Kikao cha MaRais wote, kujimwambafai, Mpango sio matumizi na uungwana wa Kinana!

Tila-lila2

JF-Expert Member
Joined
Oct 20, 2019
Posts
652
Reaction score
1,058
Juzi juzi wote tuliona Marais wote (yaani na wale wataafu) wakiwa Dodoma, wakapewa ndege tausi na wakashuhudia uzinduzi wa Jumba Jeupe la Dodoma.

Katika kikao hicho uwezekano mkubwa kuna mambo muhimu sana yalijadiliwa. La kwanza kabisa hata kabla ya kujua yale ya undani zaidi tuliona jinsi MaRais wale walivyojaribu kuiptanisha Serikali ya Awamu hii ya ile ya JK. Serikali hii imekuwa ikijimwambafai sana kwamba yenyewe tangu kipindi cha Nyerere ndiyo imewezesha Dodoma sasa kuhamiwa lakni hizi zingine yaani ya Mwinyi, Mkapa na JK (tena hasa ya MkwereJK) hawakufanya kitu chochote. Awamu hii imekuwa ikijimwambafai sana. Ajabu sana!

Aliyenifurahisha ni Mzee Mkapa alielezea vizuri kuhusu nini kilifanywa kabla ya awamu hii na hasa kipindi cha JK na tena akaongeza na maneno ya kumshukuru JK kuwa alifanya kazi nzuri. JK mwenyewe akaelezea vizuri kuhusu ujenzi wa UDOM na kubadili mpango wa wapi pa kujenga Ikulu na Mji wa Serikali. Mhhh hadi nikashtuka kumbe mwazo Ikulu ilikuwa iwe kule kule UDOM - nikaona kumbe walifanya kazi. Ila sasa JK akaniacha hoi zaidi kuwa hata yale waliyofanya wao makubwa tu, ujenzi wa bunge bora, UDOM n.k haikuwa kitu bali ilikuwa ni mpango tu na akamalizia kwa kusema "Mpango sio Matumizi". Kwa hiyo JK alijishusha wakati Mkapa alikuwa kampaisha juu.

Hayo yote yalifanyika kwa makusudi ili kumfahamisha Mkulu aliyeshika usukani kwa sasa kuwa aache kujimwambafai sana na kuwakosoa waliotangulia (hasa awamu ya JK) kuwa hawakufanya kitu. Alikumbushwa kuwa kila awamu imetekeleza wajibu wake na kumkumbusha kuwa anayotekeleza ilikuwa ni mpango tayari na ulishawekwa katika hatua nzuri ya uetelekezaji. Hivyo basi anazidi kukumbushwa aache kubeza juhudi za wenzake na kujimwambafai kuwa kila kitu kafanya yeye. Nafikiri kwa hekima zao ilibidi "wamute" wasibwatuke kuhusu mipango lukuki inayotekelezwa Chato kwa kasi utafikiri inaenda kuwa makao makuu ya tatu ya Nchi.

Kwa kumalizia yamkini kwa kikao kile cha MaRais Dodoma ndicho kilichojadili dalili za CCM kugawanyika vipande vipande na kushauri maridhiano ambayo inawekena yamesababisha Kinana akaona awe muungwana aombe radhi kiaina hata kama yeye hajawahi kuombwa radhi - kwa sababu inajulikana pia hata yeye alikosewa sana. Sometimes naamini kama mimi siku zote ni wa kuombwa msamaha tu halafu siombi msamaha basi inawezekana nikawa sipo mkamilifu sana. Kitendo cha kiungwana cha Kinana nina uhakika ni kweli kimetokana na Kikao hicho.

Zaidi ya yote, Membe kwa matumaini aliyonayo katika uongozi wa nchi hii ni kweli haimlazimu kuomba msamaha wowote. Na kaweka bayana hajamkosea mtu bali yeye ndiye kakosewa kwa sababu maongezi yake yalidukuliwa na pia hata kesi ya yeye kukashfiwa na Musiba bado ipo Mahakamani. Kuomba msamaha ina maana hata ile kesi inabidi akaifute!

Karibuni Idukilo kwetu tunywe kahawa pale kijiweni!
 
Kumbe huwa mnaangalia TBC na kusikiliza hotuba za viongozi mnaowaponda sana ?
 
Mkuu unachokisema kinafikirisha hasa ukizingatia malalamiko ya Musiba juu ya kile alichofanyiwa na vijana wa Sirro kule Lindi huenda ni sehemu ya kumridhisha Kinana.
 
Lakini leo tena Musiba inasemekana anaongea kabla ya TAL - inaonesha bado anatumika!
 
Huyu anajimwambafy lakini ataliacha Taifa na madeni makubwa sana. Hebu asssume kma kila anapoomba kukopa anapewa tu pesa, deni la Taifa si lingekuwa maradufu?
 
Bora aliyekuwa anaenda nje akirudi anapewa za bure, sio kukopa!
 
Juzi juzi wote tuliona Marais wote (yaani na wale wataafu) wakiwa Dodoma, wakapewa ndege tausi na wakashuhudia uzinduzi wa Jumba Jeupe la Dodoma.

Katika kikao hicho uwezekano mkubwa kuna mambo muhimu sana yalijadiliwa. La kwanza kabisa hata kabla ya kujua yale ya undani zaidi tuliona jinsi MaRais wale walivyojaribu kuiptanisha Serikali ya Awamu hii ya ile ya JK. Serikali hii imekuwa ikijimwambafai sana kwamba yenyewe tangu kipindi cha Nyerere ndiyo imewezesha Dodoma sasa kuhamiwa lakni hizi zingine yaani ya Mwinyi, Mkapa na JK (tena hasa ya MkwereJK) hawakufanya kitu chochote. Awamu hii imekuwa ikijimwambafai sana. Ajabu sana!

Aliyenifurahisha ni Mzee Mkapa alielezea vizuri kuhusu nini kilifanywa kabla ya awamu hii na hasa kipindi cha JK na tena akaongeza na maneno ya kumshukuru JK kuwa alifanya kazi nzuri. JK mwenyewe akaelezea vizuri kuhusu ujenzi wa UDOM na kubadili mpango wa wapi pa kujenga Ikulu na Mji wa Serikali. Mhhh hadi nikashtuka kumbe mwazo Ikulu ilikuwa iwe kule kule UDOM - nikaona kumbe walifanya kazi. Ila sasa JK akaniacha hoi zaidi kuwa hata yale waliyofanya wao makubwa tu, ujenzi wa bunge bora, UDOM n.k haikuwa kitu bali ilikuwa ni mpango tu na akamalizia kwa kusema "Mpango sio Matumizi". Kwa hiyo JK alijishusha wakati Mkapa alikuwa kampaisha juu.

Hayo yote yalifanyika kwa makusudi ili kumfahamisha Mkulu aliyeshika usukani kwa sasa kuwa aache kujimwambafai sana na kuwakosoa waliotangulia (hasa awamu ya JK) kuwa hawakufanya kitu. Alikumbushwa kuwa kila awamu imetekeleza wajibu wake na kumkumbusha kuwa anayotekeleza ilikuwa ni mpango tayari na ulishawekwa katika hatua nzuri ya uetelekezaji. Hivyo basi anazidi kukumbushwa aache kubeza juhudi za wenzake na kujimwambafai kuwa kila kitu kafanya yeye. Nafikiri kwa hekima zao ilibidi "wamute" wasibwatuke kuhusu mipango lukuki inayotekelezwa Chato kwa kasi utafikiri inaenda kuwa makao makuu ya tatu ya Nchi.

Kwa kumalizia yamkini kwa kikao kile cha MaRais Dodoma ndicho kilichojadili dalili za CCM kugawanyika vipande vipande na kushauri maridhiano ambayo inawekena yamesababisha Kinana akaona awe muungwana aombe radhi kiaina hata kama yeye hajawahi kuombwa radhi - kwa sababu inajulikana pia hata yeye alikosewa sana. Sometimes naamini kama mimi siku zote ni wa kuombwa msamaha tu halafu siombi msamaha basi inawezekana nikawa sipo mkamilifu sana. Kitendo cha kiungwana cha Kinana nina uhakika ni kweli kimetokana na Kikao hicho.

Zaidi ya yote, Membe kwa matumaini aliyonayo katika uongozi wa nchi hii ni kweli haimlazimu kuomba msamaha wowote. Na kaweka bayana hajamkosea mtu bali yeye ndiye kakosewa kwa sababu maongezi yake yalidukuliwa na pia hata kesi ya yeye kukashfiwa na Musiba bado ipo Mahakamani. Kuomba msamaha ina maana hata ile kesi inabidi akaifute!

Karibuni Idukilo kwetu tunywe kahawa pale kijiweni!
Tumekosea sana watanzania awamu hii.
 
Back
Top Bottom