Hizo taarifa za Job kujiuzulu nafasi zote za uongozi ndani ya chama, huo utakuwa ni uongo!. Kama ni kujiuzulu ni kujiuzulu uspika tuu ambao ujumbe wa CC, anakuwa ameupoteza automatically, lakini anaendelea na ubunge wake, unless kama CCM watamuweka kikao. CCM hawafanyi mambo kienyeji kama wale wenzetu.
P
Rejea Comment yako ya awali kisha rudi tupatie mrejesho baada ya Ndugai kuachia ngazi:
Hili suala la wabunge 19 wa Chadema, watu mnahamanika bure tuu. Tanzania tunafuata mfumo wa sheria wa Uingereza, common laws, ambao unafuata kanuni za natural justice. Kanuni ya kwanza inasema, everbody is presumed inocent until proven guilt, 2. no one is condemned unheard 3. The burden of proof, lies with the prosecution, the one who alleges, must prove.
Kwanini kina Halima wamehukumiwa bila kusikilizwa?. Kwa vile Spika kapelekewa majina na NEC, Chadema ndio the ones who alleges kuwa hao wabunge wame foji, and must prove, kuwa hawakuwateua, wala hawakuandika barua. Laiti mgejua Spika ana nini mkononi inayompa kiburi hivyo, CC ya Chadema isinge watimua, kwa pupa na kwa papara bila kwanza kujiridhisha majina hayo, yamefikishwa kwa Tume ya Uchaguzi kwa barua gani, iliyosainiwa na nani. Hapo ndipo kwenye mzizi wa fitna. Spika yeye kapelekewa majina tuu. Na sasa kikao cha BUK la Chadema, kitapindua maamuzi ya CC ya Chadema, mchezo utakuwa umekwisha.
Najua wengi humu, watatoa hoja kuwa wabunge hao waliitwa kupewa haki ya kusikilizwa, lakini sii wengi humu, wameisoma katiba ya Chadema na taratibu za kufuta wanachama, kwa faida ya wengi utaratibu ni huu.
1. Kwa mujibu wa katiba ya CHADEMA, ili kumvua mtu uanachama kuna mlolongo wa kanuni na taratibu za kufuatwa na miongoni mwake ni hizi nitakazo ziorodhesha hapa chini, jee zilifuatwa?.
2. Kuandaa Hati ya Mashtaka kwa maandishi yenye tuhuma zote ambazo mtuhumiwa anakabiliwa nazo. Jee hati hizi za mashitaka kimaandishi ziliandaliwa?. Kina Halima walipewa hati za mashitaka?.
3. Hati hiyo ya mashitaki kimaandishi inatakiwa ikabidhiwa kwa mtuhumiwa kwa "despatch" ili kuthibitisha imemfikia, jee hili lilifanyika?, nimesikia kuna watu waliitwa kwa simu, jee huu ndio utaratibu kwa jambo zito kama hili?.
4. Mtuhumiwa atatakiwa kuzijibu tuhuma za mashitaka hayo kimaandishi ndani ya kipindi cha siku 14 tangu tarehe aliyopokea barua ile ili apate muda wa kutosha kutafakari, jee hili lilifanyika?. Mashitaka yanatolewa kwa maandishi na kujibiwa kwa maandishi, ndipo process ya kuitana na kusikilizwa shauri inafuata.
5. Baada ya majibu ya hati ile ya mashitaka kurejeshwa, ndipo mamlaka ya nidhamu ingepaswa kuitisha kikao rasmi kwa mujibu wa katiba ya Chadema na kuwaalika watuhumiwa kwa barua ili kuwapa nafasi ya haki ya kusikilizwa, kwa kujieleza na kujitetea. Kumsikiliza mtuhumiwa kabla ya kufikia maamuzi ya kumhukumu ni moja ya haki muhimu kabisa!. Jee kwenye huo uamuzi huo wa kuwatimua, kwa nini watimuliwe uanachama bila kusikilizaa. Jee sheria, taratibu na kanuni zilifuatwa?!.
6. Kwa wabunge wale 18 ni CC ya chadema ndio mamlaka yao ya nidhamu, lakini kwa, Mwenyekiti wa Bawacha, Halima Mdee, CC ya Chadema sio mamlaka yake ya nidhamu, mamlaka yake ya nidhamu ni Baraza Kuu, sasa CC ya Chadema, imepata wapi iwezo wa kumsimamisha uanachama Mdee?.
Nawaomba sana Chadema, msishabikie maamuzi ya CC ya Chadema kukaa kama a kangaroo court na kutoa maamuzi ya kuwatimua uanachama wanachama wake shupavu, walio ipigania Chadema kwa machozi, jasho na damu, mkumbuke kuna karma.
Tukisubirie Kikao cha Baraza Kuu, kama kita endorse uamuzi huu wa a kangaroo court ya CC, kitakachofuata ni nyote kushuhudia, jinsi karma, itakavyo washughulikia watu.
Kwa msio jua karma, na inafanya nini kwa Chadema, someni hapa, angalieni chanzo kilichosababisha haya yatokee, nini kilikuja kuwakuta hao visababishi?.