Kikao cha wanaume: Njooni mnipe ushauri

Benaya-

JF-Expert Member
Joined
Jul 31, 2019
Posts
4,415
Reaction score
7,631
Wanaume, mabaharia na vijana;
Nimewaita hapa niwaulize jambo kwani kuna jambo linanitatiza.

Wakuu huwa naona wanaume wenzangu kila sketi ikipita mbele yao wanaikodolea macho na wengine hufika mbali hata kupiga mluzi au hata kuomba namba kwa ajili ya kuanzisha mahusiano.
Au sehemu za kazi hupenda kujihusisha kimapenzi na kila msichana/ mwanamke.

Na wengine husema haiwezekani kabisa kuwa na urafiki na msichana bila kutaka sex.

Kwangu mimi ni tofauti sana.
Nina bahati ya kuwa karibu sana kikazi au hata urafiki na warembo wengi sana.
Nina uwezo wa kutengeneza uhusiano kwa muda mfupi..I mean uhusiano wa kawaida.
Lakini linapofika suala la mapenzi mimi ni mchaguzi mno.
Ili msichana anivutie kimapenzi lazima awe na sifa za ziada sana.
1. Mrefu kiasi
2. Rangi sio mchaguzi sana
3. Shepu ..hiki kigezo muhimu mno
4. Ucheshi kiasi
5. Napenda mwanamke mwenye akili na sio
Akina mwajuma wa mipasho.
6. Lips zilizojaa kidogo.

Hivi hili ni tatizo?
Lakini nikipenda hufa na kuoza.
Huwa naingia mwili na roho.
Napenda mapenzi ya kumbikumbi.

Je! Wazee mnawezaje kuwa na foleni au chovya hapa na pale?
Karibuni...povu muhimu
 
Nimekusoma...sasa fanya hivi, tafuta kifaa muafaka oa kabisa achana na biashara chovya chovya...utapata sio korona tu ,na ukimwi ndugu yangu...huu ndo ushauri kutoka kiumeni
Ukisoma vizuri...tatizo langu ni uchaguzi kupitiliza
 
Ukisoma vizuri...tatizo langu ni uchaguzi kupitiliza
Sasa sikia..hakuna, nasema hakuna mkamilifu dunia hii labda uende pluto kama wanaishi viumbe huko. We tafuta ambaye 'angalau' ....! Lkn eti awe ana akili halafu awe na shepu hapo hapo...aah ndg huyo utamtafuta kwa tochi. Huku mjini waliopo ni wenye shepu kichwani ziro...hlf wapo wenye akili lkn hawana shepu...hapo amua mwenyewe unataka nini?
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…