Source: Habarileo 9th December, 2009
Katika mkutano huo, Halmashauri hiyo ilipitisha majina ya watu walioteuliwa kuongoza Idara mbalimbali za Sekretarieti ya chama hicho ambapo aliyekuwa Ofisa Habari wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), David Kafulila, ameteuliwa kuwa Mkuu wa Idara ya Habari na Uenezi wa chama hicho.
Kafulila na mwenzake Danda Juju ambaye ameteuliwa kuwa Msaidizi wa Mkuu wa Idara ya Oganaizesheni, Kampeni na Uchaguzi, walivuliwa vyeo vyao Chadema kwa kile kilichodaiwa kuwa ni watovu wa nidhamu.
Ruhuza alisema NCCR katika mkutano wake huo wa kawaida wa Halmashauri Kuu, walijadili mambo matatu ambayo ni Hali ya kisiasa nchini, Demokrasia ndani ya vyama, na mwelekeo wa NCCR kuelekea Uchaguzi Mkuu
Katika hatua nyingine, Ruhuza alisema chama hicho kimeazimia kufungua kesi Mahakama Kuu kabla ya Desemba 15 mwaka huu dhidi ya serikali kudai Tume huru ya Uchaguzi kwa kile walichodai kuwa iliyopo si huru na uchaguzi mwakani hautakuwa huru.
Halmashauri Kuu ilipitisha uamuzi wa kuishitaki serikali maana tuliipa muda wa siku 90 kuanzia Agosti 12 mwaka huu na zimeisha hakuna kilichofanyika, hili ni suala la watanzania wote ndiyo maana tumeamua hivyo, alsiema Ruhuza.
Aidha, NCCR-Mageuzi itazindua mpango wa kuchangisha fedha kwa ajili ya uchaguzi mwakani mkoani Kigoma Desemba 16, mwaka huu wakati ziara ya Mwenyekiti wa Taifa, James Mbatia na uchangiaji utaanza Januari.
Viongozi wengine waliopitishwa na Halmashauri Kuu ya chama hicho na idara zao katika mabano ni George Kahangwa (Itikadi, Sera na Mafunzo), Dk. Sengodo Mvungi (Katiba, Sheria na Haki za Binadamu), (Fedha, Uchumi na Mipango) Mariam Mwakingwe na Msaidizi wake ni Beati Mpitabakana.
Wengine ni Sebastian Thomas (Ulinzi na Usalama), Nderakindo Kessy (Mambo ya Nje), (Oganaizesheni, Kampeni na Uchaguzi), Faustin Sungura akisaidiwa na Juju, (Vijana) Raphael Tweve, (Wanawake) Amina Suleiman na (Wazee ) Ernest Mwasada.