Kikao cha NEC Zanzibar: Karume hataki kuongezewa muda!

Kikao cha NEC Zanzibar: Karume hataki kuongezewa muda!

Kuna siri ambayo imejificha nyuma ya sakata hli za Zenj. Baada ya matokeo ya daftari la wapiga kura kuhakikiwa ktk visiwa hivyo, takwimu zinaonyesha kuwa kiongozi wa chama kikuu cha upinzania atashindwa ktk kura za Urais na hivyo kufanya yale yote aliyokuwa anayalalamikia siku za nyuma ni uongo. Kwa kufanya hivyo, atakuwa anakiua chama chake kisiasa ktk visiwa hivyo.
Njia pekee aliyoiona ya kumnusuru yeye na chama chake ni kumuongezea kiongozi wa sasa muda wa miaka miwili a mitatu ili wao waweze kuzirudisha kura ktk kipindi hicho. Na hapa mgombea atakayesimamishwa sio Hamad Rashid, bali nia Juma Duni.

Too illogical to make any sensible sense!!
 
lakini kama kweli watu wa Zanzibar walishaambiwa kuwa leo Jpili kuna mkutano wao wa CCM na wakagoma kuja, basi hapo pana picha mbaya sana kwa CCM na hatima ya uongozi wa hii nchi,
 
lakini kama kweli watu wa Zanzibar walishaambiwa kuwa leo Jpili kuna mkutano wao wa CCM na wakagoma kuja, basi hapo pana picha mbaya sana kwa CCM na hatima ya uongozi wa hii nchi,

ukiona hivyo ujue Chama hakina uongozi na mwenyekiti hana sauti na hawezi kutoa amri zikaheshimiwa...hivi wakati wa Nyerere kama mwenyekiti wa chama angeweza kuitisha kikao na wajumbe wa zanzibar wakagoma kuja???hahaaaa mtoto wa kikwere jumba bovu linakuangukia hivi hiviiiii
 
That is your take, jaribu kujiuliza kiutu uzima wiki iliyopita kulitakiwa kufanyike kikao cha NEC Dodoma wajumbe wa Zanzibar wakagoma kuja kuwa wana kikao cha wawakilishi si kawaida yao kwanza si wawakilishi wote ambao ni wajumbe wa NEC.

Kikaitishwa kikao cha dharura cha CC-CCM Dar es salaam vile vile wajumbe wa zanzibar wakagoma bila kutoa sababu usiniulize kwa hili sijui kitu ambacho si cha kawaida kikao cha CC kimeahilishwa ghafula, kuona hivyo CCM bara wakamtuma Msekwa kuwafuata Zanzibar kujua kulikoni wewe bado unasema hakuna chochote.

Kwa mtazamo wa kawaida tu hii sinema si ya kawaida kwa CCM na wala tusidharau kwa kusema ni mambo ya kawaida, kama ni kujiridhisha kwa wana CCM ok endeleeni kujiridhisha lakini wenye akili zao wameliona hili na wanajua kuna jambo kubwa linatokea ndani ya CCM.

Mkuu kila mara tunapokaribia uchaguzi sarakasi kama hizi huwa zinachezwa, kali kabisa ni ile iliyochezwa na Salmin lakini at the end of the day alikuja kutoa chozi mwenyewe. My meaning is nothing substantial is going to happen,
 
mmmh kwa haya yote useme hakuna kitu substantial?aaah wapi kuna kitu kikubwa kinakuja....sio kawaida mbona haya hayakuwa yanatokea wakati wa Mkapa au Mwinyi au Nyerere??
 
Kaka this time is different kwasababu zifuatazo:-

a). mabadiliko ya katiba Salmin alikuwa anataka kufanya mabadiliko mwenyewe na sio wanaccm wote. This ni wanaccm wote from znz wanataka mabadiliko na kimsingi wameshaona Tanzania bara hakuna nia njema. Now this is crisis kwasababu unakuwa na watu ambao kweli wanasikiliza amri from NEC dodoma (ambao ni kiduchu) na wengi wao wengine ni wanafiki wanawakubalia ikifika znz wanabadilika yaani vinyonga. sasa hapa ni tatizo maana kama mwenyekiti haheshimiwi then ni tatizo kwani mwisho wa siku inaishia kuwa society of lawless kila mtu anajifanyia anavyoona yeye.

b). Ufisadi uliotokea na unaoendelea kutokea bara unawaumiza vigogo wa znz ambao wanaonekana hawafaidi kitu. Waziri unamkuta hana tofauti na mfanyakazi wa kawaida znz kitu ambacho viongozi znz. Kimsingi viongozi wa znz washaona kuwa jamaa wa bara wanawazidi kete hivyo wanaona kwakuwa karafuu haina soko na hawana source of ufisadi wanaona waekeze macho yao katika mafuta. wapate japo nao kula kitu.

c). Dharau imetokea kawaida watu tanganyika especially tanzania bara wanawaona watu kutoka znz kama hawajasoma wajinga na watu wapumbavu. Hii tabia imetengeneza chuki kwani vijana waliokuja kusoma vyuo vikuu dar na nje ndio walioshika madaraka sasa hivi znz hivyo basi wanataka kuwaonyesha wenzao wa dar kuwa wao hawajosomea elimu ya akhera bali wamesoma pia secular education.

Sasa changanya hizo sababu hapo na joto la uchaguzi linalokuja ndio unakuta safari hii is different kwasababu hata usalama wa taifa wakienda wanakuta wale informer wao wanawageuka kwani washawaona hawawatakii mema znz ndio mziki ulipo hapo!!!!
 
kuna la ziada huko jaman? maana vikao vimeahirishwa.
ila mwaka huu lazima kieleweke zanziba, wakilowanisha huu msimamo, na kuisikiliza bara lazima visiwa vyake vijitenge au la watapigana sana
 
kuna la ziada huko jaman? maana vikao vimeahirishwa.
ila mwaka huu lazima kieleweke zanziba, wakilowanisha huu msimamo, na kuisikiliza bara lazima visiwa vyake vijitenge au la watapigana sana
Tumeambiwa hali si nzuri kwa jinsi mambo yanavyoenda na mtaalamu wetu mmoja wa haya mambo. Sasa tena sijui kaenda wapi baada ya kutuambia tusubiri for two hours atakuwa tayari na full dataz. Ebu alete ata up to date basi atukizi madukuduku yetu. Lakini wapi kimya.
 
Mkuu kila mara tunapokaribia uchaguzi sarakasi kama hizi huwa zinachezwa, kali kabisa ni ile iliyochezwa na Salmin lakini at the end of the day alikuja kutoa chozi mwenyewe. My meaning is nothing substantial is going to happen,

Mkuu nakubaliana nawe kabisa hizi ni sarakasi tu na si ajabu kutakuwa hakuna kipya hasa ukitilia maanani kwamba katika vikao vilivyopita vya kamati kuu chini ya uenyekiti wa Kikwete hakukuwa na maamuzi yoyote ya maana ndani ya CCM au Tanzania....lakini tusubiri tuone kitakachojiri huko labda kinaweza kubadilisha mengi katika siasa za Bongo.
 
mmmh kwa haya yote useme hakuna kitu substantial?aaah wapi kuna kitu kikubwa kinakuja....sio kawaida mbona haya hayakuwa yanatokea wakati wa Mkapa au Mwinyi au Nyerere??
Naomba hapa tuache ushabiki usiokuwa na maana kinachotakiwa ni kujadili nini cha kufanya kama sisi taifa la leo,ni ushauri gani unatakiwa kutoa na kama ni wewe ungekuwa kwenye position hiyo ungefanya nini, lakini sio kusema kuna kitu kikubwa kinakuja basi kitaje tukijadili hapa na tukitafutie tiba.Kumbuka watoto wetu na wadogo wetu i mean new generation tunawaandaa vp kukabiliana na haya.
 
Inaonekana watu wengi bado hatujaielewa nguvu ambayo Zanzibar inakuja nayo safari hii

Z'Bar siku zote ina nguvu na inakuwa ni mwamuzi wa mambo mengi ya CCM. Naweza kusema Nguvu ya CCM-Z'bar ndo jeuri ya CCM-Tanzania.

Tatizo ni amri ya majeshi yanayopelekwa huko Zenj, hata kunapokuwa na tatizo la kisiasa. Jeshi linatumika kama tishio.

Je, mara hii ikitokea Jeshi litapelekwa? Na hasa kama Karume atakuwa M-Z'Bar maana mara nyingi Viongozi wa ngazi za juu huko hujiona kwamba usalama wao uko Bara.
 
- Well...according to more dataz ni kwamba:-

1. Muungwana aliitisha kikao cha leo CC, lakini kusikia hivyo Karume naye akaitisha kikao maalum leo huko Zanzibar kwa makusudi akijua kwamba leo pia ni siku ya CC DSM.

2. Wajumbe wa CC leo walikuwa wakifahamishwa kwa simu kwamba kikao kimeahirishwa mpaka baadaye watakapojulishwa, as opposed na katiba ambapo wajumbe huarifiwa rasmi kwa maandishi.

3. The dataz ni kwamba "muafaka wa siri" Seif na Karume, una kipengele kinachomtaka Karume kutohudhuria kikao cha ina yoyote kiwe cha CCM, au serikali upande wa bara!

(......itaendeelea.......stay...tuned...! ..tabia yetu ni ile ile kuwawahi hawa CCM na habari zao nyeti maana bila hivi huwa hawazisemi.....)

Respect.

FMes!
 
Mhhh! Nani zaidi kati ya miamba hii miwili...kweli siasa mchezo mchafu. Kama kikao kimeahirishwa kutokana Karume kuitisha kikao Zenj basi round ya kwanza Karume kashinda kwa ushindi laini kabisa, sasa tusubiri round zinazokuja na hapa lazima apatikane msindi hakuna sare hapa.
 
kuna tetesi kwamba msekwa yupo zenji kuongea na karume.Huyu jamaa inaonekana hapati usingizi kipindi hiki.
 
That is your take, jaribu kujiuliza kiutu uzima wiki iliyopita kulitakiwa kufanyike kikao cha NEC Dodoma wajumbe wa Zanzibar wakagoma kuja kuwa wana kikao cha wawakilishi si kawaida yao kwanza si wawakilishi wote ambao ni wajumbe wa NEC.

Kikaitishwa kikao cha dharura cha CC-CCM Dar es salaam vile vile wajumbe wa zanzibar wakagoma bila kutoa sababu usiniulize kwa hili sijui kitu ambacho si cha kawaida kikao cha CC kimeahilishwa ghafula, kuona hivyo CCM bara wakamtuma Msekwa kuwafuata Zanzibar kujua kulikoni wewe bado unasema hakuna chochote.

Kwa mtazamo wa kawaida tu hii sinema si ya kawaida kwa CCM na wala tusidharau kwa kusema ni mambo ya kawaida, kama ni kujiridhisha kwa wana CCM ok endeleeni kujiridhisha lakini wenye akili zao wameliona hili na wanajua kuna jambo kubwa linatokea ndani ya CCM.

bila kusahau na kamati ya mwinyi ambayo iliwekewa masharti tafauti na iliokwenda nayo zenji.
 
Naomba hapa tuache ushabiki usiokuwa na maana kinachotakiwa ni kujadili nini cha kufanya kama sisi taifa la leo,ni ushauri gani unatakiwa kutoa na kama ni wewe ungekuwa kwenye position hiyo ungefanya nini, lakini sio kusema kuna kitu kikubwa kinakuja basi kitaje tukijadili hapa na tukitafutie tiba.Kumbuka watoto wetu na wadogo wetu i mean new generation tunawaandaa vp kukabiliana na haya.

Kaka unataka solution wakati tatizo hujalijua bado? Unataka tuwe kama wachina wanatengeneza model ndipo wanakuja kuuliza maswali. Kimsingi ishu ya zanzibar ni ishu ya kwanza kuelewa ni tatizo la zanzibar (nalo ni Muungano na mgawanyiko wa rasilimali) Pili tukishajua tatizo lipo wapi tuje katika solution ya hilo.

Tatizo ni kwamba CCM tangu mapinduzi wameshazoea siasa za mabavu na kulazimishana. sasa la msingi je zitafaa wakati huu wa uwazi na maendeleo ??? To me sina jibu kwakweli. Pengine nashauri tuwaachie wazanzibar na mafuta yao kwani tukinganga nayo yatatutokea puani. Tukiwaachia nadhani wakija kuboronga tutakuwa na hoja nzuri ya kusema kwanini muungano ni muhimu kwao venginevyo tutakuwa tunapalilia moto
 
- All right, the more dataz ni kwamba Muungano uko kwenye life support, wanaomfahamu Karume kwa karibu sana wanadokeza kwamba hataki Muungano, wanasema hivi karibuni katika kikao kimoja cha Jumuiya, aliwakoromea sana Burundi na Rwanda, kwamba kwa nini wanataka kurudia makosa ya baba yake ya kujiingiza kwenye Muungano na mataifa makubwa, na kwamba baba yake alifanya makosa makubwa sana kujiingiza na bara kwa sababu siku zote miungano ya taifa kubwa na dogo, huishia kuumiza taifa dogo to the shock ya wasaidizi waliokua naye!

- The dataz ni kwamba katika moja ya kikao cha siri kati ya Seif na Karume, waliwekana sawa kwamba, wao wawili ndio Zainzibar ya sasa hakuna cha bara wala CCM, at one point Seif anasadikiwa kumuambia Karume, "..mimi nina umma na wewe una dola...sasa....wabara wa nini yakhe....!",
wanaowafahamu wote wawili kwa karibu sana wanasema kwamba wote wawili wanaunganishwa na one principle ya kutoutaka muungano!

- NEC ya mwisho ilipoitishwa Karume hakuja kwa kisingizio cha kwenda kutibiwa nje, this time ameamua kuita kikao maalum huki visiwani siku ya kikao cha CC bara, pamoja na kwamba amearifiwa toka last weeek!

- The more dataz ni Kigogo mmoja wa CCM (jina tunatunza), aling'amua mapema kwamba huko visiwani kuna something fishy, akamfahamisha Muungwana na nini cha kufanya, yaani kumuita Karume mara moja Dodoma kwa siri na kumkalia kooni, Muungwana kwa kutotaka kuonekana anafuata fuata ushauri tu wa wengine na sio maamuzi yake mwenyewe, akaukataa ule ushauri na kuamua yeye binafsi kuitisha kikao cha CC na NEC kule Dodoma, Karume akachomoa na kwenda nje kutibiwa!

- Now to make this dataz story interesting, comes the main man the one and only Rostam in the picture!

......stay....tuned....!

Respect.

FMEs!
 
- All right, the more dataz ni kwamba Muungano uko kwenye life support, wanaomfahamu Karume kwa karibu sana wanadokeza kwamba hataki Muungano, wanasema hivi karibuni katika kikao kimoja cha Jumuiya, aliwakoromea sana Burundi na Rwanda, kwamba kwa nini wanataka kurudia makosa ya baba yake ya kujiingiza kwenye Muungano na mataifa makubwa, na kwamba baba yake alifanya makosa makubwa sana kujiingiza na bara kwa sababu siku zote miungano ya taifa kubwa na dogo, huishia kuumiza taifa dogo.

- The dataz ni kwamba katika moja ya kikao cha siri kati ya Seif na Karume, waliwekana sawa kwamba, wao wawili ndio Zainzibar ya sasa hakuna cha bara wala CCM, Seif alimuambia Karume, "..mimi nina umma na wewe una dola...sasa....wabara wa nini yakhe....!",
wanaowafahamu wote wawili kwa karibu sana wanasema kwamba wote wawili wanaunganishwa na one principle ya kutoutaka muungano!

- NEC ya mwisho ilipoitishwa Karume hakuja kwa kisingizio cha kwenda kutibiwa nje, this time ameamua kuita kikao maalum huki visiwani siku ya kikao cha CC bara, pamoja na kwamba amearifiwa toka last weeek!

- The more dataz ni Kigogo mmoja wa CCM (jina tunatunza), aling'amua mapema kwamba huko visiwani kuna something fishy, akamfahamisha Muungwana na nini cha kufanya, yaani kumuita Karume mara moja Dodoma kwa siri na kumkalia kooni, Muungwana kwa kutotaka kuonekana anafuata fuata ushauri tu wa wengine na sio maamuzi yake mwenyewe, akaukataa ule ushauri na kuamua yeye binafsi kuitisha kikao cha CC na NEC kule Dodoma, Karume akachomoa na kwenda nje kutibiwa!

- Now to make this dataz story interesting, comes the main man the one and only Rostam in the picture!

......stay....tuned....!

Respect.

FMEs!

Yap hilo nilisikia nikiwa znz na ndio maana nikasema jamaa wamejipanga kisomi kama ukirudia thread ya nyuma
 
Back
Top Bottom