoi facts kwa watanzania wajue anayo yasema ni facts au propaganda za kisiasa na hajui ni yupi wa kumtetea ni bendera fuata upepo, sijamuelewa Sophia simba mpaka hapo Sophia Simba.... Must GOooooooo!

RA nae kaja na hoja ile ile na kutuonyeshea kweli ni Madaraka ndio tatizo hapo na inatuonyeshea dhahili EL alivyokuwa akitenda kazi zake na je kama kweli ndizo izo facts wanazotoa ati alikataliwa kitu fulani basi ni viongozi wetu hao hao hawana uadilifu wa uongozi na niwanafiki kuwa EL alimkatalia hiki mara kile.

Hii ni dhahili ni utawala mbovu serikali haikuewa na mikakati endelevu ya miaka 10 au hata basi miaka 5 ya baaada wafanye nini ili kujengea viongozi mazingira mazuri ka utendaji kazi na kwa wananchi wao walio wachagulia. Hapa dhahili wanajitendea wao na sio kwa manufaaa ya nchi, RA hebu tupe facts na tuachane n a propaganda za chuki kwani ni wazi.

Kama kweli wewe na EL sophia simba na wengineo inawakela sana kusutwa sutwa si mwachie hayo madaraka kwani ni yenu au ni mpo hapo kwa kura za wananchi walio wachagu kwa maisha haya EL, S. Simba na RA msema kweli na mcha mungu nyie mumepungukiwa na nini katika maisha haya ya Kitanzania???? Kiuchumi mko shwari sasa nini kujidharirisha kwenye jukwaa la siasa kama kweli mwaona ni kero kidiplomasia NG'ATUKENI hizi nyadhifa kama kweli mwaijua democrasia si wapo wengi wataongoza muone nao kama wata weza si uchu wa madaraka mlio haidiana kinafki na fitina nyingi.

RA must goooooooooo!!!!!!!
EL must gooooooooooo!!!!!!

Wanamtandao must gooooooooooooo toooooo!!!!!!!!!
 
sijui ni lini na ilikuaje Mh. Zito ukaanza kuhusishwa na hizi Blah

Off point...mkuu nguvumali tafadhari badili font size and color unatuumiza macho na hata michango yako adhimu tunashindwa kuisoma..haya tuendelee
 
Yaani tutumie mamillioni ya kodi kwa ajili ya kutafuta Rostam ajiuzuru! mbona hiki ni kichekesho. dah! Rostam ...
unashangaa kwa kuwa haya huwa yanafanyika kwa siri kimsingi wangeweza kuundia kamati vile tu wamepishana kimaslahi
 
Ondokeni humo. Hakuna mtakalofanikisha. Na kwa chaguzi za mitaa zilizopita zilivyoonyesha huenda mwakani mkawa wachache zaidi.


Hapana. Chaguzi za mitaa mwaka 1999 na mwaka 2004 zilikuwa mbaya zaidi na tukapata viti hivyo tulivyopata Bungeni.

Kumbuka mwaka 2004 CUF walipata mitaa takribani yote Mbagala lakini hawakupata kiti hata kimoja cha udiwani. Kigoma CHADEMA ilikuwa na vijiji 2 tu mwaka 2004 lakini nilishinda ubunge na madiwani 4 katika ya 10.

Uchaguzi Mkuu utaamuliwa na ajenda za mwaka kesho na aina ya wagombea ubunge tutakaoweka. Ninaamini tutapa si chini ya 25% ya kura za wabunge nchi nzima na si chini ya wabunge 50. CUF wakipata vizuri zaidi Unguja maana Pemba yao na wakipata Mkuranga, Kilwa, Rufiji zote mbili, Temeke/Kigamboni, Pangani, Mtwara mjini na Tanga mjini tutafika theluthi ya wabunge na hapo ndio ntolee kwa CCM........... mark my words
 
Back
Top Bottom