Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hawawezi kuubadili UONGOZI wa BUNGE angalau kwa sasa. Uzuri ni mmoja kwenye uongozi wa mhimili huu; SPIKA anachaguliwa, hateuliwi mbali na uteuzi ule wa awali wa chama chake ambao kwa sasa hauwezekani pia kufanyika.
Acheni CCM wanyukane kwanza. Wanayemharibia kwa sasa ni JK. Anaonekana Uraisi hauwezi na Uenyekiti wa chama chake pia umemshinda.
mkuu tusaidie nani huyo mlishaji ?ccm bado ina viongozi wachache ambao ni wasafi crystal clear, na pia miongoni wa wapiganaji, wako baadhi ni wapiganaji wa kweli, wengine ni wapiganaji kutimiza malengo yao ya agenda zao, na wengine ni njaa zao tuu kazi yao kulishwa maneno na mfadhili wao mkuu na kuja kuyatapika bungeni.
Pale Dodoma wabunge wamemwambia mzee Ruksa na kamati yake kuwa amwambie muungwana kuwa ugomvi wote na mpasuko utaisha mara moja wakiondoka kwenye uongozi/ccm lile gruop of 4, RA, El, VjiCent na Mzee wa Tics. Na wameonyesha ni wakali kweli kwenye hilo, I hope hawatarudi nyuma, maana wakishindwa kwenye hilo, wamejimaliza.
Yaani tutumie mamillioni ya kodi kwa ajili ya kutafuta Rostam ajiuzuru! mbona hiki ni kichekesho. dah! Rostam ...
Mkandara,
Wakati wa Uchaguzi wa 2005, pesa chafu ya EPA ndio iliyoirudisha CCM Madarakani, ingawa wala hawakuhitaji kuchota.
Uchaguzi wa 2000, pesa za Meremeta na upuuzi mwingine zilitumika vizuri sana maana kulikuwa na kutokuaminiana ndani ya Chama na ngao ya CCM Mwalimu Nyerere alikuwa katutoka
Uchaguzi wa 1995, pamoja na pesa zote zilizokwisha chukuliwa kisanii na CCM, ilibidi wamkimbilie Nyerere ambaye single handedly aliwaangusha Mrema na wenzake wa Muungano na kutumia fimbo ya matakoni kumrudisha Salmin.
CCM ni chama si cha kuaminiwa na wewe unalijua hilo. KInachotokea sasa hivi ni ugomvi wa nani ashike hatamu na kula utamu kwa kutumia CCM na wala si kuhusiana na maslahi ya Taifa.
Waziri wa Usalama wa Taifa anapota kauli kuwa kila mtu ni safi kuhusu RICHMOND na RADA, je unafikiri ni nani aliyetoa baraka kwa kauli kama hiyo kutolewa?
Lowassa, Rostam, Sitta, Mwakyembe na wengineo wana madhambi yao, na tatizo limekuja sasa hivi ni mapiku!
Kama kina Sitta na Wapiganaji wangesikiliza lile tulilowaambia la kutetea maslahi ya Taifa na kufanya kazi kwa manufaa ya Taifa, fedheha kama hii isingetokea na kina Lowassa, Rostam na Sophia wasingediriki kufanya wanalolifanya leo hii!
Kwa miaka mitatu tumekaa tukizungumzia tuhuma kuhusu Rostam na Lowassa, je wameshakalishwa kitako ndani ya Chama au Serikalini na wakachukuliwa hatua?
Je Chenge naye ambaye ni mkuu wa Maadili ndani ya Chama ni lini amekalishwa kitako akaambiwa ajieleze?
Juzi suala la Richmond limegeuzwa kuwa ZeComedy, kina Sitta wanabanwa Golori zao kuttokana na kupenda posho, kina Ngwiliza wanafunuliwa kwa kupata pensheni mbili mbili, huku Richmond, Kagoda, EPA, Rada na sasa Kilimo Kwanza wanapeta na tunadanganywa kuwa ni kukua kwa Demokrasia ndani ya Chama!
Huu ni uhaini wa hali ya juu, na Watanzania tunachezewa akili, tunafujiwa hazina yetu na tunafanywa wapumbavu!
Nilihoji kwa nini Wapiganaji hawajiondoi na UCCM na kupigania mambo ya Taifa? Kwa nini wanaendelea kuogopa panga na rungu la Chama kwa kuendelea kuimba CCM mbele, Tanzania nyuma kam Wakristo wanavyoimba Msalaba Mbele Dunia nyuma?
Kwao Wapiganaji wa CCM, wokovu wao(binafsi) ni kupitia CCM na si kupitia Taifa la Tanzania!
Ni upuuzi kuendelea kuwasikiliza! Kwanza afadhali na tunajua kuwa Lowassa, Rostam na Chenge ni Mafisadi na hilo kila Mtanzania analijua na usishangae kuwa mwakani, viti vyote vya Ubunge Dar vitakwenda CCM na zaidi CCM inaweza kupunguza nusu ya viti vya Upinzani hasa Bara.
Lakini kwa kuwa ni jadi ya kuoneana aibu ndani ya Chama, kina Sitta wamepoteza nafasi moja kubwa sana, walipoleta ripoti ya Richmond wakadai kuna mambo mengine hawatayazungumza ili kuifichia aibu Serikali, hapo ndipo walipouza utu wao na wakapoteza sifa ya kuwa wapiganaji na hata maana ya kuwa na tume.
Kuondoka kwa Lowassa hakukutosha, ilipaswa ripoti ilete mabadiliko ya kweli si ya watu kujiuzulu tuu!
Kama wasingeficha baadhi ya mambo eti kuionea aibu Serikali, leo hii kila lililoovu lingeanza kuweweseka na kuogopa. Lakini midhali waliamua kufukia maovu na uzembe mwingine kwa kuonea huruma na aibu Chama na Serikali, basi ni vigumu sana kwa mabadiliko na vita dhhidi ya uhujumu, uzembe na kutofuata kanuni kufanikiwa.
Lakini swali langu na lile la Mwanakijiji linarudi, Wapiganaji wanapigania nini na wanampigania nani?
Ukiona Sophia na Rostam wanatamba kama walivyofanya sasa hivi, jiulize Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania yupo wapi na yupo upande gani?
Haya maneno gani lakini jamani.. Huyu RA na Wabunge wote Mafisadi hawafahamu kwamba Spika Sitta is third in line ktk uongozi wa nchi?..
Huyu jamaa ni kama chizi kweli, ameshatuibia vya kutosha kisha tena tuendelee kutumia fedha, kisa yeye ajiuzulu.
Muda wenu umewadia, kilichobaki ni kwenda mbele na hapa CCM ni lazima ichanike
WildCard,
Unaijua katiba ya Tanzania? akiwasilisha mtu mmoja ndani ya Bunge hoja ya kutokuwa na Imani na Spika na kukafanyika kikao ambacho Spika hutoka nje, mchezo umekwisha!
Mkandara,
La nyongeza, tulishangilia kanyaboya la Mramba na Yona kufikishwa mahakamani, nikaandika https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/21106-paukwa-pakawa.html watu wakafikiri natania!
Leo hii Kiwira imerudishwa kwa Serikali, walionunua kwa bei chee wamerudishiwa pesa zao, hakuna atakayepelekwa mahakamani.
Hizo za EPA, waliopelekwa mahakamani wote ni wale waliojichongea binafsi pembeni ya mchoro orijino wa Saidia CCM Ishinde! Wataungua, mtashangilia lakini KAGODA kamwe hataguswa, Jeetu Patel kapewa tenda mpya ya Bilioni 50, je unaamini kuwa ataendelea kuwa na kesi Kisutu?
The next step wataleta hoja ya ya kupiga kura ya kutokuwa na imani na Spika; Sitta ataondoshwa (kwani wabunge kadhaa watapangiwa visema kule nje na kura itapigwa). Akiondoshwa atawekwa Spika wao (jina tunalo) ambaye ataridhia maombi ya kina RA na Sofia. Ndipo tume wataiunda wao na kina RA na EL watasafishwa rasmi kwa kutumia utaratibu wa kibunge na hivyo maamuzi kuwa legally binding.
Tayari kwa karibu wiki kadhaa sasa pesa imetembea Dodoma kwa ajili ya jambo hili na kwa ajili ya kupata support ya wabunge. Novemba 7 ni siku muhimu kwa ajili ya hili.
Third in line maana yake nini?
Rev.WildCard,
Unaijua katiba ya Tanzania? akiwasilisha mtu mmoja ndani ya Bunge hoja ya kutokuwa na Imani na Spika na kukafanyika kikao ambacho Spika hutoka nje, mchezo umekwisha!
Mkandara,
La nyongeza, tulishangilia kanyaboya la Mramba na Yona kufikishwa mahakamani, nikaandika https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/21106-paukwa-pakawa.html watu wakafikiri natania!
Leo hii Kiwira imerudishwa kwa Serikali, walionunua kwa bei chee wamerudishiwa pesa zao, hakuna atakayepelekwa mahakamani.
Hizo za EPA, waliopelekwa mahakamani wote ni wale waliojichongea binafsi pembeni ya mchoro orijino wa Saidia CCM Ishinde! Wataungua, mtashangilia lakini KAGODA kamwe hataguswa, Jeetu Patel kapewa tenda mpya ya Bilioni 50, je unaamini kuwa ataendelea kuwa na kesi Kisutu?
Hawawezi kuubadili UONGOZI wa BUNGE angalau kwa sasa. Uzuri ni mmoja kwenye uongozi wa mhimili huu; SPIKA anachaguliwa, hateuliwi mbali na uteuzi ule wa awali wa chama chake ambao kwa sasa hauwezekani pia kufanyika.
Acheni CCM wanyukane kwanza. Wanayemharibia kwa sasa ni JK. Anaonekana Uraisi hauwezi na Uenyekiti wa chama chake pia umemshinda.
Rev.
Azimio la Bunge la kumwondoa Spika Madarakani linahitaji theluthi mbili ya Wabunge kuliunga mkono (84.7.d). Kwa mazingira ya sasa hiyo ni ngumu sana. CCM pia wanaelewa madhara yake na ndio maana ile njia rahisi zaidi na ya mkato kupitia NEC yao ilishindikana.

Umekasirika?
Juzi uwanja wa ndege ya JK Nyerere nilikutana na kale ka Rais ka Madagascar Bw. Rajoelina
Spika hayumo kabisa kabisa line up ya Dola. Mwaka 2005 Katiba ilibadilishwa na line up kuwa Rais, Makamu na PM.
Sawa. Mchakato wa Azimio utawalazimu Wabunge wengi tu wawepo Bungeni.wabunge walioko Bungeni.. siyo wabunge wote!