Kikao cha Halmashauri kuu ya NCCR-Mageuzi

Kikao cha Halmashauri kuu ya NCCR-Mageuzi

Charuka

Member
Joined
Oct 20, 2009
Posts
56
Reaction score
18
Halmashauri kuu ya chama cha NCCR-Mageuzi imemaliza kikao chake cha siku mbili jijini Dar, leo jioni.
Katika kikao hicho, wanachama wapya waliohamia kutoka chama kingine walihudhuria kama waalikwa, na habari za uhakika ni kwamba kikao hicho kimeidhinisha kazi maalum walizopewa na Katibu Mkuu (Sam Ruhuza) ambaye katiba inampa mamlaka ya kuteua mtu kwa ajili ya nafasi fulani, kisha uteuzi huo kudhibitishwa na halmashauri.
Habari zaidi, soon
 
Danda amepangiwa kazi katika idara ya Organazesheni, kampeni na uchaguzi, makao makuu ya chama.
Kafulila atakuwa katika idara ya habari na uenezi, pale pale makao makuu
 
Danda amepangiwa kazi katika idara ya Organazesheni, kampeni na uchaguzi, makao makuu ya chama.
Kafulila atakuwa katika idara ya habari na uenezi, pale pale makao makuu

He he heeeeeeeeeeee!
 
Danda amepangiwa kazi katika idara ya Organazesheni, kampeni na uchaguzi, makao makuu ya chama.
Kafulila atakuwa katika idara ya habari na uenezi, pale pale makao makuu

mbona ghafla hivo?
hizo nafasi zilikuwa tupu zikiwasubiri washkaji watoke huko na uzoefu wa kufanya hizo shughuli nini?
anyway hawa nccr watoke kwenye siasa za pale habari maelezo waende kwa wananchi sasa,ni siku mingi sijasikia mkutano wa hadhara wa nccr mageuzi
 
hivi ni vituko vingone katika siasa za tanzania! na msumari wa mwisho kwenye kaburi la nccr,
tusubiri.........
 
hivi ni vituko vingone katika siasa za tanzania! na msumari wa mwisho kwenye kaburi la nccr,
tusubiri.........

hakuna vituko hapo, hizo ndio siasa za tanzania.

Tambwe hiza alikuwa wapi? na sasa yuko wapi? Salum Msabaha je? Daniel Nsanzugwanko? Abas mtemvu? Lamwai? na list inaendeleaaaaa......

hakuna cha ajbu hapo, nccr kama wamewaona wanafaa kukitumikia chama chao wacha wapewe hayo majukumu.

mbona mrema alipotua tu nccr alipewa uchea, kwani hiyo nafasi ilikuwa haina mtu? au alipokwenda TLP hakukuwa na mwenyekiti hadi apewe yeye.
suala la uamuzi wa nani afanye kazi gani waachie wenyewe, na wala mi sitarjii kwamba nccr itaingia kaburini hivi kaburini. Itaendelea kuwepo ingawa si katika makali yale ya zamani.
 
mbona ghafla hivo?
hizo nafasi zilikuwa tupu zikiwasubiri washkaji watoke huko na uzoefu wa kufanya hizo shughuli nini?
anyway hawa nccr watoke kwenye siasa za pale habari maelezo waende kwa wananchi sasa,ni siku mingi sijasikia mkutano wa hadhara wa nccr mageuzi
hujaambiwa wamepewa vacant posts, wamepangiwa idara za kufanyia kazi, hizo idara zina wakuu wake.
 
hivi ni vituko vingone katika siasa za tanzania! na msumari wa mwisho kwenye kaburi la nccr,
tusubiri.........
Dua zenu za mauti juu ya NCCR hazitakaa zisikilizwe. Vitakufa vya kwenu, NCCR itaishi huku viroho vya chuki vikiwakereketa daima!
 
Vyeo vizuri bana. hata kama umepata cheo kwenye chama kinacho jifia kwao ni bora kuliko kubaki mwanachama wa kawaida kwenye chama mbadala.
 
walevi wa madaraka, wamepewa mvinyo wa madaraka, mda si mrefu wataanza kupepesuka
 
Danda amepangiwa kazi katika idara ya Organazesheni, kampeni na uchaguzi, makao makuu ya chama.
Kafulila atakuwa katika idara ya habari na uenezi, pale pale makao makuu

Msishangae baada ya wiki tu wataanza kuhoji matumizi ya Chama.
 
Source: Habarileo 9th December, 2009
Katika mkutano huo, Halmashauri hiyo ilipitisha majina ya watu walioteuliwa kuongoza Idara mbalimbali za Sekretarieti ya chama hicho ambapo aliyekuwa Ofisa Habari wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), David Kafulila, ameteuliwa kuwa Mkuu wa Idara ya Habari na Uenezi wa chama hicho.

Kafulila na mwenzake Danda Juju ambaye ameteuliwa kuwa Msaidizi wa Mkuu wa Idara ya Oganaizesheni, Kampeni na Uchaguzi, walivuliwa vyeo vyao Chadema kwa kile kilichodaiwa kuwa ni watovu wa nidhamu.

Ruhuza alisema NCCR katika mkutano wake huo wa kawaida wa Halmashauri Kuu, walijadili mambo matatu ambayo ni Hali ya kisiasa nchini, Demokrasia ndani ya vyama, na mwelekeo wa NCCR kuelekea Uchaguzi Mkuu

Katika hatua nyingine, Ruhuza alisema
chama hicho kimeazimia kufungua kesi Mahakama Kuu kabla ya Desemba 15 mwaka huu dhidi ya serikali kudai Tume huru ya Uchaguzi kwa kile walichodai kuwa iliyopo si huru na uchaguzi mwakani hautakuwa huru.

“Halmashauri Kuu ilipitisha uamuzi wa kuishitaki serikali maana tuliipa muda wa siku 90 kuanzia Agosti 12 mwaka huu na zimeisha hakuna kilichofanyika, hili ni suala la watanzania wote ndiyo maana tumeamua hivyo,” alsiema Ruhuza.

Aidha,
NCCR-Mageuzi itazindua mpango wa kuchangisha fedha kwa ajili ya uchaguzi mwakani mkoani Kigoma Desemba 16, mwaka huu wakati ziara ya Mwenyekiti wa Taifa, James Mbatia na uchangiaji utaanza Januari.

Viongozi wengine waliopitishwa na Halmashauri Kuu ya chama hicho na idara zao katika mabano ni George Kahangwa (Itikadi, Sera na Mafunzo), Dk. Sengodo Mvungi (Katiba, Sheria na Haki za Binadamu), (Fedha, Uchumi na Mipango) Mariam Mwakingwe na Msaidizi wake ni Beati Mpitabakana.

Wengine ni Sebastian Thomas (Ulinzi na Usalama), Nderakindo Kessy (Mambo ya Nje), (Oganaizesheni, Kampeni na Uchaguzi), Faustin Sungura akisaidiwa na Juju, (Vijana) Raphael Tweve, (Wanawake) Amina Suleiman na (Wazee ) Ernest Mwasada.
 
Msishangae baada ya wiki tu wataanza kuhoji matumizi ya Chama.

Siyo muda mrefu Joseph Selasini ametimkia ChADEMA akisema NCCR akuna huongozi wala malengo leo akina Kafulila nao wanaenda huko kuwa CHADEMA hakufai, Lo siasa za Bongo hizi!!!
 
Danda amepangiwa kazi katika idara ya Organazesheni, kampeni na uchaguzi, makao makuu ya chama.
Kafulila atakuwa katika idara ya habari na uenezi, pale pale makao makuu

NA wliokuwa na hizo nafasi wamepelekwa wapi? Au sio 'wasomi' kama hao akina Danda? Siasa wa wa-Tz mh!!
 
Hivi ni chama gani kinatufaa? CCM balaa, NCCR wanapokea vibudu, CHADEMA wanatimuana, CUF wameamua kushikamana na CCM ili kuangusha upinzani, YESU RUDU HARAKA.
 
Hivi ni chama gani kinatufaa? CCM balaa, NCCR wanapokea vibudu, CHADEMA wanatimuana, CUF wameamua kushikamana na CCM ili kuangusha upinzani, YESU RUDU HARAKA.

Kama Yesu angerudi leo kabla ya watu kutubu dhambi zao za kuwaita wanadamu wenzao vibudu, unafikiri ingekuwaje Bwana Kaitaba?
 
Source: Habarileo 9th December, 2009

Viongozi wengine waliopitishwa na Halmashauri Kuu ya chama hicho na idara zao katika mabano ni George Kahangwa (Itikadi, Sera na Mafunzo), Dk. Sengodo Mvungi (Katiba, Sheria na Haki za Binadamu), (Fedha, Uchumi na Mipango) Mariam Mwakingwe na Msaidizi wake ni Beati Mpitabakana.

Mkuu Kahangwa si niliskia umejivua uanachama wa NCCR vipi tena..? Huyu ni Kahangwa wewe au mwingine??
 
Back
Top Bottom