Maazimio ya Kikao
Mahudhurio
1 Baba wa Familia
2 Mama wa Familia
3 Mtoto wa Kwanza
4 Mtoto wa Pili
5 Dada wa Kazi
6 Kijana wa Usafi
7 Mwakilishi Kampuni ya ulinzi.
- Kikao kiliridhiria kwamba Baba Awe Mwenyekiti
- Mama alichaguliwa Kwa Kauli Moja kuwa Katibu
Kikao kilifunguliwa saa 3.00 Usiku kwa sala ya kuombea familia, na taifa Kwa Ujumla
Baada ya Wajumbe kupitia hadidu za Rejea, na agenda za Kikao, waliridhia kwamba kikao kiendelee, na agenda zilizopendekezwa zijadiliwe.
Wajumbe wote waliridhia kwamba
1 Hawataki Kufa na Corona
2 Hawataki kupata Corona
3 Hawapendi kuona ndugu na jamaa wamepata Corona
4 Wanaipenda nchi Yao Tanzania na wanaitakia Kila la kheri katika mapambano na Corona.
Maazimio ya Utekelezaji ni kama yafuatavyo:
1. Tupo kwenye lockdown na Hatua zifuatazo zinachukuliwa.
2 Geti kufungwa Kwa Kofuli Muda wote
3 wageni hawaruhusiwi kuingia ndani na wakazi hawaruhusiwi kutoka nje.
4. Wanaoruhusiwa kutoka ni wale wenye shughuli maalum hususani za kipato Kwa familia.
5. Dada ajipange safari za gengeni na dukani, ikiwezekana mara moja Kwa wiki. Ikibidi isizidi mara moja Kwa siku.
5. Kwa namna inavyowezekana Baba anunue vitu in bulk na kuhakikisha mazagazaga yapo Kwa Fridge.
6. Ni kipindi kigumu cha maisha na hivyo ni lazima kufunga mikanda. Vitu vya Anasa kama burger, Pizza, weaving, nguo Mpya, perfum za gharama, manunuzi yake lazima yapitishwe kwenye mkutano huu.
7. Kingamuzi cha DSTV kuendelea kutumika, hata hivyo kifurushi kitashushwa mpaka compact
8. Mipango ya maendeleo kama Ujenzi, ununuzi wa Viwanja, uwekezaji Kwa makampuni, manunuzi ya Magari na mengine kama haya yamesitishwa Kwa Muda mpaka Hali ya Covid 19 itakapotengamaa
9 Usafi ni Muhimu, hata hivyo matumizi ya maji yawe Kwa uangalifu Mkubwa.
10. Wakati wote anayetoka nje ya Nyumba akirudi nyumbani ni lazima anawe Kwa maji yanayotiriika. Kwa namna invyowezekana aende Bafuni moja Kwa moja, na nguo chafu zibaki Kwa kapu la nguo chafu.
12 kuosha mikono mara Kwa mara Kwa kutumia maji yanayotiriika na sabuni unapokuwa nyumbani
13 kuvaa barakoa mara unapokuwa nje ya nyumbani
14 viatu kuvuliwa nje ya Geti na kufanyiwa usafi stahiki kabla ya kuingizwa ndani
15. Huduma za salon Kwa kina mama Zimesitishwa, na imeshauriwa wapunguze nywele ili waweze kuosha vichwa vyao Kila siku
16 Huduma za salon Kwa wakina Baba zitapatikana Kila jumamosi Kwa kinyozi kuja nyumbani, kabla kinyozi hajaingia nyumbani lazima afanyiwe sanitisation na kwamba nguo atakazovaa zitatoka ndani ya Nyumba. Baba atanunua mavazi Rasmi Kwa Kinyozi. Mashine itakayotumika ni za nyumbani na hakuna upuuzi wa scrub wala facial. Kinyozi atavaa Gloves na Barakoa
17 Mara Mlinzi afikapo eneo la Lindo afanyiwe sanitisation na kubadili nguo. Mlinzi atavaa Gloves na Barakoa
18. Wageni ni marufuku, isipokuwa Kwa Babu na Bibi Tu, hata na wao wanapofika lazima wapitie zoezi la sanitisation. Na wakifika hawataondoka mpaka baada ya siku 14.
19. Homework zitafanyika Kwa wakati kama zitavyokuwa zinaelekezwa na Mama
20 Ili kupunguza makali ya lockdown, Muda wa TV na Game umeongezwa Kwa masaa mawili Kila siku.
Hitimisho
Kikao kiliridhia kama Sheria hazitafuatwa sheria Kali zaidi zitawekwa
Kikao kilifungwa saa 3.45 usiku
Sent using
Jamii Forums mobile app