Kikao changu na makampuni ya simu kuhusu kesi ya kuibiwa vifurushi

Kikao changu na makampuni ya simu kuhusu kesi ya kuibiwa vifurushi

Mkuu asante sana kwa jitihada zako.

Niko tayali kuweka saini mambo yakiwa tayali.
Kwa kuongezea hata menyu zao za kutuuzia bidhaa zimejaa ujanjaujanja mwingi hasa hao voda.

Suala la kumlinda mtumiaji katika bei zao haliko wazi....niko tayali kama utahitaji tuje tuwachambue kama karanga - hawachomoki hao labda nguvu ya pesa itushinde lakini TCRA wakiweka fair play hawachomoki.
 
Hao TCRA walikupataje hadi kukutumia ujumbe mkutane?!

Nilidhani humu tuko salama, nashangaa ulipisema uliweka bandiko humu kisha TCRA wakakutumia message mkutane, au uliweka na number zako?!

Nataka kujiondoa wasiwasi.
Huwa unacomment kabla ya kusoma ama,jamaa ameweka no ya sim kabisa halafu ww unauliza wamempataje like serious?!
 
Kwa kuongezea, unapopigiwa simu na mtu data zako zisitumike kwasababu sio wewe uliyepiga, lakini huwa nashangaa nampigia mtu simu tunaongea baada ya muda, Simu yake inakata. Anaweza kukutumia ujumbe kwa simu nyingine DATA ZIMEISHA.

Mimi ndiye nimepiga sasa hiyo mitandao yao inatumia data mara mbili kwa mpigaji na aliyepigiwa?!

Na kwanini ukiwa na voda uka mpigia mtu wa tigo dakika zinaliwa sana?! Nchi moja hii connection fee inatoka wapi?!
Hili la data kuisha wako sahihi. Una maana simu yenye kutumia Internet? Kama jibu ni ndiyo basi mnatakiwa wote muwe mmeunganishwa kwenye Internet. Hivyo data za yeyote yule zikiisha simu lazima ikate
 
Safi Sana utawaokowa watu wengi ambao tunaumia moyoni tu hatuna sehemu la kupeleka,hapa Sasa nimeamini wanasheria ni wasomi mnahaki kujiita wasomi na Mimi nawaunga mkono kuwa wanasheria ni wasomi.
 
Angalia wasiaze kukuhonga maana umewavua nguo teyari,kwa hiyo wanaweza kukupa mkwaja mrefu ukatusahau na sisi huku katika haki.
 
JAMBO LA SITA

wateja tunaumizwa unapiga simu kabla ya kupokelewa huku bado simu inaita unakuta pesa zako zimeanza kukatwa. Nakumbuka kuna siku nimepiga simu nimesubiri dakika 200 yaani dakika takribani 3 ndio ikapokelewa. Muda wote wa dakika 200 umechukuliwa wakati nilikuwa sijaanza kuongea na simu haikupokelewa. Huu ni wizi mwingine.
 
Hizi ndizo kesi ambazo natamani kuiona TLS, LHRC na wana harakati wengine wanapaswa kuongeza nguvu kwa maslahi ya wananchi. Ubarikiwe sana katika taaluma yako badala ya wale wanasheria wanaotetea mabeberu.
Nami naomba kuunganishwa katika kesi hii.
 
Utapata sahihi yangu.
Pia angalia utaratibu wa ama kumpeleka mahakamani mheshimiwa Rais kwa kuvuruga mfumo wa uendeshaji wa nchi kwa kuvuruga uchaguzi wa serikali za mitaa
 
Mkuu tuwaanishie na bodi ya mikopo nipo tayari kukuchangia nauli.
 
Hongera sana mkuu,utatusaidia watanzania wengi,hayo makampuni yamekaa kinyonyaji sana
 
Yaan vodacom mm vodacom ni wahuni. Lain yao nimeipack tu.

Mkuu, Mwenyezi Mungu akuongozi hili jambo lifanikiwe. Nitakua miongoni mwa watakaoweka sahihi endapo wa mikoa jiran na Dar utatufikia.
 
Back
Top Bottom