Kikao changu na makampuni ya simu kuhusu kesi ya kuibiwa vifurushi

Na Azam tv waunganishe kwenye kesi ya msingi. Unalipia kifurushi wanachokuuzia elfu 20. Labda nikalipia leo tarehe 16/11. Kesho nijazima tv,nikasafiri kwa matatizo. Nikawa huko mpaka tar 17/12. Kufungulia tv wanakuambia kimekata. Yaani wamekwapua Tsh. 20,000 bila mimi kuitumia
 
Sijui kama nimeshindwa kukuelewa vizuri ama la.. Ila kama nimechelewa vizuri ni kuwa kampuni ambayo hujafanikiwa kukutanishwa nayo ni Hallotel

Ila naona kama mrejesho unaoutoa ni Yale uliyoongea na Aitel tu.. KWA maana hiyo ndio kampuni umeitaja kwenye huu mrejesho.
 
Hongera sana mkuu,mambo yote uliyo orodhesha ni ya msingi sana.Mimi naamini mambo yapo kama yalivyo kwa sababu ya wizi.Nadiriki kusema kwamba si bahati mbaya kwamba yako hivyo,yamefanywa yawe hivyo ili waweze kutuibia.Kifurushi nilichonunua kwa hela zangu iwe ni MB au dakika za maongezi kita-expire vipi.Hii ni lugha ya kitapeli.Ni mikakati tu ya wizi.

Ni wakati muafaka sasa kwa TCRA kuchukua hatua stahiki na haraka,tumeibiwa mno.
Mimi tayari una signature yangu mkuu.
 
Mkuu asante sana kwa kutumia elimu yako
Hongera sana kama tulivyojadilana WhatsApp, nitakua shahidi na kwamba unaweza kutumia ile HUKUMU yangu dhidi ya Tigo ambapo niliwashinda...
Mkuu asante sana na hongera sana kwa kutumia elimu yako kwa Manufaa ya umma.Nitaweka sahihi yangu.
 
Wasije kukununua tu! Endelea na moyo wako huohuo.
 
Hao TCRA walikupataje hadi kukutumia ujumbe mkutane?!

Nilidhani humu tuko salama, nashangaa ulipisema uliweka bandiko humu kisha TCRA wakakutumia message mkutane, au uliweka na number zako?!

Nataka kujiondoa wasiwasi.
Kwani hujaona namba zake hapo juu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…