Kikao cha wabunge wa CCM na kamati ya Mwinyi Dodoma

Unaposikia Jk analalamika kuwa kunamakundi usifikiri mchezo. Sasa kama Jk analalamika na mwanakijiji wa kawaida kule KINTINKU atafanyaje? ndo maana wameona wamteuwe mwinyi na wazee wengine waokoe jahazi linalozama. Nakumbuka wakati wanatwaa madaraka walisema wazee wapumzike wawapishe vijana wafanye kazi. sasa yamewatokea puani wamewakumbuka! inashangaza
 
Date::11/4/2009Kundi la Lowassa lajitokeza kwa nguvu kamati ya Mwinyi*Yumo Naibu Waziri, wapinga ufisadi wataka watuhumiwa wang'olewe CCM

Daniel Mjema, Dodoma
Mwananchi

WABUNGE wa CCM wameendelea kuparurana mbele ya kamati ya Rais Mstaafu, Ali Hassan Mwinyi, huku baadhi wakimtetea aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa na wengine wakisema watuhumiwa wote wa ufisadi wavuliwe nyadhifa za ndani ya chama.

Mvutano huo umetokea wakati kuna malumbano makali yanayoendelea baina ya wabunge na Mkurugenzi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) juu ya kuwahoji (wabunge) kuhusu kupokea posho mbili kwa kazi moja.

Hii pia ni muendelezo wa malumbano yaliyopo kuhusu utekelezaji wa maazimo ya Bunge juu ya hatua za kuwachukulia maafisa waliotuhumiwa kuhusika na kashfa ya zabuni tata ya kampuni ya kuzalisha umeme wa dharura iliyotolewa kwa Kampuni ya Richmond.

Mjadala huo mkali ulioanza saa 2:00 usiku hadi saa 7:30, huku baadhi ya wabunge wakichachamaa na kutaka baadhi ya vigogo ndani ya chama hicho wanaotuhumiwa kwa ufisadi wang’oke.

Hata hivyo, inadaiwa kuwa kundi linalomtetea Lowassa lilijibu mapigo kwamba, hakuwa na makosa na mambo aliyotuhumiwa nayo yalitungwa kwa sababu ya wivu na uchu wa madaraka na kama njia ya kumwondoa katika nafasi yake.

Naibu Waziri wa Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana, Dk Makongoro Mahanga na Mbunge wa viti maalumu, Bernadeta Mushahushu waliiponda ripoti ya Richmond kuwa iliandaliwa kummaliza Lowassa kwa wivu na uchu wa madaraka wa baadhi ya wana-CCM.

Dk Mahanga ambaye ni Mbunge wa Ukonga, alisema ripoti hiyo ni feki huku akipendekeza Rais Kikwete aunde tume huru kupata ukweli akidai kuwa Lowassa alionewa.

Wabunge waliitaka CCM iache kukumbatia viongozi wasio waadilifu na kutaka wote walio na tuhuma wajiengue au waenguliwe ili kurejesha imani ya Watanzania kwa CCM na Serikali.

Habari za uhakika kutoka ndani ya kikao hicho kilichofanyika katika Ukumbi wa Pius Msekwa, zimeeleza kuwa mbunge wa kwanza kuwasha moto alikuwa Christopher Ole Sendeka wa Jimbo la Simanjiro.

Inadaiwa kuwa mbunge huyo machachari alitaka Mbunge wa Igunga, Rostam Aziz, Mbunge wa Bariadi Magharibi, Andrew Chenge na Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa wawajibishwe kutokana na kuhusishwa na tuhuma mbalimbali za ufisadi.

Lowassa na mawaziri wengine wawili walilazimika kujiuzulu nyadhifa zao kutokana na kuhusishwa na kashfa katika mchakato wa Richmond.

Chanzo cha habari kimeeleza kuwa mbunge huyo alitaka pia kuenguliwa kwa Katibu Mkuu wa CCM, Yusuf Makamba kwa kushindwa kusimamia chama kimaadili.

“Ole Sendeka alienda mbali na kusema pamoja na nia nzuri ya serikali ya JK kupambana na ufisadi, Makamba haonekani kuguswa na tatizo hilo," kilidai chanzo hicho.

Katika kikao hicho cha faragha, Mbunge wa Sumbawanga, Paul Kimiti aliwashutumu wabunge ambao ni wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM (Nec), kwa kushiriki kumdhalilisha Spika wa Bunge, Samuel Sitta katika kikao chake kilichofanyika hivi karibuni.

Alisema Sitta ni kiongozi mahiri anayeliongoza Bunge kwa mujibu wa sheria na kanuni zilizopo na kumshutumu Mbunge wa Bahi, William Kusila kwa kitendo chake cha kumwita Spika kuwa ni laini.

Kimiti alisema kama Nec ingemnyang’anya Spika kadi ya CCM na kumwondoa kwenye uspika, basi kauli ya Baba wa Taifa, hayati Mwalimu Julius Nyerere kuwa kusambaratika CCM kungeleta upinzani wa kweli na kwamba hapo ndipo chama imara cha upinzani kingezaliwa kutoka CCM.

Kwa upande wake, Mushashu aliwabeza Wabunge wanaoitwa wapambanaji wa ufisadi na kudai kwamba vita ya ufisadi ni sera ya CCM na sio sera ya wabunge hao wachache.

Alidai wabunge hao hawajatumwa na CCM na kutaka wawajibishwe na kumshutumu mmoja wa wafanyabiashara nchini (jina tunalo) na vyombo vyake vya habari kwa kushirikiana na kundi hilo.

Mbunge wa Kalenga, Stephen Galinoma alilipongeza kundi hilo la wabunge wapambanaji wa ufisadi na kusema lengo lao ni takatifu na kumpongeza Sitta kwa kuliongoza Bunge kwa viwango.

Kwa upande wake, Mbunge wa Longido, Michael Lekule Laizer alisema CCM kimepoteza maadili na kuna ubaguzi ulioanza kujengeka ndani ya chama.

“Kuna ubaguzi ndani ya chama katika kushughulikia wanachama wake…viongozi wanakaa kimya katika masuala ya msingi ya wananchi na kuwafanya wapoteze imani na serikali,” chanzo chetu kilimkariri mbunge huyo.

Mbunge huyo alipendekeza kuwa viongozi wote wanaokabiliwa na tuhuma mbalimbali wapokonywe nyadhifa zao ndani ya CCM, kwani kuendelea kuwepo kwao kunakipaka matope chama.

Chanzo chetu cha habari kimepasha kuwa mbunge huyo alitahadharisha kuwa kama hatua za haraka hazitachukuliwa, CCM itagawanyika makundi mawili.

Alifafanua kuwa, mgawanyiko huo utatokea kwa kuwa kila kundi linaonekana kutoyumba katika misimamo yake, jambo ambalo ni la hatari sana katika mustakabali wa chama.

Kamati hiyo ya Mwinyi iliundwa na NEC ya CCM katika mkutano wake mjini Dodoma hivi karibuni, ili kuchunguza kiini cha mpasuko miongoni mwa wabunge wa CCM hali ambayo inatishia mshikamano wa chama hicho na serikali yake. Wajumbe wengine wa kamati hiyo ambayo imekwishahoji makundi mbalimbali ya wabunge na wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar ni Makamu Mwenyekiti wa CCM, Pius Msekwa na Abdulrahman Kinana.
 
Haya ni yale yale ya kila siku so hakuja jambo jipya hapa.
 
tatizo kubwa hapa ni kuwa hata hao wanao taka jamii iwatambue kuwa ni watu safi kweli si wasafi kiasi hicho wengi wao ni tatizo la ukosefu wa nafasi walizo dhani ni wao tu ndio wanao stahili
 
JK chama chake kimeishamshinda na sioni kama Mzee Mwinyi na Kamati yake watakuja na lolote la maana. Tatizo ni kwamba watuhumiwa wakuu wa ufisadi ndani ya chama ndo walikuwa key players wa kumuingiza JK Ikulu, je, ataweza kuwageuka?

Hoja ya vita ya ufisadi inapewa nguvu na hao wanaojiita wapiganaji na ndio angalau inampa nguvu JK kwamba kuna wabunge wa chama chake wanapambana na ufisadi. Tatizo la hao wapiganaji hawana nguvu ndani ya Chama, na hivyo kuwatema inaweza kuwa rahisi sana, lakini hawawezi kutemwa sasa hivi kwa kuwa CCM ikifanya hivyo itakuwa inajimaliza yenyewe.

Ngoma inamrudia JK mwenyewe, aamue kusuka ama kunyoa? Maana alitegesha bomu kwa akina Mwinyi ili yeye (JK) asije akaonekana ni mtu mbaya bali ni mapendekezo ya Kamati ya Mzee Mwinyi.

Pamoja na hayo mapendekezo (ripoti) ya Kamati ya Mzee Mwinyi itajadiliwa kwenye CC kabla ya kupelekwa kwenye NEC. Ndani ya CC mafisadi wana nguvu na hata ndani ya NEC mafisadi yana nguvu, je, watakubaliana na report ambayo itakuwa against mafisadi?

Hapa naona CCM wana buy time tu kusubiri uchaguzi wa 2010. Kuna watu watachinjwa kwenye kura za maoni na ndio itakuwa imetoka na ndiyo maana serikali imeendelea kudai kwamba watakata rufaa ya mgombea binafsi, lakini mpaka leo hakuna lolote walilofanya, maana wanajua wakipitisha sheria ya mgombea binafsi basi wale ambao watakaochinjwa na CCM kwenye kura za maoni wataamua kwenda solo (independent candidate) na inawezekana wakaenda solo huku wakiwa na support kubwa kutokana na jinsi ambavyo wao wamekuwa wakijipambanua na mafisadi.

Wakati wa kusuka ama kunyoa umewadia, JK amua moja uko na mafisadi ama uko na wale wanaojiita wapiganaji? Hapo lazima kichwa kimuume, maana aliona yaliyotokea kwenye NEC, lakini pia akaona jinsi wananchi walivyopigia makelele ujinga ulioendelea kwenye NEC hiyo pamoja na maamuzi ya NEC ambayo baadaye walianza kufafanua na mengine kuyakana.
 
Back
Top Bottom