Iwapo CCM wangekubali matokeao halali ya uchaguzi uliofanyika huko Zanzibar mwaka 1995 au yale ya 2000, huenda sasa hivi wasingekuwa na presha na siasa za zanzibar kabisa; kwanza huenda CUF ingeshindwa kudeliver katika kipindi cha kwanzana na kutupiliwa nje katika uchaguzi uliofuata. Sasa hivi walichokutana nacho ni mwiba mkali sana kwao. Karume anataka abakie madarakani, wakati Hamadi naye anataka angalau naye awepo madarakani kabla ya siku zake za kisiasa hazijaisha: yuko ukingoni sasa. Karume anajua kuwa Katiba haimruhusu, na Hamadi anajua kuwa hawezi kuyapata kwa njia ya uchaguzi. Jawabu wote wamelipata, Karume ameahidi kumpa Hamadi madaraka kikubwa katika serikali yake kama tu Hamadi huyo atamsaidia Karume kubaki madarakani.
Kati ya Hamadi na Karume, nadhani kuwa Karume ni smart sana kwani sasa hivi anamtumia Hamad kuwa mpiga debe mkuu. Hakuna uhakika iwapo Karume atampa kweli hayo madaraka akishakubaliwa kuendelea kubaki madarakani.
Zanzibar kuna ugonjwa mkali sana wa madaraka; kila inapofikia mwisho wa kipindi cha uraisi, lazima ziwepo mbwembe za kutaka kumuongezea muda. Nakumbuka hata wakati wa Mwinyi anamaliza mkataba wake wa kupanga kwenye lile jumba la magogoni, ngoma ndogo ndogo zilianza kupigiwa kumtaka aendelee na madaraka, lakini mchonga akingilia kati.
- Wanaoingia kwenye hiyo kamati kuu siku zote hwua wanasema kwamba katika ishu inayowaudhi sana wajumbe wa hii kamati ni hii ya kuongeza muda, katika kamati hii hii Salmin alimtaka Mwalimu kufafanua nini maana ya yeye kuendelea na kofia moja na sio kuachia zote mbili mara moja, ni kamati hii hii juhudi za Kolimba RIP, kutaka Mwinyi apewe term ya tatu zilipiga mwamba na kuishia kung'olewa ukatibu, na ni kamati hii hii juhudi za Mkapa kutaka term ya tatu ziliuliwa na Sumaye tena kwa ukali sana, again ni hii hii kamati kuu ilimuadhibu vikali Salmin na juhudi zake za kutaka term ya tatu,
- Kwanza walimshangaa sana na infact, waliamua kumtoa hata mgombea wake Dr. Bilali na kumpa mgombea aliyeshindwa Amani Karume according to mjumbe mmoja hii ilikuwa ni hasira ya wajumbe dhidi ya Salmin na hii idea ya term tatu, sasa kwa nini Karume anaamini kwamba he is defferent? Salmin alikua na a very strong case on his side kwamba ni yeye peke yake ndiye mwenye kuweza kuwathibiti CUF, lakini CC wakamtupilia mbali sana, na huyu naye naamini wataishia kumtupilia mbali sana, infact Salmin alitishiwa na wajumbe wengi kwamba wako radhi kumpa Seif urais, kuliko kumpa term tatu Salmin!
- Zanzibar wana tabia ya kutishia nyau, na wanafahamu sana kwamba maamuzi ugly ya kuwahusu huko Visiwani huamuliwa na wajumbe wa CC bila kumhusisha rais, makamu wala waziri mkuu, au Rais wao maana mara ya mwisho kwenye kumtwanga Salmin na term zake tatu, Mwenyekiti wa CCM Mkapa aliombwa kutoka nje ya kikao ili wamshugulikie kikamilifu, Karume naye ataishia kilio cha mbwa tu, tena very soon kule Chimwanga!
- Sio siri kwamba recently Karume amekuwa akijaribu sana kuwa a political genius, lakini kule CC wazee kina Almeir, Khatibu na Balozi Idd, wako kimya wanamuangalia tu watch siku yake itakapofika!
Respect.
FMEs!